Nyimbo za Kristo: 1-10

(NZK # 1) U-MTAKATIFU, MTAKATIFU.

1. Umtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri Sifa Zako Tutaimba;
Umtakatifu, Bwana Wa Huruma,
Mungu Wa Vyote Hata Milele.

2. Umtakatifu! Na Malaika,
Wengi Wengi Sana Wanakuabudu
Wote; Elfu Na Maelfu Wanakusujudu,
Wa Zamani Na Hata Milele.

3. U Mtakatifu! Imgawa Giza,
Lakuficha Fahari Tusiione,
U Mtakatifu! Wewe Peke Yako,
Kamili Kwa Uwezo Na Pendo.


(NZK # 2) TWAMSIFU MUNGU

1. Twamsifu Mungu Mwana Wa Upendo,
Aliyetufia Na Kupaa Juu.

 • Aleluya! Usifiwe,
  Aleluya! Amin;
  Aleluya Usiwe,
  Utubariki.

2. Twamsifu Mungu, Roho Mtukufu,
Akatufunulia Mwokozi Wetu.

3. Twamsifu Mwana, Aliyetufia,
Akatukomboa Na Kutuongoza.

4. Twamsifu Mungu, Wa Neema Yote,
Aliyetwaa Dhambi, Akazifuta

5. Tuamshe Tena,Tujaze Na Pendo;
Moyoni Uwashe Moto Wa Roho


(NZK # 3) MUNGU ATUKUZWE

1. Mungu Atukuzwe, Kwa Mambo Makuu,
Upendo Wake Ulitupa YESU,
Aliyejitoa Maisha Yake,
Tuwe Nao Uzima Wa Milele.

 • Msifu, Msifu Dunia Sikia;
  Msifu, Msifu, Watuwafurahi;
  Na Uje Kwa Baba, Kwa Yesu Mwana
  Ukamtukuze Kwa Mambo Yote.

2. Wokovu Kamili Zawadi Kwetu,
Ahadi Ya Mungu Kwa Ulimwengu;
Wanaomwamini Na Kuungama,
Mara Moja Wele Husamehewa.

3. Alitufundisha Mambo Makuu,
Alihakikisha Wokovu Wetu;
Lakini Zaidi Ajabu Kubwa,
Yesu Atakuja Na Tutamwona.


(NZK # 4) JINA LA YESU, SALAMU.

1. Jina La Yesu, Salamu! Lisujudieni, Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni Hukumu, Na Enzi Mpeni.
Ninyi Mbinguni Hukumu, Na Enzi Mpeni.

2. Enzi Na Apewe Kenu, Watetea Dini; Watetea Dini;
Mkuzeni Bwana Wenu, Na Enzi Mpeni.
Mkuzeni Bwana Wenu, Na Enzi Mpeni.

3. Enyi Mbegu Ya Rehema Nanyi Msifuni; Nanyi Msifuni;
Mmeponya Kwa Neema, Na Enzi Mpeni.
Mmeponya Kwa Neema, Na Enzi Mpeni.

4. Wenye Dhambi Kumbukeni Ya Msalabani,Ya Msalabani.
Kwa Furaha Msifuni, Na Enzi Mpeni.
Kwa Furaha Msifuni, Na Enzi Mpeni.

5. Kila Mtu Duniani Msujudieni, Msujudieni,
Kote-Kote Msifuni, Na Enzi Mpeni.
Kote-Kote Msifuni, Na Enzi Mpeni.

6. Sisi Na Wao Pamoja Tu Mumo Sifani, Tu Mumo Sifani.
Milele Sifa Ni Moja, Ni ‘Enzi Mpeni’.
Milele Sifa Ni Moja, Ni ‘Enzi Mpeni.’


(NZK # 5) NA TUMWABUDU HUYO MFALME

1. Natumwabudu Huyo Mfalme,
Sifa Za Nguvu Zake Zivume;
Ni Ngao Ni Ngome Yeye Milele,
Ndizo Sifa Zake Kale Na Kale.

2. Tazameni Ulimwengu Huu,
Uliyoumbwa Ajabu Kuu;
Sasa Umewekwa Pahali Pake,
Hata Utimize Majira Yake.

3. Kwa Ulinzi Wako Kwetu Bwana,
Twakushukuru U Mwema Sana;
Hupewa Chakula Kila Kiumbe,
Kila Kitu Kina Mahali Pake.

4. Wanadamu Tu Wanyonge Sana,
Twakutumaini Wewe Bwana;
Kamwe Haupungui Wako Wema,
Mkombozi Wetu Rafiki Mwema.


(NZK # 6) KUMEKUCHA KWA UZURI

1. Kumekucha Kwa Uzuri.
Nafumbua Macho;
Baba Amenihifadhi,
Ni Wake Mtoto.

2. Bwana Ni Leo Kutwa
Ulinzini Mwako;
Nisamehe Dhambi Niwe
Mikononi Mwako.

3. Roho Wako Anikae
Moyoni Daima;
Anitakase Nione
Uso Wako Mwema.


(NZK # 7) MUNGU MSAADA WETU

1. Mungu Msaada Wetu Tangu Miaka Yote,
Ndiwe Tumaini Letu La Zamani Zote.

2. Kivuli Cha Kiti Chako Ndiyo Ngome Yetu,
Watosha Mkono Wako Ni Ulinzi Wetu.

3. Kwanza Havijakuwako Nchi Na Milima,
Ndiwe Mungu; Chini Yako Twakaa Salama.

4. Na Miaka Elfu Ni Kama Siku Moja Kwako,
Utatulinda Daima. Tu Wenyeji Wako.

5. Bwana Msaada Wetu Tangu Miaka Yote,
Mlinzi Wetu Na Ngome, Daima, Milele.


(NZK # 8) UJE MKOMBOZI

1. Unisikie Ninapolia, Uje M-Kombozi;
Moyo Wangu Wakutazamia, Uje M-Kombozi.

 • Nimepotea Mbali Na Kwangu, Nimetanga Peke Yangu;
  Unichukulie Sasa Kwako: Uje M-Kombozi.

2. Sina Pahali Pa Kupumzika, Uje M-Kombozi;
Unipe Raha, Nuru, Uzima. Uje M-Kombozi.

3. Nimechoka Njia Ni Ndefu, Uje M-Kombozi;
Macho Yako Kuona Nataka, Uje M-Kombozi.

4. Bwana Daima Hutanidharau, Uje M-Kombozi;
Kilio;Changu Utanijibu, Uje M-Kombozi.


 

(NZK # 9) MWUMBAJI, MFALME

1. Mwumbaji, Mfalmevitu Vyote Vyako;
(Ni Kwa Ukarimu Wako Ninabarikiwa) X2

2. Uliyeniumba,Nakutegemea;
(Sina Budi Kuzisifu Hisani Zako Kuu) X2

3. Nitatoa Nini? Kwanza Vitu Vyote Vyako.
(Upendo Wako Wadai Moyo Wa Shukrani) X2

4. Nipewe Neema,Niwe Nauwezo
(Wa Kuishi Kwako, Bwana: Siku Zangu, Zako) X2


(NZK # 10) KRISTO WA NEEMA YOTE

1. Kristo Wa Neema Yote; Imbisha Moyo Wangu;
Mifulizo Yabaraka; Inaamsha Shangwe Kuu.
Unifunze Nikupende, Nikuandame Kote,
Moyo Wangu Ukajae; Furaha Na Tumai.

2. Namshukuru Sana Bwana, Aniwezesha Huku.
Salama Aniongoza, Hata Kule Nyumbani.
Yesu Alinitafuta, Njiani Mbali Kwake,
Akatoa Damu Yake, Nipone Hatarini.

3. Kweli Mimi Mwiwa Mkubwa, Wa Neema Daima;
Wema Wako Unifunge, Zaidi Kwako Bwana,
Ili Nisivutwe Tena, Kukuacha Ee Mponya,
Nitwalie Moyo Wangu, Uwe Wako Kamili.