Nyimbo Za Kikristo: 41-50

(NZK #41): Roho Mtakatifu

1. Roho Mtakatifu, Kiongozi Amini;
Utushike Mkono Tulio Wasafiri;

 • Utupe Kusikia Sauti Ya Upole;
  “Msafiri Fuata, Naongoza Nyumbani.”

2. Wewe Ndiwe Rafiki, Msaada Karibu;
Tusiache Shakani; Na Tukiwa Gizani

3. Siku Zetu Za Kazi, Zikiwa Zimekwisha,
Wala Hatuna Tamaa Ila Mbingu Na Sala;


 

(NZK #42): Ewe Roho Wa Mbinguni

1. Ewe Roho Wa Mbinguni, Maombi Sikia!
Makao Yako Yafanye Mioyoni Mwetu.

2. Kama Nuru, Tupenyeze, Giza Uondoe;
Siri Yako Tuone, Na Amani Yako.

3. Kama Moto, Tusafishe, Choma Dhambi Yetu;
Roho Zetu Ziwe Zote Hekalu La Bwana.

4. Kama Umande, Na Uje, Utuburudishe,
Moyo ‘Kavu Utakuwa Ni Wenye Baraka.

5. Kaka Upepo Ee Roho, Katika Pentekoste
Ukombozi Utangaze, Kwa Kila Taife.


(NZK #43):Furaha Gani!

1. Furaha Gani Na Ushiriki,
Nikimtegemea Yesu Tu!
Baraka Gani, Tena Amani,
Nikimtegemea Yesu Tu!

 • Tegemea, Salama Bila Hatari;
  Tegemea, Tegemea Mwokozi Yesu.

2. Nitaiweza Njia Nyembamba,
Nikimtegemea Yesu Tu;
Njia ‘Tazidi Kuwa Rahisi,
Nkimtegemea Yesu Tu!

3. Sina Sababu Ya Kuogopa,
Nikimtegemea Yesu Tu;
Atakuwa Karibu Daima,
Nikimtegemea Yesu Tu.


 

(NZK #44):Urafiki Wa Yesu

1. Hakuna Rafiki Kama Yesu, Hakuna, Hakuna!
Tabibu Mwingine Wa Rohoni, Hakuna Hakuna!

 • Yesu Ajua Shida Zetu; Daima Ataongoza.
  Hakuna Rafiki Kama Yesu, Hakuna, Hakuna!

2. Wakati Ambapo Hapo Yeye, Hapana, Hapana!
Wala Giza Kukutenga Naye, Hakuna, Hakuna!

3. Aliyesahauliwa Naye, Hakuna, Hakuna!
Mkosaji Asiyempenda, Hakuna, Hakuna!

4. Kipawa Kama Mwokozi Wetu, Hakuna, Hakuna!
Ambaye Atanyimwa Wokovu Hakuna, Hakuna!


 

(NZK #45):Mwanga Umo Mwoyoni.

1. Mlimani Pana Mwanga, Mwanga Wa Jua Zuri
Shambani Na Baharini Jua Tukufu Liko;
Mwanga Ulio Mkubwa Umo Moyoni Mwangu,
Kwa Kuwa Yesu Alipo Hapa Pana Mwangaza.

 • Mwangaza Ulio Mzuri, Mwanga Umo Moyoni;
  Akiwapo Bwana Yesu Pana Mwanga Moyoni.

2. Kama Mavazi Kukuu Ninavua Huzuni:
Nguo Nzuri Za Furaha Umenipa Za Kuvaa.
Nakuandama Rohoni Hata Nyuba Ya Juu
Iliyopambwa Vizuri Katika Pendo Lako.

3. Ulinikomboa Yesu; Maisha Yangu, Mali,
Vyote Ni Nyako, Mwokozi—Daima Nikusifu.
Nakuandama Rohoni Hata Nyumba Ya Juu
Iliyopambwa Vizuri Katika Pendo Lako.


 

(NZK #46): Miguuni Pake Yesu

1. Miguuni Pake Yesu, Maneno Yake Tamu;
Pahali Palipo Heri, Niwepo Kila Siku,
Miguuni Pake Yesu Nakumbuka Upendo
Na Hisani Vyake Kwangu, Vimenivuta Moyo.

2. Miguuni Pake Yesu, Hapa Pahali Bora
Pakuweka Dhambi Zangu: Pahali Pa Pumziko.
Miguuni Pake Yesu, Hapa Nafanya Sala,
Kwake Napewa Uwezo, Faraja Na Neema.

3. Unibariki Mwokozi, Ni Miguuni Pako,
Unitazame Kwa Pendo, Nione Uso Wako.
Nipe Bwana Nia Yake Ili Ionekane
Nimekaa Na Mwokozi Aliye Haki Yangu.


 

(NZK #47): Ni Heri Kifungo

1. Ni Heri Kifungo Kinachotufunga
Mioyo Yetu Kwa Pendo La Kikristo.

2. M-Bele Ya Baba Tunatoa Sala,
Hofu, Nia Masumbufu Yetu Ni Mamoja.

3. Tunavishiriki Matata Na Shida,
Na Mara Nyingi Twatoa Chozi La Fanaka.

4. Tunapoachana Moyoni Twalia;
Lakini Tutakutana M-Wisho Mbinguni.


 

(NZK #48):Ninakupenda Zaidi

1. Ninakupenda Zaidi, Ya Vyote Vingine;
Kwani Umenipa Raha, Na Amani, Bwana.

 • Nusu Haijatangazwa (Tangazwa)
  Ya Upendo Wako;
  Nusu Haijatangazwa (Tangazwa)
  Damu Hutakasa (Takasa).

2. Nakujua U Karibu Kuliko Dunia;
Kukukumbuka Ni Tamu Kupita Kuimba.

3. Kweli Wanifurahisha, Na Nitafurahi;
Pasipo Upendo Wako Naona Huzuni.

4. Itakuwaje Mwokozi, Kukaa Na Wewe,
Ikiwa Ulimwenguni Tuna Furaha Hii?


 

(NZK #49): Ninaye Rafiki

1. Ninaye Rafiki Naye Alinipenda Mbele;
Kwa Kamba Za Pendo Lake Nemefungwa Milele:
Aukaza Moyo Wangu, Uache Ugeuzi,
Ninakaa Ndani Yake, Yeye Kwangu Milele.

2. Ninaye Rafiki Ndiye Aliyenifilia;
Alimwaga Damu Yake Kwa Watu Wote Pia;
Sina Kitu Mimi Tena, Nikiwa Navyo Tele;
Pia Vyote Ni Amana Ndimi Wake Milele.

3. Ninaye Rafiki Naye Uwezo Amepewa;
Atanilinda Mwenyewe, Juu ‘Tachukuliwa;
Nikitazama Mbinguni Hupata Nguvu Tele;
Sasa Natumika Chini, Kisha Juu Milele.

4. Ninaye Rafiki Naye Yuna Na Moyo Mwema,
Ni Mwalimu Kiongozi, Mlinzi Wa Daima;
Ni Nani Wa Kunitenga, Na Mpenzi Wa Mbele?
Kwake Nimetia Nanga, Ndimi Wake Milele.


 

(NZK #50):Mungu Nawe Nanyi Daima

1. Mungu Nawe Nanyi Daima; Hata Twonane Ya Pili,
Awachunge Kwa Fadhili, Mungu Nawe Nanyi Daima.

 • Hata Twonane Juu, Hata Twonane Tena Kwake;
  Hata Twonane Juu, Mungu Nawe Nanyi Daima.

2. Mungu Nawe Nanyi Daima. Mungu Nawe Nanyi Daima,
Awafunike Mabawa. Awalishe, Awakuze;

3. Mungu Nawe Nanyi Daima. Mungu Nawe Nanyi Daima,
Kila Wakati Wa Shida Awalinde Hifadhini:

4. Mungu Nawe Nanyi Daima. Mungu Nawe Nanyi Daima,
Awabariki Na Pendo Ambalo Halina Mwisho; Mungu Nawe Nanyi Daima.