19-134: Mhimidini Bwana, nyote pia

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO
http://tgvs.org/archives/2328 
(a) 19-134: Mhimidini Bwana, nyote pia
(b) Jamii: Zaburi
(c) Mfululizo: Biblia Sura kwa Sura

MUHTASARI WA SURA HII:

(a) Wahusika: Bwana, watumishi Wake
(b) Tabia ya Mungu: Uaminifu
(c) Fungu Kuu: Zaburi 134:1-3
(d) Neno Kuu: Ibada, Shukrani, Sifa
(e) Msisitizo: “Kumhimidi Bwana.”

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu. Jina Lako litukuzwe milele. Asante Bwana kwa nafasi nyingine ya uhai. Asante kwa zawadi ya Neno Lako. Kabala ya kuanza kipindi hiki, tunaalika uwepo Wako, Bwana. Tunaomba Roho Mtakatifu, katika tafakari ya somo hili, atukirimie hekima ya utambuzi wa sauti Yako na nguvu ya kuitii. Tusaidie kufanya uamuzi wa busara, kila wakati, kuachana na dhambi, tukikuchagua Wewe na kuuchagua wokovu. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tubadilishe ili tufanane Nawe. Bariki kila mmoja Bwana. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!


MHIMIDINI BWANA, NYOTE PIA

Zaburi 134

1 Tazama, enyi watumishi wa Bwana, Mhimidini Bwana, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku katika nyumba ya Bwana.

2 Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi Bwana.

3 Bwana akubariki toka Sayuni, Aliyezifanya mbingu na nchi.


MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU:

Kutoa sifa/ Kumhimidi Bwana (134:1 – 2)
(a) Nini (134:1a)
(b) Nani (134:1b)
(c) Lini (134:1 m)
(d) Wapi (134:2)
(e) Nini (134:2a)

Kupokea baraka kutoka kwa Bwana (134:3)
(a) Uwezo wa Bwana (134:3a)
(b) Makazi ya Bwana (134:3b)

Tufanye nini basi na Zaburi hii?


 

MASWALI MUHIMU KATIKA SURA HII

{Pitia majibu yaliyowekwa hapo chini}

(1) Je, kuna dhambi ya kuepukwa hapa?
(2) Je, kuna dhambi ya kutubu hapa?
(3) Je, kuna ombi la kuomba hapa?
(4) Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
(5) Je, kuna agizo au wajibu wa kufanya hapa?
(6) Je, kuna makosa au mapungufu ya kuepukwa hapa?
(7) Je, sura hii inatufundisha nini kuhusu Mungu?
(8) Je, sura hii ina umuhimu gani katika mpango wa wokovu wetu?

MAJIBU YA MASWALI MUHIMU

(1) Kutokuwa na shukrani

(2) Tabia isiyo na shukrani mbele za Bwana

(3) Tazama, enyi watumishi wa Bwana, Mhimidini Bwana (1:1a)

(4) Tabia ya kumsifu Bwana daima. Hebu tuwe kama Walawi katika zamu zao pale hekaluni… “mchana na usiku” (cf. 1 Nyakati 9:33). Maandiko yanasema: “Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.”

(5) Tazama, enyi watumishi wa Bwana, “Mhimidini Bwana, nyote pia.” [134:1] “Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi Bwana.” [134:2]

(6) Tazama Jibu la # 2

(7) Mungu ni mwaminifu katika kutunza ahadi Zake.

(8) Kwa sababu uwepo wa Mungu ulikuwepo katika hema/ hekalu la Sayuni, kutokana na mtazamo wa binadamu, hekalu lingekuwa chanzo cha baraka ya kimungu. Tukumbuke pia kwamba: BWANA ndiye chanzo cha mibaraka yote. Mibaraka katika maisha haya na Mibaraka katika maisha yajayo/ ulimwengu ujao; kwa maana nyingine: Uzima wa Milele.

 

ANGALIZO:

“Painulieni Patakatifu Mikono Yenu” (Zaburi 134:2a)

Huu ulikuwa ni utamaduni wa kawaida kabisa katika Agano La Kale, yaani kutoa sifa kwa “kuinua mikono” (cf. Zab 28: 2; 63:4; 119:48; 141:2; Maombolezo 2:19), utamaduni ambao ulieleweka kistiari katika Agano Jipya (1 Timotheo 2:8).

Zaburi 28: 2;
Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo, Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.

Zaburi 63:4;
Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina Lako nitaiinua mikono yangu

Zaburi 119:48;
Na mikono yangu nitayainulia maagizo Yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako.

Zaburi 141:2;
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

Maombolezo 2:19a
Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa makesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako

1 Timotheo 2:8
Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.


 

TUFANYE NINI BASI NA SURA HII?

Sisi kama waumini twapaswa kukumbuka daima kutoa sifa na shukrani kwa Mungu wetu

Ushahidi wa ki-Biblia:

Zaburi 100:4
Ingieni malangoni Mwake kwa kushukuru; Nyuani Mwake kwa kusifu; Mshukuruni, Lihimidini Jina Lake

Zaburi 107: 22
Na wamtolee dhabihu za kushukuru, na kuyasimulia matendo Yake kwa kuimba.

Wakolosai 1:12
Mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.

Wakolosai 3:15
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

1 Wathesalonike 5:18
Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu..


SAUTI YA INJILI

Sikiliza sauti ya Mungu ikinena nasi tunapofunga kipindi hiki:

Zaburi 134

1 Tazama, enyi watumishi wa Bwana, Mhimidini Bwana, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku Katika nyumba ya Bwana.

2 Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi Bwana.

3 Bwana akubariki toka Sayuni, Aliyezifanya mbingu na nchi.
Zaburi 40: 16

16 Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu Wako waseme daima, Atukuzwe Bwana.

17 Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.

 
OMBI: Baba yetu na Mungu wetu mpendwa, tunashukuru kwa tafakari ya Neno Lako katika sura hii. Twaomba Roho Wako aendelee kutufundisha sura hii tena na tena. Tusamehe tuachane na dhambi zilizotajwa katika fundisho la Zaburi hii. Tukumbushe kukukusifu daima, kukushukuru “kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu wetu katika Kristo Yesu”. Asante Bwana kwa ombi hili fupi. Asante kwa sababu “utatubariki toka Sayuni”. Tumeomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mkombozi wetu, Amina!


The Gospel’s Voice © 2017