19-135: Ninyi mnaomcha Bwana, mhimidini Bwana.

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

 

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

http://tgvs.org/archives/2332   

 • (a) 19-135: Ninyi mnaomcha Bwana, mhimidini Bwana.
 • (b) Jamii: Zaburi
 • (c) Mfululizo: Biblia Sura kwa Sura

 

NINYI MNAOMCHA BWANA, MHIMIDINI BWANA. 

MUHTASARI WA SURA

 • (a) Wahusika: Bwana, watumishi Wake
 • (b) Tabia ya Mungu: Wema (135:3)
 • (c) Fungu Kuu: Zaburi 135:19 – 21
 • (d) Neno Kuu: Ibada / Sifa/ Himidi
 • (e) Msisitizo: Kumwabudu Baba “katika roho na kweli”.

 

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu. Jina Lako litukuzwe milele. Asante Bwana kwa nafasi nyingine ya uhai. Asante kwa zawadi ya Neno Lako. Kabala ya kuanza kipindi hiki, tunaalika uwepo Wako, Bwana. Tunaomba Roho Mtakatifu, katika tafakari ya somo hili, atukirimie hekima ya utambuzi wa sauti Yako na nguvu ya kuitii. Tusaidie kufanya uamuzi wa busara, kila wakati, kuachana na dhambi, tukikuchagua Wewe na kuuchagua wokovu. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tubadilishe ili tufanane Nawe. Bariki kila mmoja Bwana. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!


 

UTANGULIZI:

Mtunzi wa Zaburi hii hajatajwa bayana. Zaburi 135 na 136 zinahitimisha nyimbo kuu za “Hallel” ziilizo anza kuanzia sura ya 120 = [the “Great Hallel]. Zaburi 135:15–20  ina uhusiano wa karibu sana na Zaburi 115:4–11.

“Zaburi 135 na 136 ni kama  jozi ya mapacha wanaofanana. Zote ni Zaburi yatima, lakini yatima gani?. Hapa tuna mayatima wawili walio na furaha zaidi duniani.  Lisifuni Jina la BWANA… Msifuni BWANA… Kutoa sifa kwa Bwana… Mhimidini BWANA… Mshukrani kwa BWANA!” Hizo ndizo mada kuu za Zaburi hizi mbili.”

“Pengine ziliandikwa na Hezekia katika furaha na mfuriko wa nafsi yake baada ya ukombozi wake mara mbili — kwanza kutokana na ugonjwa, pili kutoka kuzingirwa na maadui wake. Hata hivyo, utafiti wa kina wa Zaburi hii haisemi hivyo. Roho Mtakatifu anapendelea Zaburi hizi mbili zisimame pekee “bila ya baba au mama, bila ya mwanzo wala mwisho wa siku” — kama Melkizedeki, hivyo kusema, kutokuwa na ukumiliki baba lakini Mungu (Waebrania 7:3). ” [John Phillips, Exploring Psalms, Volume Two, Psalm 135]

 

 

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU:

Mada kuu katika Zaburi 135 ni Ibada. Kwanza tuna:

 1. Ibada yenye Sifa (135: 1 – 2)
 2. Ibada yenye Akili (135: 3 – 14)
 3. Ibada iliyokufa ganzi (135:15 – 18)
 4. Ibada yenye Msisitizo (135:19 – 21)
 5. Tufanye nini basi na Zaburi hii? = “Ibada”

 

ZABURI 135

1 Haleluya. Lisifuni jina la Bwana, Enyi watumishi wa Bwana, sifuni.

2 Ninyi msimamao nyumbani mwa Bwana, Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu.

3 Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.

4 Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa.

5 Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu, Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.

6 Bwana amefanya kila lililompendeza, Katika mbingu na katika nchi, Katika bahari na katika vilindi vyote.

7 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika hazina zake.

8 Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri, Wa wanadamu na wa wanyama.

9 Alipeleka ishara na maajabu kati yako, Ee Misri, Juu ya Farao na watumishi wake wote.

10 Aliwapiga mataifa mengi, Akawaua wafalme wenye nguvu;

11 Sihoni, mfalme wa Waamori, Na Ogu, mfalme wa Bashani, Na falme zote za Kanaani.

12 Akaitoa nchi yao iwe urithi, Urithi wa Israeli watu wake.

13 Ee Bwana, jina lako ni la milele, Bwana, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.

14 Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumishi wake.

15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu.

16 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,

17 Zina masikio lakini hazisikii, Wala hamna pumzi vinywani mwake.

18 Wazifanyao watafanana nazo, Na kila mmoja anayezitumainia.

19 Enyi mlango wa Israeli, mhimidini Bwana; Enyi mlango wa Haruni, mhimidini Bwana;

20 Enyi mlango wa Lawi, mhimidini Bwana; Ninyi mnaomcha Bwana, mhimidini Bwana.

21 Na ahimidiwe Bwana toka Sayuni, Akaaye Yerusalemu. Haleluya.

 


 

MASWALI MUHIMU KATIKA SURA HII

{Pitia majibu yaliyowekwa hapo chini}

 • (1)   Je, kuna dhambi ya kuepukwa hapa?
 • (2)   Je, kuna dhambi ya kutubu hapa?
 • (3)   Je, kuna ombi la kuomba hapa?
 • (4)   Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
 • (5)   Je, kuna agizo au wajibu wa kufanya hapa?
 • (6)   Je, kuna makosa au mapungufu ya kuepukwa hapa?
 • (7)   Je, sura hii inatufundisha nini kuhusu Mungu?
 • (8)   Je, sura hii ina umuhimu gani katika mpango wa wokovu wetu?

 

MAJIBU YA MASWALI MUHIMU

(1) Ibada ya sanamu, Ibada iliyokufa ganzi (135:15 – 18)

(2) BWANA! Hatujakuabudu kama itupasavyo. Utusamehe BWANA!

(3) Angalia Zaburi 135:19-21

(4) Mtazamo wa Maombi, Sifa na Ibada ya kweli

(5) “Mhimidini BWANA” (Zaburi 135: 19-21). Tukumbuke makundi makuu manne yaliyotajwa mwishoni mwa sura hii (1) Israeli, (2) Haruni, (3) Lawi, na (4) “Ninyi mnaomcha BWANA.” Makundi haya manne yanarejelea taifa kwa ujumla (Israeli), ukuhani (Haruni na Lawi), na waumini/ washiriki/ watu wote (“Ninyi mnaomcha Bwana”).

(6) Kushindwa kutoa ibada sahihi, sifa, au kumhimidi Mungu wetu, au kuwa wasio na shukrani (cf. Warumi 1:21)

(7) Sura hii ina mengi ya kusema kuhusu Mungu. Katika sura hii Mtunga Zaburi ametupa sababu za kutosha za kumsifu Mungu. Kwanza kabisa, tabia Yake (Zaburi 135:3); Uchaguzi wake wa Yakobo (Zaburi 135:4); Uwezo/utawala  Wake katika uumbaji (Zaburi 135:5 – 7); Ukombozi wa Israeli (Zaburi 135:8-12); zaidi kuliko; asili Yake ya kipekee (Zaburi 135:13–18)

(8) Ibada ya kweli [mtazamo na matendo] itatuelekeza moja kwa moja kwa Mwokozi. (Tazama maelezo ya ziada hapo chini)


 

ASILI YA KIPEKEE YA MUNGU KATIKA ZABURI HII (Zaburi 135:13–18)

 • Jina Lake ladumu milele (Zaburi 135:13a)
 • Umaarufu Wake, “katika vizazi vyote” (Zaburi 135:13b)
 • Yeye ni Mwamuzi/ Jaji/ Hakimu Mkuu (Zaburi 135:14a)
 • Yeye ni Mungu mwenye huruma… ” Atawahurumia watumishi Wake ” (Zaburi 135:14b)
 • Yeye ni Mungu wa miungu, (Zaburi 135:15-18)
 • Yeye ni Mungu Mwenyezi, Mwenye Enzi (Zaburi 135:15-18)
 • Yeye ni BWANA, MUNGU!

 

 

MAELEZO YA ZIADA

Yohana 4:23 – 24

 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

 

(KWANZA): Waumini wote wa kweli lazima wamwabudu Mungu katika “roho na kweli.” Yaani, ibada ya kweli inachukua nafasi ya ndani, katika moyo au roho ya huyo anayeabudu (cf. Zaburi 45: 1; 103:1 – 2).

 • Zaburi 45: 1
  • Moyo wangu umefurika kwa Neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia Mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi. 
 • Psalm 45:1 (NKJV)
  • My heart is overflowing with a good theme; I recite my composition concerning the King; My tongue is the pen of a ready writer.
 • Zaburi 103:1 – 2
  • 1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi Jina Lake takatifu. 
  • 2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. 

 

(PILI): Ibada ya kupendeza kwa Mungu lazima iwe ya uaminifu na uwazi, ikitolewa kwa unyenyekevu na moyo safi (cf Zab 24:3 – 4; Isa 66:2).

 • Zaburi 24:3 – 4
  • 3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
  • 4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.
 •  Isaya 66:2
  • Maana mkono Wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo Neno Langu.

 

(TATU): “Kumwabudu Baba Katika Roho Na Kweli”

Kuabudu “katika kweli” huunganisha moyo au “roho ya ibada” na ukweli kuhusu Mungu na kazi Yake ya ukombozi kama ilivyofunuliwa katika nafsi ya Yesu Kristo na katika maandiko matakatifu.

Daudi alielewa umuhimu wa kuabudu katika kweli na uhusiano muhimu sana kati ya “Kweli” na Neno la Mungu wakati alipoandika, “Unifundishe njia yako, Ee Bwana”  (cf. Zaburi 86:11; cf. Zaburi 145: 18). 

 • Zaburi 86:11;
  • Ee Bwana, unifundishe njia Yako; Nitakwenda katika kweli Yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha Jina Lako.
 • Zaburi 145: 18
  • Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.

 

Katika mafungu hayo hapo juu, tunaona maagano yote yanavyokubaliana! (yaani: Agano la kale na Agano jipya). Ibada ya kweli kwa Mungu kimsingi ni ibada ya ndani, ni suala la  moyoni, ni swala la moyo na roho lililo na mizizi katika ufahamu wa na utiifu kwa NENO LA MUNGU lililofunuliwa kwetu katika Biblia.


 

TUFANYE NINI BASI NA SURA HII?

Hebu tukumbuke kumwabudu Mungu daima katika “roho na kweli”.

 

Ibada ya kweli italeta faida zifuatazo kwa watu wa Mungu:

 • (1) Mibaraka
 • (2) Mwongozo
 • (3) Ukombozi
 • (4) Furaha
 • (5) Ufahamu wa uwepo wa Mungu
 • (6) Maana ya kina ya uongozi wa Yesu Kristo
 • (7) Ujasiri wa/ katika kushuhudia
 • (8) Ibada ya kweli yawatia hatiani wenye dhambi

 

Zaburi 50: 14 – 15

 • 14 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
 • 15 Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.

 

KORNELIO = (mfano wa kuigwa)

 • Matendo 10:2  
  • 1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia
  • 2 Mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. 

 

 SAUTI YA INJILI

Hebu sikiliza Sauti ya Mungu ikinena nasi, tunapofunga kipindi hiki.

 • Zaburi 22:23
  • Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni, Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.
 • Waebrania 12:28
  • Kwa hivyo, tangu sisi tupokea ufalme ambayo haiwezi kuyumbishwa, na tuwe na neema, ambayo inaweza tunamtumikia Mungu kifungu kwa heshima na hofu ya kimungu.
 • Zaburi 2:11
  • Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.

 

OMBI LA MTUNGA ZABURI

 • Zaburi 86:11
 • Ee Bwana, unifundishe njia Yako; Nitakwenda katika kweli Yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha Jina Lako.

 

 • Zaburi 145: 18  (AHADI)
 • Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.

 

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu mpendwa, tunashukuru kwa tafakari ya Neno Lako katika sura hii. Twaomba Roho Wako aendelee kutufundisha sura hii tena na tena. Tusamehe tuachane na dhambi zilizotajwa katika fundisho la Zaburi hii. Tukumbushe kukukusifu daima, kukushukuru “kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu wetu katika Kristo Yesu”. Asante Bwana kwa ombi hili fupi. Asante kwa sababu “utatubariki toka Sayuni”.  Tumeomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mkombozi wetu, Amina!


 

The Gospel’s Voice © 2017