106-002: Tamaa

MWENDELEZO WA MASOMO YA BIBLIA KUHUSU UZENZI WA TABIA YA KIKRISTO

OMBI: Baba Yetu na Mungu wetu, asante kwa ajili ya nafasi nyingine uliyotupatia kulitafakari Neno Lako. Tunakaribisha Uwepo Wako sasa, Bwana. Twasihi Roho Wako aendelee kutufundisha. Tufungue masikio yetu ya ndani, na kutupa usikivu wa Kina. Lakini zaidi ya yote, ebu injili hii ya Leo, ikapate kutusogeza karibu sana na Msalaba Wako. Tuandae kwa ajili ya Marejeo Yako, Bwana. Twasema asante kwa kusikia ombi hili fupi. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Kristo Yesu, aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.


 

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU

 1. Utangulizi
 2. Moyo na asili ya Tamaa
 3. Tamaa na wasioamini
 4. Mifano ya Tamaa katika Biblia
 5. Siri ya ushindi dhidi ya tamaa
 6. Hitimisho: Tufanye nini basi?

TAMAA (Utangulizi)

Maandiko matakatifu, yaani Biblia, inalaani tamaa ya kila aina. Wauumini wanatakiwa kujizuia na kujitenga mbali na dhambi hii ya Tamaa.

MATUMIZI YA NENO “TAMAA”

Katika ulimwengu wa leo, neno “tamaa” linatumika hususan kumaanisha hamu ya uasherati, au hisia za kimapenzi au ngono.

Katika Agano la Kale neno “tamaa” limetumika kama nomino na inatafsiriwa katika Biblia ya KJV toka kwenye maneno ya Kiebrania, miongoni mwa mambo mengine, kama ifutavyo:

 1. Hamu kubwa kwa vita takatifu (Kutoka 15:9);
 2. Tamaa/hamu ya chakula (Zaburi 78);
 3. Hamu mbaya sana kiasi kwamba neno “ukaidi” waweza kuwa tafsiri sahihi zaidi (Zaburi 81:12), na
 4. Hamu ya ngono [sexual desire] (Mithali 6:25).

Katika Agano Jipya, neno “tamaa” [Gk. epithymɩa]  linatumika kumaanisha mambo yafuatayo:

 1. Tafsiri ya jumla kama “tamaa” (Marko 4:19).
 2. Hamu safi ya Kristo (Luka 22:15),
 3. Hamu ya kuwa pamoja na Kristo (Flp. 1:23),
 4. Hamu ya kutenda uovu (Yohana 8:44),
 5. Hamu ya uasherati (Mathayo 5:28)
 6. Tamaa ya Uasherati (Warumi 1:24)
 7. Tamaa ya kutenda dhambi (Warumi 6:12)
 8. Tamaa ya “matendo ya mwili” (Wagalatia 5:16, 24)

Mbali na epithymɩa, Agano Jipya pia hutumia maneno mengine kama [Gk. órexis, thymós, hedone, na pathos]. Maneno hayo yanapotumika ni vyema kuhakiki kila tumizi moja moja, ili kupata tafsiri sahihi iliyokusudiwa katika kila fungu katika Biblia.


 

TAMAA INA ASILI YAKE KATIKA MOYO NA AKILI

Matayo 5:27-28

 • 27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
 • 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Mwanzo 3:6

 • Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Ayubu 31:1

 • Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?

Yakobo 1:12-15

 • 12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
 • 13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
 • 14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
 • 15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Mithali 6:20-29;

 • 20 Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.
 • 21 Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako.
 • 22 Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe.
 • 23 Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
 • 24 Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
 • 25 Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
 • 26 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani
 • 27 Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe?
 • 28 Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?
 • 29 Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.

 

TAMAA NI ASILI KWA WASIOAMINI

Warumi 1:18-27

 • 18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
 • 19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
 • 20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;
 • 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
 • 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
 • 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
 • 24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
 • 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
 • 26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
 • 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

Warumi 7:5

 • Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.

 

1 Wakorintho 6:9-11

 • 9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
 • 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
 • 11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

1 Petro 4:1-3

 • 1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
 • 2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
 • 3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

 

2 Petro 2:14-18

 • 14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;
 • 15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;
 • 16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.
 • 17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.
 • 18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;

 

MIFANO MICHACHE YA TAMAA

 

(1) Tamaa inayojidhihirisha katika shauku ya mahusiano haramu ya kimapenzi

 

Mwanzo 39:6-12 (Yusufu & mke wa Potifa)

 • 6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.
 • 7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
 • 8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
 • 9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
 • 10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.
 • 11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;
 • 12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.

2 Samweli 11:2-5 (Daudi na Bath-sheba)

 • 1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu.
 • 2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.
 • 3 Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
 • 4 Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.
 • 5 Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito.

 

(2) Tamaa ya fedha

1 Timotheo 6:9-10

 • 9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
 • 10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

1 Timotheo 3:3

 • 1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.
 • 2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
 • 3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
 • 4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;

 

(3) Tamaa/ hamu haramu ya Israeli na Yuda kufanya muunganiko na mataifa mengine

 • Angalizo: falme zote walitaka usalama kutoka ushirikiano kama huo, badala ya kumwamini Mungu.
 • Soma: Ezekieli 23:1-21

 

KWA NEEMA YA MUNGU, WAUMINI WANAPASWA KUISHINDA TAMAA, NA KUWA NA KIASI

 

Wagalatia 5:16-21

 • 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
 • 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
 • 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
 • 19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
 • 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
 • 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Waefeso 3:5-7

 • 5 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
 • 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.
 • 7 Basi msishirikiane nao.

 

SIRI YA USHINDI DHIDI YA TAMAA

Ayubu 31:1

 • Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?

1 Yohana 2:16

 • Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani Yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama Yeye alivyoenenda.

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

1 Wakorintho 9:27

 • 27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Wagalatia 5:24-25

 • 24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
 • 25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

Waefeso 4:22;

 • 22 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
 • 23 na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
 • 24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

1 Wathesalonike 4:3-5

 • 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
 • 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
 • 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

2 Timotheo 2:22

 • Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

Tito 2:11-13

 • 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
 • 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
 • 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

1 Petro 2:11

 • 11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
 • 12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

 

OMBI. Asante Bwana kwa mwendelezo wa masomo haya kuhusu Ujenzi wa Tabia ya Kikristo. Tukumbuse kuwa sisi ni “wapitaji na wasafiri”, na hatuna budi “kuziepuka tamaa za mwili zipiganazo na roho”. Naomba kwa ajili ya mtu mmoja atakayesoma/ sikia injili hii, mtu fulani ambaye bado anasumbuliwa na dhambi hii ya tamaa. Naomba kwa ajili ya kijana mmoja, binti mmoja, mzee mmoja, mama mmoja, ambaye hajapata ushindi katika swala hili.

Tusamehe sote Bwana, sisi ni wenye dhambi mbele zako, lakini tuna ujasiri wa kuja Kwako kwa sababu utatupatia Roho Wako Mtakatifu, na hakika tutakuwa washindi. Tusaidie tujinyenyekeze basi mbele Zako, na kuomba, na kuutafuta Uso Wako kila saa, na kuikimbia tamaa, na kuziacha njia zetu mbaya.

Asante Bwana kwa neema Yako “iwaokoayo wanadamu wote.” Neema isiyobagua, Neema iliyofunuliwa kwetu sote, Neema inayotufundisha “kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu”

Siku moja utakapokuja, Ee Bwana, tukapate kuuona Uso Wako.

Asante Bwana kwa ombi hili fupi. Tumeshukuru, na twaja katika Jina la Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, Amen.


 

BWANA ATUBARIKI SOTE!

 

© Sauti Ya Injili SDA: www.tgvs.org