19-127: Zaburi 127- “Bwana Asipoijenga Nyumba”

 
Biblia: “Soma, Elewa, Shuhudia”

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

http://tgvs.org/archives/2314

(a) 19-127: Zaburi 127- “Bwana Asipoijenga Nyumba”
(b) Jamii: Zaburi
(c) Mfululizo: Biblia Sura kwa Sura
(d) Wahusika: Bwana, watu Wake
(e) Tabia ya Mungu: Uaminifu
(f) Fungu Kuu: Zaburi 127:1-2
(g) Neno Kuu: bure, Zaburi 127:1-2
(h) Msisitizo: Kumtegemea Bwana
OMBI: Baba yetu na Mungu wetu. Jina Lako litukuzwe milele. Asante Bwana kwa nafasi nyingine ya uhai. Asante kwa zawadi ya Neno Lako. Kabla ya kuanza kipindi hiki, tunaalika uwepo Wako, Bwana. Tunaomba Roho Mtakatifu, katika tafakari ya somo hili atukirimie hekima ya utambuzi wa sauti Yako na nguvu ya kuitii. Tusaidie kufanya uamuzi wa busara, kila wakati, kuachana na dhambi, tukikuchagua Wewe na kuuchagua wokovu. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tubadilishe ili tufanane Nawe. Bariki kila mmoja Bwana. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!
“BWANA ASIPOIJENGA NYUMBA”

Muhtasari Wa Mawazo Makuu

MAANA HALISI YA UBATILI (127:1 – 2)
(a) Ujenzi bure (127:1a)
(b) Kazi bure (127:1a)
(c) Ukinzi bure (127:1b)
(d) Wasiwasi bure (127:2)

MAANA HALISI YA THAMANI (127: 3 – 5)
(a) Watoto ni urithi wetu (127: 3)
(b) Watoto ni wasaidizi wetu (127:4)
(c) Watoto ni furaha yetu (127:5)

Zaburi 127

1 Bwana asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure.

2 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.

3 Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu.

4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.

5 Heri mtu yule aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu wanaposema na adui langoni.

 

FUNDISHO KUU:

Mtegemee Mungu pekee katika mipango yako yote, usimtegemee mwanadamu.

 

Mifano michache ya Biblia:

Mwanzo 43:14 (Israeli, baba yao)

Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.

Kutoka17:8–11 (Waameleki & Israeli)

8 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.

9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.

10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.

11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
Zaburi 60:11b–12

11 Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai.

12 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
Zaburi 108:10–13

10 Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?

11 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?

12 Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai.

13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

 

TUFANYE NINI BASI NA SURA HII?

Maswali ya kujihoji Katika Sura Hii:
(1) Je, kuna dhambi ya kuepukwa hapa?
(2) Je, kuna dhambi ya kutubu hapa?
(3) Je, kuna ombi la kuomba hapa?
(4) Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
(5) Je, kuna agizo au wajibu wa kufanya hapa?
(6) Je, kuna makosa au mapungufu ya kuepukwa hapa?
(7) Je, sura hii inatufundisha nini kuhusu Mungu?
(8) Je, sura hii ina umuhimu gani katika mpango wa wokovu wetu?

SAUTI YA INJILI

Sikiliza Sauti ya Mungu kwako leo tunapofunga kipindi hiki

Zaburi 127:1
Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
OMBI: Baba yetu na Mungu wetu mpendwa, tunashukuru kwa tafakari ya Neno Lako katika sura hii. Twaomba Roho Wako aendelee kutufundisha sura hii tena na tena. Tukumbushe kukutegemea wewe daima. Ebu mmoja aguswe na kubadilishwa na Neno hili zuri la Kristo Yesu. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mkombozi wetu, Amina!

BWANA ATUBARIKI SOTE!
The Gospel’s Voice © 2017

KARIBUNI TUJADILI/ TUJIBU MASWALI HAYO HAPO JUU.