19-126: Zaburi 126 -Tutashangilia wenye mavuno.

Biblia: “Soma, Elewa, Shuhudia”

 

USOMAJI WA BIBLIA  KWA MPANGO

http://tgvs.org/archives/2310

 • (a) 19-126: Zaburi 126 -Tutashangilia wenye mavuno.
 • (b) Kategoria : Zaburi
 • (c) Mfululizo: Biblia Sura kwa Sura
 • (d) WahusikaBwana, watu Wake
 • (e) Tabia ya Mungu: Uaminifu, Uwezo
 • (f) Fungu Kuu: Zaburi 126:1-3
 • (g) Neno Kuu: Kurejeshwa, Zaburi 126: 1,4
 • (h) Msisitizo: Bwana Alipowarejeza Mateka

 

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU

 1. Mandhari ya nyuma
 2. Uhalisia: Ukombozi (Zaburi 126: 1)
 3. Uhalisia: Furaha (Zaburi 126:2a)
 4. Majibu/ Hisia (Zaburi 126:2b – 3)
 5. Majibu yakushangaza ya Mataifa (Zaburi 126:2b)
 6. Majibu ya uthibitisho ya Waebrania (Zaburi 126: 3)
 7. Ombi Maalumu (Zaburi 126:4)
 8. Jibu la Ombi (Zaburi 126:5-6)
 9. Wakati wa Maombolezo (Zaburi 126:5-6a)
 10. Wakati wa Mavuno (Zaburi 126:6)
 11. Hitimisho

 

 ZABURI 126

1 Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.

2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.

3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi.

4 Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini.

5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.

6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.


 

 

TUFANYE NINI BASI NA SURA HII?

Maswali Muhimu Katika Sura Hii

 • Je, kuna dhambi ya kuepukwa hapa?
 • Je, kuna dhambi ya kutubu hapa?
 • Je, kuna ombi la kuomba au kurudiwa hapa?
 • Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
 • Je, kuna agizo au wajibu wa kufanya hapa?
 • Je, kuna makosa au mapungufu ya kuepukwa hapa?
 • Je, sura hii inanifundisha mimi nini kuhusu Mungu?
 • Je, sura hii ina umuhimu gani katika mpango wa wokovu wangu?

 

SAUTI YA INJILI

Sikiliza Sauti ya Mungu kwako leo tunapofunga kipindi hiki

 

Isaya 12:1 – 3

 • 1 Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
 • 2 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
 • 3 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.

 

MWITIKIO WETU

NZK # : 55: Twapanda Mapema

1.
Twapanda mapema, na mchana kutwa
Mbegu za fadhili hata jioni,
Twangojea sasa siku za kuvuna;
Tutashangilia wenye mavuno.

Wenye Mavuno, Wenye Mavuno,
Tutashangilia Wenye Mavuno.
Wenye Mavuno, Wenye Mavuno,
Tutashangilia Wenye Mavuno.

2.
Twapanda mwangani na kwenye kivuli;
Tusishindwe na baridi na pepo;
Punde itakwisha kazi yetu hapa:
Tutashangilia wenye mavuno.

3.
Twapanda kwa Bwana mbegu kila siku.
Tujapoona taabu na huzuni;
Tuishapo shinda atatupokea:
Tutashangilia wenye mavuno.


 

 

NITAPATAJE SOMO LA LEO?

 • Mobile App: The Gospel’s Voice
 • Facebook: Sauti Ya Injili SDA
 • Whats App: Sauti Ya Injili SDA

WAWEZA PIA KUSIKILIZA KUPITIA:

 • Kiungo cha TGV Mobile App
 • Kiungo cha Tovuti: Sauti Ya Injili SDA

BWANA ATUBARIKI SOTE!

 

The Gospel’s Voice © 2017