103-008 Maombi na Imani

MFULULIZO WA MASOMO MAFUPI KUHUSU MAOMBI

 

OMBI: Baba Yetu na Mungu wetu, asante kwa ajili ya nafasi nyingine uliyotupatia kulitafakari Neno Lako. Tunakaribisha Uwepo Wako sasa, Bwana. Twasihi Roho Wako aendelee kutufundisha. Tufungue masikio yetu ya ndani, na kutupa usikivu wa Kina. Lakini zaidi ya yote, ebu injili hii ya Leo, ikapate kutusogeza karibu sana na Msalaba Wako. Tuandae kwa ajili ya Marejeo Yako, Bwana. Twasema asante kwa kusikia ombi hili fupi. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Kristo Yesu, aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.


 

MAOMBI NA IMANI

 • Maombi mashuhuri yanategemea imani, hasa kwa nia ya kuamini katika uaminifu wa Mungu kuhusu ahadi zake kwa watu Wake.

Muhtasari Wa Mawazo Makuu:

 1. Imani ni muhimu ili kumkaribia Mungu
 2. Imani ni muhimu ili kupokea faida kutoka kwa Mungu
 3. Imani ni muhimu kwa ajili ya maombi ya ufanisi
 4. Mifano ya maombi mashuhuri ya imani
 5. Yesu alijibu maombi ya watu mbalimbali kulingana na Imani waliyokuwanayo Kwake

 

IMANI NI MUHIMU ILI KUMKARIBIA/ KUMWENDEA MUNGU

Waebrania 11:6

 • Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

IMANI NI MUHIMU ILI KUPOKEA FAIDA KUTOKA KWA MUNGU

Mariko 6:5-6

 • 5 Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono Yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.
 • 6 Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha.

Yakobo 5:16-18

 • 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
 • 16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
 • 17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
 • 18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.

Waefeso 3:12

 • 11 kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
 • 12 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.

Waebrania 10:22

 • Na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.

IMANI NI MUHIMU KWA AJILI YA MAOMBI YA UFANISI

Matayo 21:21-22

 • 20 Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara?
 • 21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka.
 • 22 Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.

 

Mariko 11:22-24

 • 22 Yesu akajibu, akamwambia, MWAMININI MUNGU.
 • 23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
 • 24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, AMININI YA KWAMBA MNAYAPOKEA, nayo yatakuwa yenu.

 

Yakobo 1:5-8

 • 5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
 • 6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
 • 7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
 • 8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

 

Yakobo 5:14-15

 • 14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
 • 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

 

MIFANO YA MAOMBI MASHUHURI YA IMANI

 1. 1 Wafalme 18:36-37 Eliya, katika mashindano na manabii wa Baali;
 2. Yakobo 5:17-18          Eliya, kuomba kuhusu mvua;
 3. 1 Wafalme 17:19-22 Eliya na mwana wa mjane;
 4. 2 Wafalme 4:32-35 Elisha na mwana wa Mshunami

 

YESU ALIJIBU MAOMBI YA WATU MBALIMBALI KULINGANA NA IMANI WALIYOKUWANAYO KWAKE

Matayo 9:27-30 (Vipofu wawili)

 • 27 Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.
 • 28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana.
 • 29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, KWA KADIRI YA IMANI YENU MPATE.
 • 30 Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue.

 

Matayo 8:5-13 (Mtumishi wa Akida)

 • 5 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
 • 6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
 • 7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
 • 8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
 • 9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
 • 10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.
 • 11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
 • 12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
 • 13 Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.

 

Matayo 9:20-22, (Mwanamke = ugonjwa wa kutoka damu)

 • 20 Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
 • 21 Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.
 • 22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

 

Matayo 15:21-28 (Binti aliyepagawa sana na pepo)

 • 21 Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.
 • 22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
 • 23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
 • 24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
 • 25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
 • 26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
 • 27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
 • 28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

 

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI LA LEO?

Matayo 7:7, 11.

 • 7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
 • 8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
 • 9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?
 • 10 Au akiomba samaki, atampa nyoka?
 • 11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?

Yeremia 33:3

 • Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Mariko11:24.

 • Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Yohan 14:13-14

 • 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa Jina Langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
 • 14 Mkiniomba neno lo lote kwa Jina Langu, nitalifanya.

Yohana15:7

 • Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Waefeso 3:20

 • Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

1 Yohana 5:14, 15

 • 14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
 • 15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

 


OMBI.

Asante Bwana kwa somo la Leo. Asante kwa ahadi Yako kuwa utakuwa katikati yetu. Naomba Ombi rasmi sasa kwa ajili ya wanamaombi katika Chumba cha Maombi. Watakase, waimarishe, wasamehe makosa yao. Ebu maombi haya ya muungano yakapate kibali mbele Zako. Lakini Bwana, wakumbushe pia wasije wakasahau umuhimu wa maombi ya faragha, mtu mmoja mmoja, kwani katika maombi hayo kuna ushindi mkuu dhidi ya dhambi.

Tusaidie tujinyenyekeze mbele Zako, na kuomba, na kuutafuta Uso Wako, na kuziacha njia zetu mbaya. Tusidie kama familia tukapate kubebeana na kuchukuliana mizigo, kwa sababu kwa kufanya hivyo “tutaitimiza sheria ya Kristo”. Tusaidie tuweze kuomba kila Saa, siku zote za maisha yetu. Tusaidie tuwe na Imani katika Mungu. Siku moja utakapokuja, Ee Bwana, tukapate kuuona Uso Wako.

Asante Bwana kwa ombi hili fipi. Tumeshukuru, na twaja katika Jina La Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, Amen.