Nyimbo za Kristo: 21-30

(NZK # 21) BABA TWAKUJIA

1. Bwana Twakujia, Uwe Msaada;
Uwe Kimbilio, Twakusihi.
Dunia Ni Giza, Tukitengwa Nawe;
Tufariji Hapa, Baba Yetu.

 • Baba Twakujia, Tu Dhaifu,
  Usitugeue, Tusikie.

2. Salama Tulinde, Kati Ya Taabu;
Uwe Raha Yetu, Mashakani.
Roho Yasumbuka, Baba Tujalie;
Twakuomba Sana, Tupe Nguvu.

3. Neema Utupe, Tukubali Kwako;
Moyo Wetulinda, Safarini;
Tuongoe Mbele, Tupate Kushinda,
Na Kufika Ng’ambo, Kule Kwako.


(NZK # 22) USINIPITE MWOKOZI

1. Usinipite, Mwokozi, Unisikie;
Unapozuru Wengine, Usinipite.

 • Bwana, Bwana,(naomba) Unisikie;
  Unapozuru Wengini, Usinipite.

2. Kiti Chako Cha Rehema, Nakitazama;
Magoti Napiga Pale, Nisamehewe.

3. Sina Ya Kutegemea, Ila Wewe Tu;
Uso Wako Uwe Kwangu: Nakuabudu.

4. Wewe Tu U Mfariji: Sina Mbinguni,
Wala Duniani Pote, Bwana Mwingine.


(NZK # 23) YESU FURAHA YA MOYO

1. Yesu, Furaha Ya Moyo! Hazina Ya Pendo, Na Nuru.
Yote Yatupendezayo, Yasilinganishe Nawe.

2. Kweli Yako Ya Daima, Wawajibu Wakwitao,
Ni Siku Zote U Mwema Kwao Wakutafutao,.

3. U Mkate Wa Uzima, Kupokea Ni Baraka,
Twanya Kwako U Kisima Roho Zikiburudika.

4. Mwokozi Twakutamani, Kwako Roho Hutulia;
Twakushika Kwa Imani, Nawe Watubarikia.

5. Yesu, Ndiwe Kwetu Mwanga, Tufurahishe Daima;
Giza Ya Dhambi Fukuza, Uwe Mwanga Wa Uzima.


(NZK # 24) JINA LA YESU TAMU

1. Jina Lake Yesu Tamu Tukilisikia,
Hutupoza, Tena Hamu Hutuondolea.

2. Roho Ilioumia Kwalo Hutibika,
Chakula, Njaani Pia; Raha, Tukichoka.

3. Jina Hili Ni Msingi, Ngao, Ngome, Mwamba,
Kwa Hili Napata Ungi, Kwangu Ni Akiba.

4. Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Na Amina, Mali Yangu Yote!

5. Moyo Wangu Hauwezi Kukusifu Kweli;
Ila Sifa Zangu Hizi, Bwana, Zikubali.


(NZK # 25) TAJI MVIKENI

1. Taji Mvikeni. Taji Nyingi Sana,
Kondoo Mwake Kitini, Bwana Wa Mabwana;
Nami Tamsifu Alikufa Kwangu,
Ni Mfalme Mtukufu, Seyidi Wa Mbingu.

2. Taji Mvikeni Mwana Wa Bikira;
Anazovaa Kichani Aliteka Nyara;
Shilo Wa Manabii Mchunga Wa Watu
Shina Na Tanzu Ya Yesu Wa Bethliehemu.

3. Taji Mvikeni Bwana Wa Mapenzi;
Jeraha Zake Ni Shani Ni Vito Nya Enzi,
Mbingu Haina Hata Malaika
Awezae Kuziona Pasipo Kushangaa!

4. Taji Mvikeni Bwana Wa Salama;
Kote – Kote Duniani Vita Vitakoma;
Nayo Enzi Yake Itaendelea,
Chini Ya Miguu Yake, Maua Humea.


(NZK # 26) TUTOKAPO TUBARIKI

1. Tutokapo Tubariki, Utupe Kufurahi;
Tuwe Na Upendo Wako, Neema Ya Kushinda.
Nawe Utuburudishe Tukisafiri Chini.

2. Twatoa Sifa, Shukrani Kwa Neno La Injili;
Matunda Yake Wokovu Yaonekane Kwetu;
Daima Tuwe Amini Kwa Kweli Yako, Bwana.

3. Siku Zetu Zikizidi Tuzitoe Kwa Yesu;
Tuwe Na Nguvu Moyoni Tusichoke Njiani;
Hata Tutakapoona Utukufu Wa Bwana.


(NZK # 26A) TUPE AMANI

1. Mungu Mtukufu Aliyeumba
Pepo Kuvuma Na Radi Kali;
Toa Neema Unapotawala,
Tupe Amani Bwana Wa Wema.

2. Mungu Wa Neema, Nchi Imeacha
Amri Tukufu Na Neno Lako;
Hasira Zako Zisituharibu,
Tupe Amani, Bwana Wa Wema.

3. Mwumbaji Wa Haki, Watu Wabaya
Wamedharau, Utukufu Wako;
Lakini Wema Wako Utadumu;
Endesha Kweli Bwana Wa Wema.

4. Tunakutolea Ibada Safi
Kwa Ajili Ya Wokovu Wako;
Hivi Tunaziimba Sifa Zako;
Wako Uwezo Na Utukufu.


(NZK # 27) TWALITUKUZA JINA LAKO

1. Tena, Mwokozi, Twalitukuza
Jina Lako Lenye Kupendeza,
Twangojea Neno La Amani,
Kabla Hatujakwenda Nyumbani.

2. Tupe Amani Njiani Mwetu,
Wewe U Mwanzo, U Mwisho Wetu;
Dhambini Kamwe Isiingie
Midomo Ikitajayo Wewe.

3. Utupe Amani Usiku Huu,
Ili Gizani Kuwe Nuru Kuu.
Tulinde Kwa Kuwa Kwako Bwana.
Usiku Ni Sawa Na Mchana.

4. Tupe Amani Ulimwenguni
Ndiyo Dawa Yetu Majonzini;
Na Ikitwita Sauti Yako,
Tupe Amani Milele Kwako.


(NZK # 28) JINA LA THAMANI

1. Jina Lake Yesu Tamu, Lihifadhi Moyoni;
Litatufariji Ndugu, Enda Nalo Po Pote.

 • Jina La (Thamani) Thamani, (Thamani)
  Tumai La Dunia
  Jina La (Jina La Thamani-Tamu!) Thamani,
  Furaha Ya Mbinguni.

2. Jina La Yesu Lafaa Kama Ngao Vitani,
Majaribu Yakisonga, Omba Kwa Jina Hili.

3. Jina Hili La Thamani Linatufurahisha,
Anapotukaribisha, Na Tunapomwimbia.

4. Mwisho Wa Safari Yetu Tutakapomsujudu,
Jina Hili Tutasifu Furaha Ya Mbinguni.


(NZK # 29): YESU, NAKUPENDA

1. Yesu Nakupenda, U Mali Yangu,
Anasa Za Dhambi Sitaki Kwangu;
Na Mwokozi Aliyeniokoa
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

2. Moyo Umejaa Mapenzi Tele
Kwa Vile Ulivyonipenda Mbele,
Uhai Wako Ukanitolea
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

3. Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe Tulio Ndambini;
Taji Ya Miiba Uliyoivaa,
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.

4. Mawanda Mazuri Na Masikani
Niyatazamapo Huko Mbinguni,
‘Tusema Na Taji Nitakayovaa
Sasa Nakupenda, Kuzidi Pia.


(NZK # 30) YESU, UNIPENDAYE

1. Yesu Unipendaye Kwako Nakimbilia,
Ni Wewe Utoshaye Mwovu Akinijia.
Yafiche Ubavuni Mwako Maisha Yangu;
Nifishe Bandarini, Wokoe Moyo Wangu.

2. Ngome Nyingine Sina; Nategemea Kwako,
Usinitupe Bwana, Nipe Neema Yako,
Ninakuamania, Mwenye Kuniwezesha;
Shari Wanikingia, Vitani Wanitosha.

3. Nakutaka Mpaji, Vyote Napata Kwako;
Niwapo Muhitaji, Utanijazi Vyako;
Nao Waangukao Wanyonge Wape Nguvu;
Poza Wauguao, Uongoze Vipofu.

4. Mwana Umeniosha Moyo Kwa Damu Yako;
Neema Ya Kutosha Yapatikana Kwako;
Kwako Bwana Naona Kisima Cha Uzima;
Mwangu Moyoni, Bwana, Bubujika Daima.