Jumatano: 15/3/2017

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

CHUMBA CHA MAOMBI
(a) http://tgvs.org/archives/2330
(b) Jumatano: 15/3/2017
(c) Mada Kuu: Familia, Ajira, Masomo, Miradi, nk.

LEO KATIKA ZAMU YA KUOMBA:
(1) Br. David
(2) Binti Mubarikiwa
(3) Yeyote aliyetayari
CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.

(1) MAGONJWA, MIKOSI, VIFO

(2) DANIEL: Uchumi wake (Ajira); Mke mtarajiwa

(3) MARIA: anga’e katika Jina La Yesu Kristo

(4) UINJILIST: Radio Morning Star & Staff wote

(5) DEVON: Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu

(6) Br. DAVID: Shemeji yangu yu mgonjwa sana, tumkumbuke kwa maombi

(7) WANAKIKUNDI: Ujazo wa Roho Mtakatifu, Upendo, Umoja, Msamaha, Utakaso, na Uaminifu wa Members wote wa kikundi hiki, ili wawe waaminifu katika Kuomba na Kuombea wengine pia.

(8) UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. (Yakobo 1:22)

(9) Tutafakari MAONYO YA YESU; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Luka 21:36)
AHADI YA LEO
Matayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

ANGALIZO:
Tunaweka nadhiri na Mungu wetu kuwa Jukwaa hili litakuwa CHUMBA CHA MAOMBI. Kwa maana nyingine, “CHUMBA CHETU CHA NDANI” (Matayo 6:6). Hivyo basi, ni makosa makubwa kupeperusha Maombi haya katika magroup mengine. Yanayosemwa na kutajwa humu yatabakie humu ndani. Changamoto wanazopitia ndugu zetu katika magroup mbalimbali ni Siri na hayapaswi kupeperushwa hadharani. Yeyote atakayekiuka atajitafutia laana mwenyewe.

Matayo 6:6
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

(1) Kuweka Maombi (Maandishi/ Sauti)

(2) Kutoa ushuhuda wa matendo makuu ya Mungu wetu.

(3) Kuorodhesha changamoto mbalimbali toka kwa ndugu, jamaa, na marafiki.
BWANA ATUBARIKI SOTE.

Matayo 26:41
“Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.