Jumanne: January 10, 2017

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

KIPINDI CHA MAOMBI NA IBADA YA ASUBUHI

 

MAANDALIZI KWA AJILI YA SIKU 10 ZA MAOMBI & KUFUNGA.

 • Wapendwa, kama ilivyotangazwa awali, kesho tutajiunga na waumuni wengine ulimwenguni katika mchakato wa maombi ya kina na kufunga. Programu hizi zitaendelea hadi Jumamosi ya tarehe 21-1-2017.

 

KATIKA KIPINDI HIKI TUNAOMBWA:

 1. Tujihoji nafsi zetu, tumlilie Mungu, tuutafute uso Wake;
 2. Tusameheane, ili Baba yetu wa Mbinguni atusamehe pia;
 3. Tuwe na Huzuni ya dhambi; Tuungame, Tutubu;
 4. Tuachane na mizaha, kejeli, matani, n.k.
 5. Tupost masomo ya Biblia, Nyimbo, n.k
 6. Tuepeke chochote kile kitakacholeta kikwazo kwa wenzetu.

  

SAUTI YA INJILI:

(Ebu sikiliza ahadi/ sauti ya Mungu ikinena nawe asubuhi ya leo)

Kutoka 19:5-6

 • 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,  6 Nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.

 

 CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.

 • UINJILIST: Radio Morning Star & Staff wote
 • DEVON: Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu
 • WANAKIKUNDI: Ujazo wa Roho Mtakatifu, Upendo, Umoja, Msamaha, Utakaso, na Uaminifu wa Members wote wa kikundi hiki, ili wawe waaminifu katika Kuomba na Kuombea wengine pia.
 • MSHITU: Anaendesha mahibiri kwa njia ya Radio, na tayari watu wanne (4) wamejitokeza kubatizwa; tuzidi kuombea huduma yake.
 • ANNA: (a) “hali ya hewa-Mungu atunyeshee mvua ili mazao yetu yastawi na hatimae tupate chakula”, (b) “familia zetu ziwe nuru ya kuwavuta wengine kwa Kristo”
 • OGETO: Job Interview jana, tumuombee ili mambo yaende sambamba, kama ni mapenzi ya Mungu, achaguliwe katika candidates wengi waliopelekamaombi ya kazi.
 • UTII WA NENO– “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

 UNGANA NASI KWA AJILI YA MAOMBI

 1. Kila Siku Alfajiri: Hapa katika kikundi
 2. Siku 10 za Maombi: January 11–21; 2017
 3. Ombea jirani yako: changamoto mbalimbali zinazowasibu
 4. Ombea nafsi yako: utubu, uokolewe, uingie mbinguni
 5. Ombea viongozi wa serikali: Hekima, Amani, n.k.
 6. Ombea viongozi wetu wa kanisa: Bwana awatangulie
 7. Ombea huduma hii ya Sauti Ya Injili SDA
 8. Ombea mchakato wa Injili Ulimwenguni kote (Matayo 28:19-20)
 9. Ombea mtu mmoja atakayesikia kweli hizi za Biblia akapate kuokolewa.
 10. Jiandae: “Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli”; (Amosi 4:12).

 

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 • Kuweka Maombi (Maandishi/ Sauti)
 • Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya Mungu wetu.
 • Kuandika Mahitaji/ Maombi/ Changamoto mbalimbali zinazokusibu

ANGALIZO:

 • Kama nimesahau ombi la mtu fulani, naomba uniinbox, ili tuliweke.
 • Mahitaji yatakayo orodheshwa leo, yatakusanywa na kuombewa kesho Asubuhi.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE.

 • Matayo 26:41 :“Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.
 • Sauti Ya Injili SDA ©  2017.  Haki zote zimehifadhiwa.