Jumanne: (12/13/16) Kifo cha Kristo

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA

 • Wiki hii: Mkombozi wa Ayubu
 • Fungu la kukariri: Isaya 53:4
 • Kitengo: Kila Jioni
 • http://tgvs.org/archives/2158
 • Jumanne: (12/13/16) Kifo cha Kristo

Isaya 53:4

 • Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

 

KIFO CHA KRISTO

Mafungu yafuatayo yanatwambia nini kuhusu Kristo na namna tunavyotakiwa kumtazama?

1 Yohana 2:6,

 • Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani Yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama Yeye alivyoenenda.

Wagalatia 4:19.

 • Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;

 

YESU NI MFANO PEKEE TULIO NAO

Bila maswali, Yesu ni mtu wa kumwiga. Maisha yake – tabia Yake – Yeye ni mfano ili kwamba wale wote wanaomfuata wanatakiwa kuomba neema ya Mungu ili wafanane Naye. Yesu ni mfano pekee tulio nao katika suala la namna ya kuishi maisha ambayo Mungu anataka tuyaishi.

Bado, Yesu hakuja hapa duniani kwa lengo la kutupatia mfano tu. Hali yetu ya dhambi ilihitaji kitu kingine zaidi ya kuboreshwa kwa tabia, kama vile kufanya matengenezo ya tabia zetu na kutufanya tufanane Naye. Hivyo vyote vilikuwa ni kazi Yake Yeye kama Mkombozi.

Tulihitaji zaidi ya hao; tulihitaji Mbadala, mtu wa kulipa deni la dhambi zetu. Hakuja ili tu aishi maisha makamilifu iwe mfano kwetu sisi wote; pia alikuja kwa lengo la kufa kifo ambacho tulitakiwa kufa ili kwamba yale maisha Yake makamilifu yafanywe kuwa yetu.

 

MAFUNGU YAFUATAYO YANATUFUNDISHA NINI JUU YA UMUHIMU WA KIFO CHA KRISTO KWA AJILI YETU?

Marko 8:31

 • Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.

Luka 9:22

 • Akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.

Luka 24:7

 • Akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu.

Wagalatia 2:21.

 • Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure.

 

Ilimpasa Yesu afe kwa ajili yetu ili kutimiza dai la sheria, japo sheria ndio kiini cha maisha ya Kikristo, sicho kinachomwokoa aliyeanguka. “Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria” (Wagalatia 3:21).

Kama kuna sheria yo yote ambayo ingeweza kumwokoa mdhambi, ingekuwa ni sheria ya Mungu, lakini hata hiyo haiwezi kutuokoa. Ni maisha makamilifu tu ya kielelezo chetu, Yesu, ndiyo yanayoweza kutuokoa, na hivyo Kristo alikuja kujitoa yeye kama “dhabihu moja idumuyo hata milele” (Waebrania 10:12).

 

MASWALI YA MJADALA

Ni kwa vipi kumbukumbu zako za ushikaji wa sheria zinakuonesha hitaji lako la Mbadala?


 

NYONGEZA

Sikiliza Audio ya Somo linalosema: