Nyimbo za Kristo: 31-40

(NZK # 30) YESU, UNIPENDAYE

1. Yesu Unipendaye Kwako Nakimbilia,
Ni Wewe Utoshaye Mwovu Akinijia.
Yafiche Ubavuni Mwako Maisha Yangu;
Nifishe Bandarini, Wokoe Moyo Wangu.

2. Ngome Nyingine Sina; Nategemea Kwako,
Usinitupe Bwana, Nipe Neema Yako,
Ninakuamania, Mwenye Kuniwezesha;
Shari Wanikingia, Vitani Wanitosha.

3. Nakutaka Mpaji, Vyote Napata Kwako;
Niwapo Muhitaji, Utanijazi Vyako;
Nao Waangukao Wanyonge Wape Nguvu;
Poza Wauguao, Uongoze Vipofu.

4. Mwana Umeniosha Moyo Kwa Damu Yako;
Neema Ya Kutosha Yapatikana Kwako;
Kwako Bwana Naona Kisima Cha Uzima;
Mwangu Moyoni, Bwana, Bubujika Daima.


 

(NZK # 31) NIIMBE PENDO LAKO

1. Niimbe (Niimbe) Pendo Lake,
Pendo La (Pendo La) Yesu Bwana;
Sababu (Sababu) Alitika
Kwa Baba Akafa.

 • Niimbe (Niimbe) Pendo Lake;
  Sifa Kuu (Sifa Kuu) Nitatoa;
  Akafa (Akafa) Niwe Hai, —
  Niimbe Pendo Lake.

2. Machozi (Machozi) Alitoa
Ijapo (Ijapo) Sijalia;
Maombi (Maombi) Yangu Bado,
Aniombeapo.

3. Upendo (Upendo) Kubwa Huo!
Dunia (Dunia) Haijui
Samaha (Samaha) Kwa Makosa
Kubwa Kama Yangu.

4. Hapana (Hapana) Tendo Jema
Ambalo (Ambalo) Nilitenda,
Nataka (Nataka) Toka Leo
Nimwonyeshe Pendo.


(NZK # 32): TANGU KUAMINI

1. Ninao Wimbo Mzuri, Tangu Kuamini;
Wa Mkombozo Mfalme, Tangu Kuamini.

 • Tangu Kuamini, (Tangu Kuamini), Jina Lake ‘Tasifu,
  Tangu Kuamini, (Tangu Kuamini), Nitalisifu Jina Lake.

2. Kristo Anatosha Kweli, Tangu Kuamini,
Mapenzi Yake Napenda, Tangu Kuamini.

3. Ninalo Shuhuda Sawa, Tangu Kuamini,
Linalofukuza Shaka, Tangu Kuamini.

4. Ninalo Kao Tayari, Tangu Kuamini,
Nililorithi Kwa Yesu, Tangu Kuamini.


 

(NZK # 33): KARIBU SANA

1. Karibu Sana Univute, Karibu Sana Daima Nawe.
Bwana Napenda Unishike, Unilinde Nisianguke Nawe.
Unilinde Nisitengwe Nawe.

2. Karibu Sana, Sina Kitu Sina, Sadaka Kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa Moyo Wangu: Uutakase Katika Damu,
Uutakase Katika Damu.

3. Karibu Sana, Wewe Nami. Ninafirahi Kuacha Dhambi-
Anasa Zote Na Kiburi: Nipe Yesu Niliyemsulibi,
Nipe Yesu Niliyemsulibi.

4. Karibu Sana, Hata Mwisho. Hata Mbinguni Nisimamapo:
Daima Dawamu Niwepo Nitakapoona Usi Wako,
Nitakapoona Uso Wako.


(NZK # 34): HADITHI KISA CHA YESU

1. Nipe Habari Za Yesu, Kwangu Ni Tamu Sana:
Kisa Chake Cha Thamani Hunipendeza Sana.
Jinsi Malaika Wengi Walivyo Imba Sifa,
Alopoleta Amani Kwa Watu Wa Dunia.

 • Nipe Habari Za Yesu, Kaza Moyoni Mwangu;
  Kisa Chake Cha Thamani Hunipendeza Sana.

2. Kisa Cha Alivyogungwa Peke Yake Jangwani.
Jinsi Alivyomshinda Jaribu La Shetani;
Kazi Aliyoifanya, Na Siku Za Huzuni,
Jinsi Walivyomtesa: Yote Ni Ya Ajabu!

3. Habari Za Msalaba Alivyosulubiwa;
Jinsi Walivyo Mzika, Akashida Kaburi.
Kisa Chake Cha Rehema. Upendo Wake Kwangu.
Alivyotoa Maisha Nipokee Wokovu.


(NZK # 35): NIMEKOMBOLEWA NA YESU

1. Nimekombolewa Na Yesu Na Sasa Nimefurahi;
Kwa Bei Ya Mauti Yake Mimi Ni Mtoto Wake.

 • Kombolewa! Nakombolewa Na Damu.
  Kombolewa! Mimi Mwana Wake Kweli.

2. Kukombolewa Nafurahi, Kupita Lugha Kutamka;
Kulionyesha Pendo Lake, Mimi Ni Mtoto Wake.

3. Nitamwona Mfalme Wangu Katika Uzuri Wake,
Ambaye Najifurahisha Katika Torati Yake.

4. Najua Taji Imewekwa Mbinguni Tayari Kwangu,
Muda Kitambo Atakuja Ili Alipo Niwepo.


 

(NZK # 36): SIKU KUU

1. Ni Siku Kuu Siku Ile Ya Kumkiri Mwokozi!
Moyo Umejaa Tele Kunyamaza Hauwezi.

 • Siku Kuu! Siku Kuu! Ya Kwushwa Dhambi Zangu Kuu!
  Hukesha Na Kuomba Tu, Ananiongoza Miguu.
  Siku Kuu! Siku Kuu! Ya Kwoshwa Dhambi Zangu Kuu!

2. Tumekwisha Kupatana, Mimi Bwake, Yeye Mbwangu,
Na Sasa Nitamwandama, Nikiri Neno La Mungu.

3. Moyo Tulia Kwa Bwana, Kiimi Cha Raha Yako;
Huna Njia Mbili Tena: Uwe Naye, Yote Ndako.


(NZK # 37): PENDO LAKO, EE MWIKOZI

1. Pendo Lako, Ee Mwokozi, Hushinda Pendo Zote!
Kaa Nasi, Ndani Yetu, Furaha Ya Mbinguni.
Yesu U Rehema Tupu, Safi Na Kusamehe,
Mfariji Mwenye Huzuni Ziondoe Machozi.

2. Roho Yako Ya Upendo, Tuma Kwa Kundi Lako;
Hebu Tuirithi Raha, Iliyoahidiwa,
Uondoe Moyo Mbaya, U Mwanzo Tena Mwisho;
Timiza Imani Yetu, Ili Tuwekwe ‘Huru.

3. Yesu, Uje Kwetu Sasa, Tupokee Huruma;
Rudi Kwetu, Tena Kamwe Usituache Pekee,
Tungekutukuza Leo, Pamoja Na Malaika,
Imba Na Kutoa Sifa, Ingia Kwa Ibada.

4. Sasa, Bwana, Kazi Yako, Imalize Moyoni;
Takasa Hekalu Lako, Wokovu Kamilisha!
Safisha Viumbe Nyako Katika Wakati Huu;
Tupumzike ‘Toka Dhambi, Tuingie Mbinguni.


(NZK # 38):: NASIFU SHANI YA MUNGU

1. Nasifu Dhani Ya Mungu, Mweneza Bahari,
Muumba Pia Wa Mbingu, Jua, Nyota, Mwezi.
Ni Tukufu Yako Shani, Mtengeza Mambo
Ya Nyakati Na Zamani, Yasiyo Na Mwisho.

2. Kadiri Ya Nionayo, Yakusifu Mungu;
Nchi Niikanyagayo, Na Hayo Mawingu;
Hakuna Hata Unyasi, Usiokukuza;
Na Upepo Wavumisha, Au Kutuliza.

3. Nami Kwa Mkono Wako, Naongozwa Sawa,
Ni Pato Nikusipo, Kukwomba Ni Dawa;
Umenizingira Nyuma, Na Mbele Baraka,
Maarifa Ya Ajabu! Yanishinda Mimi!


(NZK # 39): ATI, KUNA MVUA NJEMA

1. Ati, Kuna Mvua Njema Yanya Yenye Neema;
Watu Wanaona Vyema Bwana, Huninyeshei?

 • Na Mimi? Na Mimi? Bwana, Huninyeshei?

2. Sinipite, Baba Mwema; Dhambini Nimezama;
Rehema Niza Daima; Bwana Hunionyeshi?

3. Sinipite, Yesu Mwema; Niwe Nawe Daima,
Natamani Kukwandama: Bwana, Hunichukui?

4. Sinipite, Roho Mwema, Mpaji Wa Uzima,
Nawe Shahidi Wa Wema, Bwana Wema Hunipi?


(NZK # 40): NIJAZE SASA

1. Njoo, Roho Mtukufu Uoshe Moyo Wangu,
Utakase Nia Yangu, Njoo, Nijaze Sasa.

 • Roho Mtukufu, Njoo, Nijaze Sasa;
  Utakase Nia Yangu, Njoo, Nijaze Sasa.

2. Unijaze Moyo Wangu Ijapo Sikuoni,
Nami Ninakuhitaji, Njoo, Nijaze Sasa.

3. Nimejaa Udhaifu, Nainamia Kwako;
Roho Mtukufu Sasa, Nitilie Na Nguvu.

4. Unioshe Nifariji Niponye, Nibariki,
Unijaze Moyo Wangu; Ndiwe Mwenye Uwezo.