89-001: Mungu kama Hakimu

 

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

MWENDELEZO WA MASOMO YA BIBLIA KUHUSU HUKUMU YA MUNGU

 

Waebrania 2:1-3

 • 1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.
 • 2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
 • 3 Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

OMBI: Baba yetu mwema wa Mbinguni, Jina Lako litukuzwe milele. Tunapokwenda kuangalia somo hili fupi, tunaomba Roho Wako akapate kutuongoza katika tafakari hii. Tukumbushe kua Wewe ni Hakimu Mkuu na unahukumu dhambi. Tunakumbushwa: “Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale?’ Tusaidie kutambua dhambi zetu na kutubu sasa, kabla mlango wa rehema kufungwa. Asante Bwana kusikia ombi hili fupi. Tumeomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo, Amina!


 

HUKUMU YA MUNGU

Part 1: MUNGU KAMA HAKIMU

 

Muhtasasi wa Mawazo Makuu:

 1. Mungu ana mamlaka ya kuhukumu
 2. Cheo cha Mungu kama Hakimu
 3. Mungu anaamua Migogoro
 4. Mungu: Mkuu wa mahakama ya Mbinguni
 5. Mungu katika Kiti cha Enzi, Kikubwa, Cheupe
 6. Tufanye nini basi na somo la leo?

 

MUNGU ANA MAMLAKA YA KUHUKUMU

Kwa sababu yeye ndiye Muumbaji wa mwanadamu na viumbe vyote, kwa asili kabisa anayo mamlaka na uhalali wa kutoa hukumu, kama vile baba katka familia awezavyo kuwahukuhumu wanawe.

Tuangalie tu mifano ya kwanza kabisa katika Biblia

 • Mwanzo 3:14 (Hukumu kwa Nyoka)
  • Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
 • Mwanzo 3:15 (Hukumu: Vita Kuu)
  • Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
 • Mwanzo 3:16 (Hukumu kwa Hawa)
  • Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
 • Mwanzo 3:17 (Hukumu kwa Adamu)
  • Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

 

CHEO CHA MUNGU KAMA HAKIMU

 • Zaburi 75:7
  • Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.
 • Zaburi 50:6
  • Na mbingu zitatangaza haki Yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.
 • Isaya  33: 22
  • Kwa maana Bwana ndiye Mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; Ndiye atakayetuokoa.
 • Isaya 66:16
  • Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga Wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.

 

MUNGU ANAAMUA MIGOGORO

Waamuzi 11:27 = (Israeli & Amoni)

 • Basi mimi sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye Bwana, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni.

Mwanzo 16:5c =(Sarai & Abramu)

 • Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.

Mwanzo 31:53 = (Labani & Yakobo)

 • Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu.

1 Samweli 24:15 = (Daudi & Sauli)

 • Basi Bwana atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe na mkono wako

Yakobo  5:9 = (Mwamuzi ni Mungu)

 • Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, Mwamuzi amesimama mbele ya milango.

 

MUNGU: MKUU WA MAHAKAMA YA MBINGUNI

 • Isaya 3:13
  • Bwana asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.
 • Zaburi  50:4;
  • Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu wake.
 • Zaburi 82:1;
  • Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.
 • Danieli 7:9-10;
  • 9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye Mzee wa siku ameketi; mavazi Yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa Chake kama sufu safi; kiti Chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu Zake moto uwakao.
  • 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
 • Yoeli 3:12;
  • Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.

 

MUNGU KATIKA KITI CHA ENZI, KIKUBWA, CHEUPE

Ufunuo 20:11-15

11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

 • Muhubiri 11:9
  • Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
 • 2 Timotheo  4:8 (Paulo: Mfano wa kuigwa)
  • 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;  8 Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo BWANA, Mhukumu Mwenye Haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

 

MAONYO YA YESU

Waebrania 12:25-26

 • 25 Angalieni msimkatae Yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa Yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na Yeye atuonyaye kutoka mbinguni;
 • 26 Ambaye sauti Yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.

 

SAUTI YA INJILI

Sikiliza Ahadi/ Sauti ya Mungu ikinena nawe, tunapofunga kipindi hiki:

Isaya 1:18

 • 18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
 • 19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; 20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.

MWITIKIO WETU

NZK # 171. “HUKUMU”

(The Judgment Has Set)

 

Imeanzishwa hukumu mbinguni; Tutasimamaje pale; Apimapo Mungu hakimu kula wazo na tendo?

 • Tutasimamaje sote katika siku kuu ile?
 • Dhambi zitu zitafutika ama zitatuangusha?

 

Wametangulia wafu kupimwa, Kitambo ndipo wahai, Watapokea neno la mwisho, Vitabuni mwa Mungu.

Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja, Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!


 

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu mpendwa, ninakiri nikisema mimi ni mdhambi. Katika somo la leo, tumejifunza dhahiri kwamba wewe ni Hakimu na hakika utahukumu dhambi. “Tutasimamaje usiku ule, Siri zetu, kila moja, Zafunuliwa toka vitabu; Yesu atusaidie!” Saidia kila mmoja atakaye soma Injili hii, akate shauri, na kuungama, na kutubu dhambi yake. Hakika ahadi Zako ni za kweli- kwamaba utasamehe uovu wetu. Tusamehe, tusafishe, tutakase, na ukatuhifadhi katika Pendo Lako. Siku ile Hakimu Mkuu atakapokuja, ebu tuwe miongoni mwa wateule wako. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mkombozi wetu, Amina!

 

BWANA ATUBARIKI SOTE!

The Gospel’s Voice © 2017

 

NITAPATAJE SOMO LA LEO?

 • Mobile App: The Gospel’s Voice (TGV)

Waweza sikiliza pia toleo la Sauti kupitia:

 • Facebook: Sauti Ya Injili SDA
 • Whats App: Sauti Ya Injili SDA
 • Kiungo cha TGV Mobile App
 • Kiungo cha Tovuti: tgvs.org