2/25/17: Gharama Chungu

2/25/2017: Gharama Chungu

Mwl. Peter Daniel Marwa


Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi. Waebrania 12:17.

Mara baada ya Yakobo kuondoka hemani mwa babaye, Esau aliingia. Japo Esau alikuwa ameuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza na kuthibitisha hilo kwa kiapo , sasa alikuwa ameazimia kujitwalia baraka zake,licha ya madai ya ndugu yake . Baraka hizi za kiroho zilikuwa zimeunganika na haki ya uzaliwa wa kwanza isiyo ya kudumu ambayo ingempa kuwa kichwa chs familia na kupata mara mbili ya sehemu zinazogawanywa kutoka kwa mali ya baba yake. Hizi zilikuwa ndizo baraka alizozithamini..

Esau alipuuzia thamani ya baraka wakati ilipokuwa imemkaribia , lakini sasa akatamani kuwa nayo ilipokuwa imemwacha milele. Nguvu zake.zote.za asili yenye msukumo na hisia kali zikaamshwa na huzuni na hasira yake vikawa vikali kiasi cha kutisha . Alilia 😥 kilio cha uchungu sana , “NIBARIKI NA MIMI , MIMI NAMI , EE BABANGU”…

Haki ya uzaliwa wa kwanza ambayo aliiuza kwa uzembe hivyo, sasa hakuweza kuimiliki tena . Kwa ajili ya “MEGO” moja tu , kwa sababu ya kuridhisha uchu wa chakula ambao kamwe haukuwahi kudhibitiwa, Esau alipoteza urithi wake , lakini alipoona upumbavu wake , alikuwa amechelewa sana kurejesha baraka yake..

Esau hakuwa amefungiwa nje ya fursa ya kutafuta fadhili ya Mungu kwa kutubu, lakini hakupata njia ya kurejesha haki ya uzaliwa wa kwanza . Huzuni yake haikutokana na kuiona hatia ya dhambi ; hakutamani kupatanishwa upya na Mungu . Alihuzunika kwa sababu ya matokeo ya dhambi yake, lakini haikuwa kwa sababu ya dhambi yenyewe..

Toba huwa inahusisha sikitiko kwa sababu ya dhambi na kuiacha . Hatutaiacha dhambi kama hatuwezi kuona uovu wake ; hadi tutakapoiacha moyoni. hakutakuwa na badiliko la kweli maishani..

Wapo wengi wanoshindwa kuelewa asili ya kweli ya toba . Wengi huwa wanasikitika kwamba wametenda dhambi na hata hufanya matengezo ya nje , kwa sababu wanaogopa kuwa makosa yao yatawaletea taabu . Lakini hii siyo toba kulingna na maana ya Biblia. Hawa huombolezea mateso , badala ya dhambi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa huzuni ya Esau alipoona kwamba alikuwa amepoteza milele haki ya uzaliwa wa kwanza.