103-004 Maombi kwa ajili ya Wengine

MFULULIZO WA MASOMO MAFUPI KUHUSU MAOMBI

 

MAOMBI KWA AJILI YA WENGINE

 UTANGULIZI

 • Waumini wanapaswa kuomba, sio tu kwa ajili ya mahitaji yao wenyewe, lakini kwa mahitaji ya wengine pia. Maandiko matakatifu hutoa mifano mingi ya maombezi, na tunashauriwa kushiriki katika tendo hili jema na takatifu kwa sababu tendo hili humpendeza Mungu.

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU:

 • (1) Waumini lazima wathamini wengine
 • (2) Mifano ya kuwaombea wengine
 • (3) Mifano ya maombi mashuhuri ya maombezi (intercession)
 • (4) Mifano ya maombi kwa Yesu Kristo kwa niaba ya wengine
 • (5) Yesu Kristo huombea (intercedes) waumini
 • (6) Roho Mtakatifu huombea (intercedes) waumini
 • (7) Wakristo wanapaswa kuomba kwa ajili ya wengine

 

 SISI KAMA WAUMINI LAZIMA TUTHAMINI WENGINE

 Wafilipi 2:3-4

 • 2 Ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.
 • 3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
 • 4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

MIFANO YA KUWAOMBEA WENGINE

 1. Musa anaomba kwa ajili ya Waisraeli (Torati 9:18-19;Kutoka 32: 9-14; 34: 9; Hesabu 14:11-19; Torati 9:25-29)
 2. Samweli anaomba kwa ajili ya Israeli (1 Samweli 7:5-9; 1 Samweli 12:19-23)
 3. Ayubu anaomba kwa ajili ya rafiki zake (Ayubu 42:10)
 4. Yeremia anaomba kwa ajili ya Yuda (Yeremia 7:16; Yeremia 11:14; 14:11)

 Angalizo: Mungu alimuagiza nabii Yeremia kuomba kwa ajili ya watu wake kwa sababu walikuwa watenda dhambi wasiotubu.

 

MIFANO YA MAOMBI MASHUHURI YA MAOMBEZI (INTERCESSION)

 • (1) Hezekia kwa ajili ya ukombozi (2 Wafalme 19:14-19; Isaya 37: 14-20)
 • (2) Ezra kwa ajili ya safari nzuri na salama (Ezr 8:21-23)
 • (3) Danieli kwa ajili ya Yerusalemu (Danieli 9:1-19)
 • (4) Yesu Kristo kwa ajili ya Wanafunzi Wake (Yohana 17:6-26)
 • (5) Paulo kwa ajili ya waumini kule Efeso (Waefeso 1:15-21; 3:14-21)
 • (6) Paulo kwa ajili ya waumini katika Colosai (Wakolosai 1:9-13)

 

 SISI KAMA WAUMINI YUNAPASWA KUFANYA MAOMBEZI KWA AJILI YA WENGINE

 • (1) Yatupasa kuomba kwa ajili ya maadui zetu (Matayo 5:44)
 • (2) Yatupasa kuomba kwa ajili ya watu wengine
 • (3) Yatupasa kuomba kwa ajili ya watawala (1Timotheo 2:1-2)

 

YATUPASA KUOMBA KWA AJILI YA WATU WENGINE

 •  Waefeso 6:18
  • 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
  • 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote
 • 1 Wathesalonike 5:25
  • “Ndugu, tuombeeni”
 • Filemoni 1: 22
  • Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.
 • Waebrania 13:18-19
  • 18 Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote. 19 Nami nawasihi zaidi sana kufanya hayo ili nirudishwe kwenu upesi.
 • Yakobo 5:14-16
  • 14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
  • 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
  • 16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

 

MIFANO YA MAOMBI YALIYOPELEKWA KWA YESU KRISTO KWA NIABA YA WENGINE

 • Matayo 8:5-13;
 • Luka 7:1-10;
 • Matayo 15:21-28;
 • Mariko 7:24-30;
 • Matayo 17:14-20;
 • Matayo 9:14-29;
 • Luka 9:37-42

 

HUDUMA YA YESU KRISTO SASA: ANADUMU KUWAOMBEA WAUMINI

 • Warumi 8:34
  • Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
 • Isaya 53:12
  • Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
 •  Waebrania 7:25
  • 24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
  • 25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; MAANA YU HAI SIKUZOTE ILI AWAOMBEE.
 •  1 Yohana 2:1
  • 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye MWOMBEZI KWA BABA, YESU KRISTO MWENYE HAKI,
  • 2 Naye ndiye KIPATANISHO kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

 

 

HUDUMA YA ROHO MTAKATIFU SASA: ANADUMU KUWAOMBEA WAUMINI

 •  Warumi 8:26-27
  • 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
  • 27 Na Yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

 • Tuige mfano wa Watakatifu wote katika Biblia
 • Tuige mfano wa Mtume Paulo
 • Tuige mfano wa Kristo Yesu.
 • Tuendelee kudumu katika Maombi, tukiwakumbuka na kuwaombea watu wote.

 

 • Waefeso 1:15-16
  • 15 Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,
  • 16 siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,
 • Matendo 12:5
  • Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.
 • 2 Wakorintho 1:11
  • Ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.
 • 1 Timotheo 2:1
  • Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote.

 

MWITO WA LEO: (NZK # 99 ) “Twende kwa Yesu”

 • Twende kwa Yesu, mimi nawe, Njia atwonya tuijue; Imo chuoni; na mwenyewe,Hapo asema, njoo!
 • Wana na waje, ”atwambia; Furahini mkisikia; Ndiye mwokozi wetu pia, Na tumtii, njoo.
 • Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikwatapo, Ewe kijana, njoo.
  • Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako mwokozi kuonana, Na milele kukaa.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE!

 • Mch. David Partson.