103-007 Je, tunapaswa kuomba wakati gani?

   MFULULIZO WA MASOMO MAFUPI KUHUSU MAOMBI

 

OMBI: Baba Yetu na Mungu wetu, asante kwa ajili ya nafasi nyingine uliyotupatia kulitafakari Neno Lako. Tunakaribisha Uwepo Wako sasa, Bwana. Twasihi Roho Wako aendelee kutufundisha. Tufungue masikio yetu ya ndani, na kutupa usikivu wa Kina. Lakini zaidi ya yote, ebu injili hii ya Leo, ikapate kutusogeza karibu sana na Msalaba Wako. Tuandae kwa ajili ya Marejeo Yako, Bwana. Twasema asante kwa kusikia ombi hili fupi. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Kristo Yesu, aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.


 

JE, TUNAPASWA KUOMBA WAKATI GANI?

 Muhtasari wa Mawazo Makuu

 1. Wakati wote
 2. Mchana na Usiku
 3. Kila Siku
 4. Kila Asubuhi
 5. Makesha ya usiku
 6. Kabla ya Mapambazuko
 7. Siku ya taabu yangu
 8. Kabla ya kufanya maamuzi fulani fulani
 9. Mapema sana Alfajiri
 10. Wakati vyombo vyetu vya maisha vinazama
 11. Je, Yesu aliomba muda gani?
 12. Tufanye nini basi na Somo hili la Leo?

 

TUNAPASWA KUOMBA WAKATI WOTE

1 Wathesalonike 5:16-18

 • 16 Furahini siku zote;
 • 17 ombeni bila kukoma;
 • 18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

 

TUNAPASWA KUOMBA MCHANA NA USIKU

Zaburi 88:1

 • Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu Mchana na Usiku nimelia mbele zako.

Zaburi 88:9

 • Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso Bwana, nimekuita kila siku; Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.

 

TUNAPASWA KUOMBA KILA ASUBUHI

 Zaburi 5:3

 • Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.

 

TUNAPASWA KUOMBA KABLA YA MAPAMBAZUKO

 Zaburi 119:146-148

 • 146 Nimekuita Wewe, uniokoe, Nami nitazishika shuhuda zako.
 • 147 Kutangulia mapambazuko naliomba msaada, Naliyangojea maneno yako kwa tumaini.
 • 148 Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku, Ili kuitafakari ahadi yako.

 

TUNAPASWA KUOMBA “SIKU YA TAABU YANGU”

Zaburi 77:1–2, 6   (Siku ya taabu yangu)

 • 1 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.
 • 2 Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.
 • 6 Nakumbuka wimbo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu ikatafuta.

Zaburi 88:2–3  (Kila Saa)

 • 2 Maombi yangu yafike mbele zako, Uutegee ukelele wangu sikio lako.
 • 3 Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai wangu umekaribia kuzimu.

Zaburi 116:3–4

 • 3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;
 • 4 Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu.

 

TUNAPASWA KUOMBA WAKATI VYOMBO VYETU VYA MAISHA VINAZAMA

Matayo 14:25-30 (Petro = Bwana, Niokoe)

 • 25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
 • 26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.
 • 27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.
 • 28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.
 • 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
 • 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

 


 

JE, YESU ALIOMBA MUDA GANI?

Mariko 1:35 (YESU = alfajiri na mapema)

 • 33 Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni.
 • 34 Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
 • 35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
 • 36 Simoni na wenziwe wakamfuata;

 

Yohan 8:1-2 (YESU = Usiku kucha)

 • 1 Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.
 • 2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.

 

Luka 6:12–13 (YESU = usiku kucha)

 • 12 Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.
 • 13 Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume;

 

KUMBUKA WAPENDWA

 • Yesu Kristo anatuombea Usiku na Mchana
 • Yesu Kristo Yu Hai Sikuzote Akituombea

 

YESU KRISTO ANATUOMBEA USIKU NA MCHANA

Zaburi 121

 • 1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
 • 2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
 • 3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;
 • 4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
 • 5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.
 • 6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
 • 7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
 • 8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

 

YESU KRISTO YU HAI SIKUZOTE AKITUOMBEA

Waebrania 7:24-25

 • 24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
 • 25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

 


 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI LA LEO?

 • Tuendelee kudumu katika maombi siku zote za maisha yetu

 

Zaburi 116: 1–2 (AHADI YA BWANA)

 • 1 Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.
 • 2 Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.

 

Zaburi 5:1-2 (OMBI LA LEO)

 • 1 Ee Bwana, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu.
 • 2 Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.

 

Zaburi 119:146-148

 • 146 Nimekuita Wewe, uniokoe, Nami nitazishika shuhuda zako.
 • 147 Kutangulia mapambazuko naliomba msaada, Naliyangojea maneno yako kwa tumaini.
 • 148 Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku, Ili kuitafakari ahadi yako.
 • 149 Uisikie sauti yangu SAWASAWA NA FADHILI ZAKO, Ee Bwana, unihuishe SAWASAWA NA HUKUMU YAKO.

 


OMBI.

Asante Bwana kwa somo la Leo. Asante kwa ahadi Yako kuwa utakuwa katikati yetu. Naomba Ombi rasmi sasa kwa ajili ya wanamaombi katika Chumba cha Maombi. Watakase, waimarishe, wasamehe makosa yao. Ebu maombi haya ya muungano yakapate kibali mbele Zako. Lakini Bwana, wakumbushe pia wasije wakasahau umuhimu wa maombi ya faragha, mtu mmoja mmoja, kwani katika maombi hayo kuna ushindi mkuu dhidi ya dhambi.

Tusaidie tujinyenyekeze mbele Zako, na kuomba, na kuutafuta Uso Wako, na kuziacha njia zetu mbaya. Tusidie kama familia tukapate kubebeana na kuchukuliana mizigo, kwa sababu kwa kufanya hivyo “tutaitimiza sheria ya Kristo”. Tusaidie tuweze kuomba kila Saa, siku zote za maisha yetu. Siku moja utakapokuja, Ee Bwana, tukapate kuuona Uso Wako.

Asante Bwana kwa ombi hili fipi. Tumeshukuru, na twaja katika Jina La Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, Amen.