19-118: Zaburi 118

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

 

MUHTASARI WA ZABURI 118       

 • Neno Kuu: Mshukuruni Bwana
 • Tabia ya Mungu: Ukuu, Uwezo, Uaminifu
 • Mistari Ya Msisitizo: Zaburi 118:1, 22, 29
 • Wahusika: Mungu, Watu Wake

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu. Jina Lako litukuzwe milele. Asante Bwana kwa nafasi nyingine ya uhai. Asante kwa zawadi ya Neno Lako. Kabala ya kuanza kipindi hiki, tunaalika uwepo Wako, Bwana. Tunaomba Roho Mtakatifu, katika tafakari ya somo hili, atukirimie hekima ya utambuzi wa sauti Yako na nguvu ya kuitii. Tusaidie kufanya uamuzi wa busara, kila wakati, kuachana na dhambi, tukikuchagua Wewe na kuuchagua wokovu. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tubadilishe ili tufanane Nawe. Bariki kila mmoja Bwana. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!


 

ZABURI 118

MSHUKURUNI BWANA KWA KUWA NI MWEMA

 • 1 Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
 • 2 Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
 • 3 Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
 • 4 Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

 

MKABIDHI BWANA SHIDA ZAKO ZOTE

 • 5 Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.
 • 6 Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
 • 7 Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
 • 8 Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.
 • 9 Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.
 • 10 Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
 • 11 Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
 • 12 Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
 • 13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia.
 • 14 Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.

 

MKONO WA KUUME WA BWANA

 • 15 Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
 • 16 Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
 • 17 Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.
 • 18 Bwana ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife.
 • 19 Nifungulieni malango ya haki, Nitaingia na kumshukuru Bwana.
 • 20 Lango hili ni la Bwana, Wenye haki ndio watakaoliingia.
 • 21 Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.

 

JIWE KUU LA PEMBENI.

 • 22 Jiwe walilolikataa waashi limekuwa Jiwe Kuu la pembeni.
 • 23 Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu.
 • 24 Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.
 • 25 Ee Bwana, utuokoe, twakusihi; Ee Bwana, utufanikishe, twakusihi.
 • 26 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana; Tumewabarikia toka nyumbani mwa Bwana.
 • 27 Bwana ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu.
 • 28 Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
 • 29 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

 

TUFANYE NINI BASI NA ZABURI HII?

29 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili Zake ni za milele.


 

 

UFUPISHO WA ZABURI 118

Kwa tukio la Pasaka, nyumba zote katika Yerusalemu zifunguliwa kwa ajili ya wahaji. mahema pia yalipigwa katika kila nafasi iliyopatikana katika mji na vilima vilivyo zunguka mji.  Pasaka ilisherehekewa na sherehe yake takatifu kwa kuadhimisha ukombozi kutoka utumwa wa Misri, na kuelekeza mbele zaidi kwa Dhabihu ambayo  ingekomboa watu  kutoka utumwa wa dhambi. Kama Israeli walivyosherehekea ukombozi wa baba zao kwa Mungu na uhifadhi Wake wa kimuujiza wakati wa safari yao kutoka Misri, vivyo hivyo nasi lazima kumshukuru na  kukukumbuka njia mbalimbli ambazo Mungu imetutoa kutoka gizani kwenda kwenye nuru ya thamani ya neema na ukweli Wake.

Sikukuu ya Vibanda haikusherehekea mavuno tu lakini pia ilikumbusha watu kuhusu uwepo wa Mungu katika jangwa na mbele zaidi katika siku kuu ya kusanyanyiko la mwisho. Bwana atawatuma wavunaji Wake kukusanya magugu kwa ajili ya moto na ngano itakusanywa katika ghala Lake. Katika wakati huo waovu na dhambi zitaangamizwa. Na kila sauti katika ulimwengu mzima utaungana katika sifa na furaha za shangwe kwa Mungu.

Jan Harry Cabungcal

 • Neuroscientist
 • Europe for Jesus
 • Switzerland

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu mpendwa, tunashukuru kwa tafakari ya Neno Lako katika sura hii. Twaomba Roho Wako aendelee kutufundisha sura hii tena na tena. Tukumbushe kuyasoma maandiko, na kuendelea kuyasikia “maneno ya Unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu”.Tusaidie kuwa “watendaji wa Neno, wala si wasikiaji tu, hali tukijidanganya nafsi zetu”. Ebu mmoja aguswe na kubadilishwa na Neno hili zuri la Kristo Yesu. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mkombozi wetu, Amina!