103-002: TABIA SABA ZA MWANA-MAOMBI

MFULULIZO WA MASOMO MAFUPI KUHUSU MAOMBI

 

TABIA SABA ZA MWANA-MAOMBI

Fungu Kuu: 1 Timotheo 6:10-16

Neno Kuu: φεύγω (pheugō): Kuyakimbia

 1. Flee, run away (Mt 24:16; Heb 12:25 )
 2. Escape, avoid danger (Heb 11:34)
 3. Disappear quickly (Rev 16:20)
 4. Avoid, elude (1 Cor 6:18; 2 Tim 2:22)
 5. Become invisible (Rev 16:20)

1 Timotheo 6:10-16

 • 10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
 • 11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.
 • 12 Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.
 • 13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,
 • 14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
 • 15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;
 • 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

 


Ufupisho Wa Somo

TABIA ZA MTU WA MUNGU (MWANA –MAOMBI)

 • Huyakimbia mambo ya Dunia
 • Huitafuta: Haki, Utauwa, Imani, Upendo, Saburi, Upole.
 • Hupiga Vita vile vizuri vya Imani
 • Huungama maungamo mazuri “mbele ya mashahidi wengi”
 • Huilinda “amri hii pasipo mawaa”.
 • Huilinda “amri hii pasipo lawama”
 • Huilinda “hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo”

TUZO YA MTU WA MUNGU (MWANA –MAOMBI)

 • Yeye Kwa Majira Yake
 • Atadhihirishwa

KWANINI TUPELEKE MAOMBI YETU KWA KRISTO?

 • Yeye pekee anahimidiwa
 • Yeye pekee ni “Mwenye uweza”
 • Yeye pekee ni “Mfalme wa wafalme”
 • Yeye pekee ni “Bwana wa mabwana”
 • Yeye pekee “hapatikani na mauti”
 • Yeye pekee “amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa”
 • Wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona.
 • Yeye pekee ana “Heshima na Uweza”
 • Yeye pekee ana Uweza udumuo milele zote
 • Yeye pekee anastahili kuabudiwa Milele zote.

TUFANYE NIN BASI?

 • (1 Timotheo 6:11)
 • Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate HAKI, UTAUWA, IMANI, UPENDO, SABURI, UPOLE.

MWITO WA LEO: (NZK # 99 ) “Twende kwa Yesu”

 1. Twende kwa Yesu, mimi nawe, Njia atwonya tuijue; Imo chuoni; na mwenyewe,Hapo asema, njoo!
 2. Wana na waje, ”atwambia; Furahini mkisikia; Ndiye mwokozi wetu pia, Na tumtii, njoo.
 3. Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikwatapo, Ewe kijana, njoo.

Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako mwokozi kuonana, Na milele kukaa.


 

TUOMBE:

Yeye aliyehimidiwa, Mwenye Uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; ambaye Yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una Yeye hata milele. Amina.

Baba Yetu mpendwa, asante kwa somo hili fupi. Tusaidie tuwe na Tabia hizi Saba kulingana na aya hii ya 1 Timotheo 6:10-16. Tusamehe makosa yetu Bwana. Tusaidie tuwe watu wa Maombi. Tunapofunga kipindi hiki sasa, tunajikabidhi mbele Zako. Kaa pamoja na kila mmoja wetu. Wenye shida na changamoto mbalimbali za maisha Bwana, watatulie kulingana na wing wa Fadhili Zako; wenye njaa na kiu ya Haki, washibishe Bwana. Tusaidie tukaifuate HAKI Yako, na UTAUWA, na IMANI, na UPENDO, na SABURI, na UPOLE. Tuongezee Imani, tuwe na imani kama ya mtumishi wako mtume Paulo. Tumeomba haya tukiamini kuwa umesikia, na utatenda sawasawa na Fadhili Zako. Asante, Bwana kwa yote. Tumeomba haya katika Jina Pekee la Yesu Kristo, aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.