40-010: “Matunda Yapasayo Toba”

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

INJILI YA ASUBUHI: MATAYO MTAKATIFU


 

MATUNDA YAPASAYO TOBA

Mawazo Makuu katika Injili ya Leo:

UTANGULIZI

 • “Yohana Mbatizaji”
 • Ujumbe wa Onyo: “Tubuni”
 • Yerusalemu, na Uyahudi wote
 • Akawabatiza katika mto wa Yordani

MAFARISAYO NA MASADUKAYO

 • Mafarisayo na Masadukayo
 • Enyi wazao wa Nyoka
 • Tunaye baba, ndiye Ibrahimu

HUKUMU IJAYO

 • “Shoka limekwisha kuwekwa”
 • “Hukatwa na kutupwa motoni”
 • “Pepeto Lake li mkononi Mwake”

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

 • Ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kwa Moto.
 • Basi Zaeni Matunda Yapasayo Toba (Mt. 3:8)

 

MATAYO 3:5-12

5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;

6 Naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.

7 Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?

8 Basi zaeni matunda yapasayo toba;

9 Wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.

10 Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali Yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu Vyake; Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

12 Ambaye pepeto Lake li mkononi mwake, Naye atausafisha sana uwanda Wake; na kuikusanya ngano Yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.


 

NITASIKILIZAJE INJILI YA LEO?

 1. Bofya link hiyo katika Tovuti
 2. Bofya link hiyo katika Mobile App
 3. Mobile App: The Gospel’s Voice
 4. Pakua Audio hii hapa.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE!

The Gospel’s Voice © 2017