03-Njia Ya Uzima
MFULILIZO WA MASOMO MAFUPI YA INJILI
- Mhutubu: Angelo Nyamtema, MD, PhD
- Kituo: Ifakara-Tanzania, East Africa
Mada: Njia Ya Uzima
UFUPISHO WA SOMO
YOHANA 14:5-6
- 4 Nami niendako mwaijua njia.
- 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
- 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
MATENDO 4:12
- Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
WAEBRANIA 9:22
- Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
WALAWI 17:11
- Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
1 YOHANA 2:1-2
- 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
BWANA ATUBARIKI SOTE!