103-003: Kwanini Tuelekeze Maombi Kwa Kristo Yesu?

MFULULIZO WA MASOMO MAFUPI KUHUSU MAOMBI

Kwanini Tuelekeze Maombi Kwa Kristo Yesu?

 • Fungu Kuu: Ufunuo 1:1-8
 • Neno Kuu: ἀποκάλυψις (apokalypsis) =Ufunuo
  • Revelation, what is revealed, a disclosure

Tumizi la neno apokalypsis

 1. Luka 2:32
 2. Warumi 16:25
 3. 1 Wakorintho 1:7; 14:6
 4. 2 Wakorintho 12:1
 5. Wagalatia 1:12
 6. Waefeso 1:17
 7. 2 Wathesalonike 1:7
 8. 1 Petro 1:7
 9. Ufunuo 1:1

 


 

Ufunuo 1:1-8

 • 1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;
 • 2 aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.
 • 3 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.
 • 4 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
 • 5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,
 • 6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.
 • 7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
 • 8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

 


 Ufupisho Wa Somo

MAANDALIZI KWA AJILI YA MAREJEO YA KRISTO.

 • Heri yeye “asomaye”
 • Heri “wao wayasikiao maneno ya unabii huu”
 • Heri hao “wanaoyashika yaliyoandikwa humo”
 • Kwa maana wakati u karibu.

SALAAMU KWA YALE MAKANISA SABA

 • Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia;
 • Neema na iwe kwenu na amani
 • Zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja
 • Na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi

KWANINI TUELEKEZE MAOMBI KWA KRISTO YESU?

 1. Yeye ni Yesu Kristo
 2. Yeye ni Shahidi Aliye Mwaminifu
 3. Yeye ni Mzaliwa Wa Kwanza Wa Waliokufa
 4. Yeye ni Mkuu wa wafalme wa dunia.
 5. Yeye atupendaye
 6. Yeye anayetuosha dhambi zetu katika damu yake,
 7. Yeye anayetufanya kuwa Ufalme
 8. Yeye anayetufanya Makuhani kwa Mungu
 9. Yeye mwenye Utukufu na Ukuu – hata milele na milele. Amina.
 10. Yeye Mfalme ajaye: Tazama, yuaja na mawingu.
 11. Yeye Hakimu ajaye: Na kila jicho litamwona….
 12. Yeye ni Alfa na Omega
 13. Yeye ni Mwanzo Na Mwisho
 14. Yeye ni Bwana Mungu
 15. Yeye ni Aliyeko na Aliyekuwako na Atakayekuja
 16. Yeye ni Mwenyezi.

 

TUFANYE NIN BASI?

(Waebrania 3:1) = Tumtafakari sana Yesu

 • Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,

 

MWITO WA LEO: (NZK # 99 ) “Twende kwa Yesu”

 • Twende kwa Yesu, mimi nawe, Njia atwonya tuijue; Imo chuoni; na mwenyewe,Hapo asema, njoo!
 • Wana na waje, ”atwambia; Furahini mkisikia; Ndiye mwokozi wetu pia, Na tumtii, njoo.
 • Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikwatapo, Ewe kijana, njoo.
  • Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana,
  • Kwako mwokozi kuonana, Na milele kukaa.

(Waebrania 4:14-16)

 • 14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
 • 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
 • 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

TUOMBE:

Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. Amina.

Baba Yetu mpendwa, asante kwa somo hili fupi. Tusaidie tuelewe na kutafakari sifahizi 16 za Kristo Yesu kulingana na aya hii ya Ufunuo 1;1-8. Tusamehe makosa yetu Bwana. Tusaidie tuwe watu wa Maombi. Tunapofunga kipindi hiki sasa, tunajikabidhi mbele Zako. Kaa pamoja na kila mmoja wetu. Wenye shida na changamoto mbalimbali za maisha Bwana, watatulie kulingana na wingi wa Fadhili Zako; wenye njaa na kiu ya Haki, washibishe Bwana. Tusaidie kila siku, kila saa kujiweka tayari kwa ajili ya Marejeo Yako. Tuongezee Imani, tuwe na imani kama ya mtumishi wako Yohana katika kisiwa cha Patmos. Tumeomba haya tukiamini kuwa umesikia, na utatenda sawasawa na Fadhili Zako. Asante, Bwana kwa yote. Tumeomba haya katika Jina Pekee, Jina la Thamani, Jina  la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.