89-002: Asili ya hukumu ya Mungu

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

 

MWENDELEZO WA MASOMO YA BIBLIA KUHUSU HUKUMU YA MUNGU

Waebrania 2:1-3

1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.  2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,  3 Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

 

HUKUMU YA MUNGU

Part 2: ASILI YA HUKUMU YA MUNGU

 

Muhtasari wa Mawazo Makuu:

Asili ya hukumu ya Mungu

 • Uhakika wake
 • Haki zake
 • Uadilifu wake

LENGO LA HUKUMU YA MUNGU

 • Kuonyesha utukufu wake
 • Kutenda/ Kulipa haki
 • Kutetea wanyonge
 • Kuleta wokovu kwa watu Wake
 • Kuadhibu dhambi/ wadhambi
 • Kugeuka watu Mungu

HUKUMU YA MUNGU INAWEZA KUCHELEWA


 

OMBI: Baba yetu mwema wa Mbinguni, Jina Lako litukuzwe milele. Tunapokwenda kuangalia somo hili fupi, tunaomba Roho Wako akapate kutuongoza katika tafakari hii. Tukumbushe kua Wewe ni Hakimu Mkuu na unahukumu dhambi. Tunakumbushwa: “Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale?’ Tusaidie kutambua dhambi zetu na kutubu sasa, kabla mlango wa rehema kufungwa. Asante Bwana kusikia ombi hili fupi. Tumeomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo, Amina!

 

ASILI YA HUKUMU YA MUNGU

(1) Uhakika wake

Mhubiri 12:14

13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Soma pia Zaburi 7:11; Mhubiri 3:17; 11:9; Yakobo 5:9

 

(2) Haki Yake

Warumi 2:11 

Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

 

Mwanzo  18:23-26

23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?

24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?

25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.

 

 

Soma pia Zaburi 9:7-8; 50:6; 96:13; 1 Nyakati 16:33

 

(3) Uadilifu  wake

 

2 Nyakati 19:6-7

6 Akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu. 7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.

 

Angalia pia  Torati 10:17; Ayubu 34: 19; Zaburi 98:9; Warumi 2:11; Efeso 6:9

 

 

 

LENGO LA HUKUMU YA MUNGU

 

(1) Kuonyesha utukufu Wake

 

Isa 5:16

Bali Bwana wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki.

 

Kutoka 14:3-4

3 Naye Farao atasema katika habari za wana wa Israeli, Wametatanishwa katika nchi, ile jangwa imewazuia wasitoke.  4 Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi wakafanya hivyo.

 

Isa 59:18-19;

18 Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo. 19 Basi, wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.

 

Soma pia Ezekieli 7:27; 38:23;

 

 

(2) Kutenda/ Kulipa haki

 

Ufunuo 16:5-7

 

4 Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, Uliyeko na Uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili. 7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, NI ZA KWELI, na ZA HAKI, hukumu Zako.

 

 

(3) Kutetea wanyonge

 

Zaburi 140:12

Najua ya kuwa Bwana atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.

 

Isaya 11:4

Bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.

 

Soma Ezekieli 34:16-22

 

 

(4) Kuleta wokovu kwa watu Wake

 

Isa 30:18

Kwa ajili ya hayo Bwana atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana Bwana ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.

 

Kutoka 6:6

Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa

 

Torati 32:36;

Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa

 

 

Soma pia Zaburi 76:8-9; 105:5-16:12; Isaya 33: 22

 

 

(5) Kuadhibu dhambi/ wadhambi

 

Warumi 2:12

11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. 12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.

 

Yohana 12:48

Yeye anikataaye Mimi, asiyeyakubali maneno Yangu, anaye amhukumuye; Neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

 

Yohana 12:48 [Bibilia Takatifu (SNT)]

Mtu anayenikataa na kuyapuuza maneno yangu anaye hakimu; neno nililotamka litamhukumu siku ya mwisho.

 

Waebrania 13:4

Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

 

Waebrania 10:30a

Maana twamjua Yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu Yangu, Mimi nitalipa.

 

Isaya 19:22

Naye Bwana atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa Bwana, atakubali maombi yao na kuwaponya.

 

 

 

HUKUMU YA MUNGU INAWEZA KUCHELEWA/ KUCHELEWESHWA

 

Ufunuo 6:10

Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

 

Ufunuo 6:10  [Bibilia Takatifu (SNT)]

Wakalia kwa sauti kuu wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliye mtakatifu na mwaminifu, utakawia mpaka lini kuwa hukumu na kulipiza kisasi juu ya watu wote waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?”

 

 

Matendo 17:30;

Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.

 

2 Petro 3:9

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

 

Tazama pia  Ayubu 24:1-4; Zaburi 74: 10-11; 94:2-3; Habakuki 1:2-4,13;

 

 

 

 

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

 

Muhubiri 11:9

 

Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.

 

Ufunuo 14:6-7

 

6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,

 

7 Akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.

 

 

 

MAONYO YA YESU

 

Waebrania 10:26-30;

 

26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;

 

27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

 

28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

 

29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

 

30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.

Kugeuka watu Mungu

 

 

 

SAUTI YA INJILI

 

Sikiliza Ahadi/ Sauti ya Mungu ikinena nawe, tunapofunga kipindi hiki:

 

 

Isaya 1:18

 

18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

 

19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; 20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.

 

 

 

MWITIKIO WETU

 

NZK # 171. “HUKUMU”

(The Judgment Has Set)

 

Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale

Apimapo Mungu hakimu kula wazo na tendo?

 

Tutasimamaje sote katika siku kuu ile?

Dhambi zitu zitafutika ama zitatuangusha?

 

Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai,

Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu.

 

Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja,

Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!

 

 

 

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu mpendwa, ninakiri nikisema mimi ni mdhambi. Katika somo la leo, tumejifunza dhahiri kwamba wewe ni Hakimu na hakika utahukumu dhambi. “Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja, Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!” Saidia kila mmoja atakaye soma Injili hii, akate shauri, na kuungama, na kutubu dhambi yake. Hakika ahadi Zako ni za kweli- kwamaba utasamehe uovu wetu. Tusamehe, tusafishe, tutakase, na ukatuhifadhi katika Pendo Lako. Siku ile Hakimu Mkuu atakapokuja, ebu tuwe miongoni mwa wateule wako. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mkombozi wetu, Amina!

 

 

 

 

BWANA ATUBARIKI SOTE!

 

 

The Gospel’s Voice © 2017

 

 

 

 

NITAPATAJE SOMO LA LEO?

 

Mobile App: The Gospel’s Voice (TGV)

 

Waweza sikiliza pia toleo la Sauti kupitia:

 • Facebook: Sauti Ya Injili SDA
 • Whats App: Sauti Ya Injili SDA
 • Kiungo cha TGV Mobile App
 • Kiungo cha Tovuti: tgvs.org

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mungu ni mwamuzi juu viumbe/ au uumbaji wote

Yeye waamuzi dunia Ge 18:25 tazama pia Ps 9:8; 58: 11; 82: 8; 94:2; 96:13; 98:9

Majaji kila 33:20 ya Eze ona binafsi pia Ecc 3:17; Ebr 9:27; 1Pet 4:5; Jude 15; Rev 20:12

Yeye anahukumu Mataifa Yoeli 3:12 Angalia pia Ps 9:19-20; 110:6; OB 15; Zep 3:8

Majaji wakuu wa Isa ya Mataifa 40: 23; Yer 25:17-27; Rev 6:15-17

Majaji watu wake Ebr 10:30 ona pia Dt 32:36; PS 78:62; Yer 1:16; 1Pet 4:17

Majaji malaika 2Pe 2:4; Yuda 6

Majaji Shetani Ge 3:14-15; Mt 25: 41; 1Ti 3:6; Rev 20:10

 

 

Mungu ni mwamuzi juu viumbe/ au uumbaji wote

Yeye waamuzi dunia Ge 18:25 tazama pia Ps 9:8; 58: 11; 82: 8; 94:2; 96:13; 98:9

Majaji kila 33:20 ya Eze ona binafsi pia Ecc 3:17; Ebr 9:27; 1Pet 4:5; Jude 15; Rev 20:12

Yeye anahukumu Mataifa Yoeli 3:12 Angalia pia Ps 9:19-20; 110:6; OB 15; Zep 3:8

Majaji wakuu wa Isa ya Mataifa 40: 23; Yer 25:17-27; Rev 6:15-17

Majaji watu wake Ebr 10:30 ona pia Dt 32:36; PS 78:62; Yer 1:16; 1Pet 4:17

Majaji malaika 2Pe 2:4; Yuda 6

Majaji Shetani Ge 3:14-15; Mt 25: 41; 1Ti 3:6; Rev 20:10

 

 

 

Hukumu ya Mungu ni isiyoepukika

Hakuna mtu anaweza kujiepusha Mungu Ob ona 4 pia ubadilishaji 3:8-9; Ayubu 11:20; Yer 11:11; Ni 9:1-4

 

Mungu anapekua mioyo ya wanadamu Yer 17:10 ona pia 1Ch 28: 9; PS: 7 9; PR 5:21; Yer 11:20

 

Mungu hufunua siri Ro 2:16 ona pia Ecc 12:14; Yer 16:17; 1Co 4:5; Ebr 4:13

 

Mifano ya Mungu kutenda kama Jaji

Hukumu yake ya dunia katika kutuma gharika Ge 6:7, 13, 17; 7:21-23

 

Hukumu yake ya watu Kaini Ge 4:9-12; Anania ya AC 5:3-10 na Sapphira; AC 13:8-11 Elima mchawi

 

Hukumu yake ya familia Jos 7:24-25 ya Akani; 1Sa 3:12-13 wa Eli

 

Hukumu yake ya miji ya Ubadilishaji Jeni 19:24-25 Sodoma na Gomora; Jos 6:24 Jericho

 

Hukumu yake Mataifa Dt 7:1-5 na Mkanaani Mataifa

 

Hukumu yake watawala wa Mataifa 2Ch 26: 16-21 Uzia; Da Nebukadreza 4:31-33; Da 5:22-30 Belshaza; AC 12:22-23 Herode

 

Hukumu yake yake watu Amu 2:11-15; 2Ch 36: 15-20; Isa. 33: 22

 

Tabia ya Mungu ni wazi kupitia hukumu zake za haki

Uhuru wake Ps 9:7; 96:10; 99:4; Eze 6:14

 

Uwezo wake kutoka 6:6; 14:31; Eze 20:33-36; Rev 18:8

 

Utakatifu wake Lev 10:1-3; 1Sa 6:19-20; Eze 28:22; Rev 16:5

 

Hasira yake rangi 1:2-3; RO 2:5

 

Ukweli wake Ps 96:13; RO 2:2; Rev 16:7

 

Wake uadilifu 2Ch 19:7; RO 2:9-11; Safuwima 3:25; 1Pet 1:17

 

Wake huruma La 3:31-33; Hos 11:8-9; Jnh 3:10; 4:2

 

Uvumilivu wake Nu 14:18; Ne 9:30; 2Pe 3:9

 

Rehema yake Ne 9:31; Ayubu 9:15; PS 78:38; Kipaza sauti 7:18

 

Yesu Kristo anaendelea kazi ya Mungu kama hakimu

Yn 5:22 Angalia pia Yn 5:27; AC 10:42

 

Mungu atatenda kama hakimu siku ya mwisho

Rev 20:12 Angalia pia Isa 2:17; Zep 1:14-18; Yn 12:48; AC 17:31; RO 2:16; 14:10; 1Co 4:5; 2Ti 4:1; 1Pet 4:5; 2Pe 2:9; 3:7