102-001: “Mimi Hapa, Nitume Mimi”

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

 

INJILI FUPI YA ASUBUHI

 • 102-001:  “Mimi Hapa, Nitume Mimi”
 • Category: Masomo katika Biblia
 • Neno Kuu: Utayari wa Utume
 • Fungu Kuu: Isaya 6:8
 • http://tgvs.org/archives/2093
 • Mobile App: The Gospel’s Voice

OMBI: Baba yetu Mpendwa, asante tena kwa nafasi nyingine ya kusoma na kusikiliza Injili Yako. Tunaalika uwepo wa Roho Mtakatifu katika tafakari hii fupi ya Injili ya Leo. Tusamehe, tuokoe, tutakase, tuandae kwa ajili ya marejeo Yako. Ebu Injili hii fupi ikapate kutusogeza karibu sana nawe. Tunakushukuru kwa yote, na twaja katika Jina la Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, Amina.


 

Isaya 6:8

 • Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.

 

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU:

Katika maandiko matakatifu tunaamriwa kufanya mambo yafuatayo yanayolandana na Utume katika shamba la Bwana. Mambo makuu sita ni haya:

 1. Kwenda kwa Mataifa
 2. Kutangaza Wokovu wa Bwana
 3. Kuombea Utume wa Injili
 4. Kuhubiri Injili
 5. Kutuma/ kufadhili wahubiri
 6. Kuwasaidia wamisionary

 

KWENDA KWA MATAIFA

 • Zaburi 96:2-3
  • 2 Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
  • 3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.
 • Zaburi 96:10
  • Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.

 

KUTANGAZA WOKOVU WA BWANA

 • Zaburi 96:2
  • 2 Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

 

KUOMBEA UTUME

Tunapaswa kuendelea kuwaombea wainjilisti/ wamisionary/ wachungaji, n.k

 • Luka 10:2
  • Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.
 • Wakolosai 4:3–4
  • 2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
  • 3 mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,
  • 4 ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.

 

KUHUBIRI INJILI

 • Matendo 10:42
 • Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu.

 

KUDHAMINI/ KUPELEKA WAMISIONARI/ WAHUBIRI

Warumi 10:14–15

 • (13)    Kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
 • (14a)  Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini?
 • (14b) Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia?
 • (14c) Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
 • (15a) Tena wahubirije, wasipopelekwa?
 • (15b) Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!

 

HITIMISHO LA SOMO

Matayo 9:35-38

 • 35 Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
 • 36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
 • 37 Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.
 • 38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

 

Kumbuka ndugu mpendwa, Yesu aongei tu kwa maneno, la hasha! Alitufundisha umuhimu wa utume kwa vitendo.

 1. Alizunguka katika miji yote
 2. Alizunguka katika vijiji vyote
 3. Alifundisha katika masinagogi yao
 4. Alihubiri habari njema za ufalme wake
 5. Aliponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
 6. Alijawa na Huruma nyingi
 7. Alitukumbusha akisema: “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache”

 

TUFANYE NINI BASI NA INJILI YA LEO?

Tunapaswa kuiga mfano wa Yesu na kudumu kuendelea kufanya mambo yafuatayo:

 1. Uinjilisti wa nyumba kwa nyumba
 2. Kumshuhudia Kristo kwa Mataifa
 3. Kutangaza Wokovu wa Bwana
 4. Kuombea Utume wa Injili
 5. Kuhubiri Injili Ulimwenguni
 6. Kutuma/ kufadhili wahubiri
 7. Kuwasaidia wamisionari
 8. Kuomba ili “Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake”
 9. Kujiweka tayari kwa ajili ya Marejeo Yake.

 

ANGALIZO:

 • Fundisho hili la Utume wa Injili halihusu tu wachungaji na wanateologia, ni mwito mtakatifu kwa kila mmoja wetu kushiriki kwa namna moja au nyingine. Swali muhimu, ndugu mpendwa ni hili: Je, uko tayari?

 

MFANO WA KUIGWA = (Isaya)

 • Isaya 6:8
 • Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.

 

SAUTI YA INJILI

{Mpendwa ebu sikia Sauti Ya Bwana kwako leo}

 

 • Yohana 17:18
  • Kama vile ulivyonituma Mimi ulimwenguni, Nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
 • Matayo 28:19-10
  • 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, Mimi nipo pamoja nanyi SIKU ZOTE, hata ukamilifu wa dahari.

 

MWITIKIO WETU LEO

Nyimbo za Kristo # 107.

 • Nipo Bwana, Nitume
 • Hark! The Voice of Jesus
 • Sauti ni yake Bwana, “Kwenda, nani tayari“; Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
 • Kwa kudumu amaita, Zawadi atatoa; Nani atakayejibu “Nipo Bwana, nitume.”
 • Kana huwezi safari, Hata Nchi za mbali, Pana watu karibuni Wasio mjua Yesu;
 • Kama huwezi kusema Jinsi ya malaika, Waweza kuutangaza, Upendo wa mwokozi.
 • Ingawa huwezi kuwa, Mkesha mlangoniUkiwatolea watu Nafasi ya uzima;
 • Kwa sala na kwa sadaka Watoa msaada, Kama Harun mwaminifu, Kuinua Mikono.
 • Roho za watu zikifa, Bwana akikuita, Usiseme kwa uvivu, “Hakuna kazi kwangu.”
 • Kwa furaha anza kazi Ile akiyokupa, Ukajibu mara moja, “nipo Bwana, nitume.”

 

OMBI LA MWISHO

Sauti ni yake Bwana, “Kwenda, nani tayari”; Mavuno yanakawia, Nani atayavuna? Kwa kudumu amaita, Zawadi atatoa; Nani atakayejibu “Nipo Bwana, nitume”

Na hili ndilo ombi letu Bwana, tusaidie ili tuweze kujubu kwa ujasiri leo: Nipo Bwana, Nitume Mimi. Ee Bwana tusaidie tuwe na utayari kutumika shambani Mwako. Tusamehe makosa yetu. Tuimarishe kusaidia kazi Yako kwa hali na mali, kila inapowezekana. Tuandae kwa ajili ya Ufalme Wako. Tumeomba haya tukiamini kuwa umesikia na utatenda sawasawa na fadhili Zako. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Kristo Yesu, Amina.


 

© Sauti Ya Injili SDA { www.tgvs.org }