02-Njia Mbili za Umilele
MFULILIZO WA MASOMO MAFUPI YA INJILI
- Mhutubu: Angelo Nyamtema, MD, PhD
- Sehemu: Ifakara-Tanzania, East Africa
Mada: Njia Mbili za Umilele
UFUPISHO WA SOMO
Torati 3:15-17
- 15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;
- 16 kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
- 17 Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia;
Mithali 14:12
- Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
1 Yohana 2:4 (Dhambi ni nini)?
- 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
- 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
BWANA ATUBARIKI SOTE!