Jumapili: January 8, 2017

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

KIPINDI CHA MAOMBI NA IBADA YA ASUBUHI

SAUTI YA INJILI: (Ebu sikiliza Ahadi/ Sauti ya Mungu ikinena nawe Asubuhi ya Leo)

2 Timothy 2:11: “Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja Naye, tutaishi pamoja Naye pia”


 

CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.

 1. UINJILISTI: Radio Morning Star & Staff wote
 2. DEVON: Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu
 3. WANAKIKUNDI: Ujazo wa Roho Mtakatifu, Upendo, Umoja, Msamaha, Utakaso, na Uaminifu wa Members wote wa kikundi hiki, ili wawe waaminifu katika Kuomba na Kuombea wengine pia.
 4. UTII WA NENO“Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

 

UNGANA NASI KWA AJILI YA MAOMBI

 1. Kila Siku Alfajiri: Hapa katika kikundi
 2. Siku 10 za Maombi: January 11–21; 2017
 3. Ombea jirani yako: changamoto mbalimbali zinazowasibu
 4. Ombea nafsi yako: utubu, uokolewe, uingie mbinguni
 5. Ombea viongozi wa serikali: Hekima, Amani, n.k.
 6. Ombea viongozi wetu wa kanisa: Bwana awatangulie
 7. Ombea huduma hii ya Sauti Ya Injili SDA
 8. Ombea mchakato wa Injili Ulimwenguni kote (Matayo 28:19-20)
 9. Ombea mtu mmoja atakayesikia kweli hizi za Biblia akapate kuokolewa.
 10. Jiandae kukutana na Mungu Wako.Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli”; (Amosi 4:12).

 

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 1. Kuweka Maombi (Maandishi/ Sauti)
 2. Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya Mungu wetu.
 3. Kuandika Mahitaji/ Maombi/ Changamoto mbalimbali zinazokusibu

ANGALIZO:

 • Mahitaji yatakayo orodheshwa leo, yatakusanywa na kuombewa kesho Asubuhi.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE.

 • Matayo 26:41  “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.

© Sauti Ya Injili SDA -2017