Nyimbo za Kristo: 11-20

(NZK # 11) JINA LA BWANA LI HERI

1. Sauti Zote Ziimbe, Jina La Yesu Li Heri!
Sifa Za Mfalme Mungu, Jina La Yesu Li Heri!

 • Jina Li Heri Jina Liheri, Jina La Yesu Li Heri!
  Jina Li Heri, Jina Li Heri, Jina La Yesu Li Heri!

2. Hofu Zote Latuliza Jina La Yesu Li Heri!
Mwenye Dhambi Hukubali Jina La Yesu Li Heri!

3. Huvunja Nguvu Za Dhambi, Jina La Yesu Li Heri!
Damu Yake Hutakasa, Jina La Yesu Li Heri!

4. Sauti Yake Nitamu, Jina La Yesu Li Heri!
Wakaburini Husikia, Jina La Yesu Li Heri!

5. Lugha Maelf(U) Zitaimba, Jina La Yesu Li Heri!
Astahili Mwana-Kondoo, Jina La Yesu Li Heri!


(NZK # 12) MSIFU MUNGU

Msifu Mungu Wa Neema,
Enyi Viumbe Po Pote;
Wa Juu Pia Sifuni Baba,
Mwana Naye Roho! [Amin]

(SDA Hymnal 694)
PRAISE GOD FROM WHOM

Praise God, From Whom All Blessings Flow;
Praise Him, All Creatures Here Below;
Praise Him Above, Ye Heavenly Host;
Praise Father, Son, And Holy Ghost.
AMEN.


 

(NZK # 13) YESU UJE KWETU

1. Umetuahidi Ya Kwamba Wawili
Watatu, Kwa Jina, Lako Wakija,
Utawabariki Kwa Hivi Leo
Twapiga Magoti Nyumbani Pako.

 • Yesu Uje Kwetu Utubariki,
  Yesu Uje Kwetu Uwe Karibu.

2. Umekuwa Nasi Siku Nyingine
Tunakuhitaji Mpaka Mwisho.
Uje Mkombozi; Tupe Neema;
Tusikie Yesu Utubariki.

3. Uje Utawale Sauti Zetu:
Nyimbo, Nazo Sala Uzingize.
Imani Izidi, Ikamilike;
Pendo Liwe Safi, Na Njia Nuru.


(NZK # 14) NITEMBEE NAWE

1. Nitembee Nawe Mungu,
Alivyotembea Enok;
Mkono Wangu Uushike;
Unene Nami Kwa Pole;
Ingawa Njia Siioni,
Yesu Nitembee Nawe.

2. Siwezi Tembea Peke;
Pana Dhoruba Mbinguni;
Mitego Ya Miguu, Elfu;
Adui Wengi Hufichwa;
Uitulize Bahari,
Yesu Nitembee Nawe.

3. Ukinishika Mkono,
Anasa Kwangu Hasara;
Kwa Nguvu Nitasafiri;
Tautwika Msalaba;
Hata Mji Wa Sayuni,
Yesu Nitembee Nawe.


(NZK # 15) NENA ROHONI YESU

1. Nena Rohoni Yesu, Nena Kwa Upole
Sema Kwangu Kwa Pendo, “Huachwi Upweke.”
Fungua Moyo Wangu, Nisikie Mara;
Jaza Roho Na Sifa, Sifa Zako Bwana.

 • Kila Siku Unene, Vile Kwa Upole,
  Nong’oneza Kwa Pole (Kwa Pole) Wa Pendo:
  Daima Utashinda, Uhuru Niwako.
  Nisikie Maneno: “Huachwi Upweke.

2. Nena Kwa Wana Wako, Waonyeshe Njia,
Wajaze Kwa Furaha, Fundisha Kuomba;
Wajifunze Kutoa Maisha Kamili,
Wahimize Ufalme, Tumwone Mwokozi.

3. Nena Kama Zamani, Ulipoitoa
Sheria Takatifu: Niiweke Pia;
Nipate Kutukuza Wewe Mungu Wangu,
Mpanzi Yako Tena, Daima ‘Kusifu.


 

(NZK # 16) NINAKUHITAJI

1. Bwana Ninakuhitaji! Ni Mpofu, Maskini;
Unishike Mkononi, Kwako Napata Nguvu.

 • Kila Saa, Kila Saa Bwana Ninakuhitaji;
  Kila Saa, Kila Saa, Unilinde Kila Saa.

2. Univute Na Mavazi Ya Usikivu Wako;
Nguo Zangu Ni Machafu, Nazitamani Zako.

3. Wewe Ukiniongoza Nitakwenda Salama;
Nenda Nani Siku Zote, U Nuru Na Uzima.

4. Na Ikiwa M-Beleni Sehemu Yangu Ngumu,
Au Ikiwa Furaha, Unilinde Kila Saa.


 

(NZK # 17) SI MIMI, KRISTO

1. Si Mimi, Kristo Astahili Sifa;
Si Mimi, Kristo Ajulikane;
Si Mimi, Kristo Katika Maneno,
Si Mimi, Kristo Kwakila Tendo.

2. Si Mimi, Kristo, Kuponya Huzuni;
Kristo Pekee, Kufuta Machozi;
Si Mimi, Kristo, Kubeba Mzigo;
Si Mimi, Kristo, Kupunga Hofu.

3. Kristo Pekee, Pasipo Kujisifu;
Kristo Pekee, Na Nizungunze,
Kristo Pekee, Na Hakuna Kiburi;
Kristo Pekee, Sifa Yangu Ife.

4. Kristo Pekee, Mahitaji Atoe,
Si Mimi, Kristo, Kisima Changu;
Kristo Pekee, Kwa Mwili Na Kwa Moyo;
Si Mimi, Kristo, Hata Milele.


(NZK # 18) MWOKOZI, KAMA MCHUNGA

1. Mwokozi Kama Mchunga Utuongoze Leo;
Ututume Malishoni, Fanya Tayari Boma.
Bwana Yesu, Peke Yako, Umetuvuta Kwako.

2. Tu Wako, Uwe Rafiki, Uwe Mlinzi Wetu;
Kundi Lako Ulilinde, Tusivutwe Na Dhambi;
Bwana Yesu Tusikie, Tukiomba, Samehe.

3. Umetuahidi Kwamba, Utakubali Watu,
Utawahurumia Na Utawapa Neema;
Bwana Yesu, Tunapenda, Kuwa, Mapema.


 

(NZK # 19) MSALABANI PA MWOKOZI

1. Msalabani Pa Mwokozi, Hapo Niliomba Upozi,
Moyo Wangu Ulitakaswa, Na Asifiwe.

 • Na Asifiwe,
  Na Asifiwe.
  Alitukomboa Kwa Damu,
  Na Asifiwe.

2. Chini Ya Mti Msumbufu, Niliomba Utakatifu,
Alinikomboa Kwa Damu, Na Asifiwe.

3. Kwa Ajabu Ninaokoka, Yesu Anakaa Moyoni;
Mtini Alinifilia, Na Asifiwe.

4. Damu Ya Yesu Ya Thamani, Huniokoa Makosani;
Huniendesha Wokovuni, Na Asifiwe.


(NZK # 20) MUNGU WETU YEYE MWAMBA

1. Mungu Wetu Yeye Mwamba, Kimbilio Taabuni;
Msaada Penye Shida Ulio Karibu Sana.

 • Mwamba Wetu Kutupumzisha,
  Yu Kivuli Kuburudusha,
  Yu Mwongozi Katika Njia,
  Kimbilio Taabuni.

2. Mchana Usiku, Yule Kimbilio Taabuni,
Hivyo Hatutaogopa, Kwani Yu Karibu Sana.

3. Iwayo Yote, Yeye Tu, Kimbilio Taabuni,
Twajua Yeye Mlinzi Aliye Karibu Sana.

4. Mungu Wetu Ficho Kwetu, Kimbilio Taabuni.
Siku Zote Uwe Boma Lililo Karibu Sana.