103-005 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana

MFULULIZO WA MASOMO MAFUPI KUHUSU MAOMBI

 

MTAFUTENI BWANA, MAADAMU ANAPATIKANA.

 • Fungu Kuu: Isaya 55:6-7
 • Neno Kuu: qārāʾ bešēm = kuita

 

Isaya 55:6-7

 • 6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
 • 7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.

 

Kuna wakati fulani Bwana hatapatikana kabisa

 1. Wakati tunajenga kuta za dhambi zetu
 2. Wakati kikombe chetu kimejaa
 3. Wakati tunampuuza Roho Mtakatifu
 4. Wakati mlango wa Rehema Umekwisha

 

Ushahidi wa Kibiblia

 • Matayo 25:11-12
  • 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
  • 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
 • Luka 13:23-25
  • 23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
  • 24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
  • 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
 • Zaburi 32:6
  • Kwa hiyo kila mtu mtauwa Akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.
 • Ufunuo 15:8 (Mlango wa Rehema kufungwa)
  • Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake.
  • Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.

 

MTAFUTENI BWANA

 • Isaya 45:19.
 • 1 Nyakati 28:9.
 • 2 Nyakati 19:3.
 • Ayubu 8:5
 • Zaburi 14:2
 • Zaburi 27:8
 • Zaburi 95:6-7
 • Mithali 8:17
 • Yeremia 29:12-14.
 • Amosi 5:6.
 • Matayo 7:7-8.
 • Matayo 25:11, 12.
 • Luka 13:25.
 • Johana 7:33, 34.
 • Yohana 8:21
 • Yohana 12:35-36.
 • 2 Wakorintho 6:1-2.
 • Waebrania 2:3
 • Waebrania 3:13.
 • Yakobo 4:8.

 

MWITENI, MAADAMU YU KARIBU

 • Isaya 12:6.
 • Isaya 46:13
 • Mwanzo 6:3
 • Torati 4:7.
 • Zaburi 75:1
 • Zaburi 145:18
 • Zaburi 148:14
 • Mithali 1:28
 • 2 Wakorintho 6:2.
 • Waefeso 2:13, 17.

 

TUFANYE NINI BASI?

 1. Mtu mbaya na aache njia yake
 2. Mtu asiye haki aache mawazo yake
 3. Mtu mbaya na amrudie bwana
 4. Naye [Mungu] atamrehemu;
 5. Mtu mbaya na arejee kwa mungu wetu,
 6. Naye [Mungu] atamsamehe kabisa.

 

Je, Mungu ana Rehema?

 • Kutoka 34:6-7a
  • Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi;

 

Je, Mungu anatoa Msamaha?

 • Isaya 43:25.
  • Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
 • Isaya 44:22.
  • Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa
 • Waefeso 1:7
  • Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.