125-002: “Ee Bwana, Usione Hasira Nyingi”.

SAA YA IBADA NA MAOMBI.

 • (a) http://tgvs.org/archives/2174
 • (b) 125-002: Ee Bwana, Usione Hasira Nyingi”.
 • (c) Jamii: Saa Ya Ibada
 • (d) Msisitizo: Kulilia msamaha wa Mungu
 • (e) Fungu Kuu: Isaya 64: 8 – 9
 • (f) Wimbo: NZK # 122:  Yote namtolea Yesu

 

Isaya 64: 8 – 9 (NKJV)

 • 8 Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
 • 9 Ee Bwana, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.

UTANGULIZI

 • Ombi la nabii Isaya katika aya hii ni mfano wa kuigwa. Watu walijua kuwa wlimkosea Mungu kabisa; kuwa walitenda dhambi hivyo kuasi dhidi Yake, walitambua kuwa walilistahili ghadhabu Yake; lakini walimsihi Bwana “asione hasira nyingi, wala asiukumbuke uovu siku zote.
 • Wapendwa, hata Bwana yu tayari kusamehe makosa, na dhambi, punde tunapomlilia, na kurudi Kwake.

 

MAFUNGU MENGINE:

 •  Zaburi 6:1
  • 1 Bwana, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
 •  Zaburi 38: 1
  • 1 Ee Bwana, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.
 •  Zaburi 74:1
  • 1 Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?

 

NUKUU YA ROHO YA UNABII

 • “Katika neno lake, Mungu anajilinganisha Mwenyewe kama mfinyanzi na na watu Wake kama udongo. Kazi Yake ni kuwafinyanga na kuwabadilisha wawe na tabia Yake mwenyewe. Somo wanalotakiwa kujifunza ni utii na unyenyekevuNafsi yapaswa kuondolewa kabisa. Kama maelekezo ya kiungu yatazingatiwa, kama nafsi itasalimishwa chini ya mapenzi ya Mungu, mkono wa Mfinyanzi utazalisha chombo bora zaidi”. (Ellen G. White, In Heavenly Places; p.28.1)

TUFANYE NINI BASI?

KUMBUKA!

 • (1) Kumbuka kuomba msamaha Wake
 • (2) Kumbuka kumuogopa BWANA!
 • (3) Kumbuka kutotenda dhambi tena!
 • (4) Kumbuka kumtolea shukrani milele
 • (5) Kumbuka kuzisimulia sifa Zake kizazi kwa kizazi.
 • (6) Kumbuka kujisalimisha Kwake leo
 • (7) Kumbuka kushika Amri na Hukumu Zake

Zaburi 103:13 – 14

 • 13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.
 • 14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

Zaburi 74:1-2

 • 1 Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?
 • 2 Ulikumbuke kusanyiko lako, Ulilolinunua zamani. Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako, Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.

Zaburi 79:13

 • 13 Na sisi tulio watu wako, Na kondoo za malisho yako, Tutakushukuru milele; Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi.

 


MWITIKIO WETU:

NZK # 122:  Yote namtolea Yesu

 1. Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake: Ninavutwa na upendo, kwa hivyo, najitoa.
 2. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake; Nimeacha na anasa, kwako Yesu nipokee.
 3. Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako; Nipe Roho yako, Bwana, anilinde daima.
 4. Yote namtolea Yesu, nami naona sasa, Furaha ya ukombozi, nasifu jina Lake. 
 •  Yote Kwa Yesu, Yote Kwa Yesu, Upendo Wako Hushinda; Yesu, Natoa.

 OMBI LA MWISHO

 Zaburi 119:94

 • Mimi ni wako, uniokoe, Kwa maana nimejifunza mausia yako.

 BWANA ATUBARIKI SOTE!

©Sauti Ya Injili SDA.