January 9, 2017

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

KIPINDI CHA MAOMBI NA IBADA YA ASUBUHI

 

SAUTI YA INJILI:

 • (Ebu sikiliza Ahadi/ Sauti ya Mungu ikinena nawe Asubuhi ya Leo)

2 Corinthians 6:17–18

 • 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
 • 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.

 

CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.

 • UINJILIST: Radio Morning Star & Staff wote
 • DEVON: Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu
 • WANAKIKUNDI: Ujazo wa Roho Mtakatifu, Upendo, Umoja, Msamaha, Utakaso, na Uaminifu wa Members wote wa kikundi hiki, ili wawe waaminifu katika Kuomba na Kuombea wengine pia.
 • MSHITU: Anaendesha mahibiri kwa njia ya Radio, na tayari watu wanne (4) wamejitokeza kubatizwa; tuzidi kuombea huduma yake.
 • OGETO: Ana Job Interview leo hii, tumuombee ili mambo yaende sambamba, kama ni mapenzi ya Mungu, achaguliwe katika candidates wengi waliopelekamaombi ya kazi.
 • UTII WA NENO– “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

 

UNGANA NASI KWA AJILI YA MAOMBI

 • Kila Siku Alfajiri: Hapa katika kikundi
 • Siku 10 za Maombi: January 11–21; 2017
 • Ombea jirani yako: changamoto mbalimbali zinazowasibu
 • Ombea nafsi yako: utubu, uokolewe, uingie mbinguni
 • Ombea viongozi wa serikali: Hekima, Amani, n.k.
 • Ombea viongozi wetu wa kanisa: Bwana awatangulie
 • Ombea huduma hii ya Sauti Ya Injili SDA
 • Ombea mchakato wa Injili Ulimwenguni kote (Matayo 28:19-20)
 • Ombea mtu mmoja atakayesikia kweli hizi za Biblia akapate kuokolewa.
 • Jiandae kukutana na Mungu Wako. “Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli”; (Amosi 4:12).

 

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 • Kuweka Maombi (Maandishi/ Sauti)
 • Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya Mungu wetu.
 • Kuandika Mahitaji/ Maombi/ Changamoto mbalimbali zinazokusibu

ANGALIZO:

 • Kama nimesahau ombi la mtu fulani, naomba uniinbox, ili tuliweke.
 • Mahitaji yatakayo orodheshwa leo, yatakusanywa na kuombewa kesho Asubuhi.

BWANA ATUBARIKI SOTE.

 


Matayo 26:41

“Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.

 

 

 

Sauti Ya Injili SDA ©  2017.  Haki zote zimehifadhiwa.