04-Usiombee Wafu

MFULILIZO WA MASOMO MAFUPI YA INJILI

 • Mhutubu: Angelo Nyamtema, MD, PhD
 • Kituo: Ifakara-Tanzania, East Africa

Mada: USIOMBE WAFU

UFUPISHO WA SOMO

TORATI 18:9-13

 • 9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.
 • 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
 • 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
 • 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
 • 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.

ZABURI 146:4

 • Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.

MUHUBIRI 9:5

 • kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

1 YOHANA 2:1-2

 • 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
 • 2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE!