125-014: “Njoni, tumwimbie Bwana”.

SAA YA IBADA NA MAOMBI.

 • (a) http://tgvs.org/archives/2240
 • (b) 125-014: “Njoni, tumwimbie Bwana”.
 • (c) Jamii: Saa Ya Ibada
 • (d) Msisitizo: Sifa na Shukrani
 • (e) Fungu Kuu: Zaburi 95:1

 

“MWITO WA IBADA” (sehemu ya 1)

 • Zaburi 95:1
 • Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.

 

MAFUNGU MENGINE:

 • Zaburi 34:3;
  • Mtukuzeni Bwana pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
 • Zaburi 66:8;
  • Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu, Itangazeni sauti ya sifa zake;
 • Zaburi 107:8,
  • Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
 • Zaburi 107:15,
  • Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
 • Zaburi 107:21;
  • Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu
 • Zaburi 117:1-2
  • 1 Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidini.
  • 2 Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa Bwana ni wa milele.
 • Zaburi 118:1;
  • Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele

 

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

 • Zaburi 136:1-3;
 • 1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
 • 2 Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
 • 3 Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

 

 • Zaburi 148:11-13;
 • 13 Na walisifu jina la Bwana, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
 • 14 Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.

 

HITIMISHO

 • Zaburi 150:6
 • Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

 

OMBI LA MWISHO

Ee Bwana! Jina Lako lihimidiwe. Tukumbushe kukusifu na kukuabudu siku hii ya leo. Tusamehe makosa yetu.Tumeomba haya katika Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, Amina.

 


 

BWANA ATUBARIKI SOTE!

 

Sauti Ya Injili SDA © 2017