14-10-2016

TGV- CHUMBA CHA MAOMBI

 1. Ijumaa: 14-10-2016

FUNGU KUU: (Matayo 28:19-20)

 • 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
 • 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

 

SIFA & SHUKRANI

 1. Nafasi nyingine ya Uhai Leo
 2. Ahadi ya Uzima wa Milele
 3. Msamaha wa dhambi Zetu
 4. Ushindi dhidi ya dhambi zetu.

MAUNGAMO/ KUKIRI MBELE ZA BWANA.

 1. Kujinyenyekeza mbele za Bwana.
 2. Kuomba
 3. Kuutafuta Uso Wake
 4. Kuziacha Njia Zetu Mbaya
 5. Kuwachukulia wengine kwa Upole

MADA KUU YA MAOMBI YA JUMLA -LEO

 1. Huduma Ya Sauti Ya Injili
 2. Kazi Ya Injili Ulimwenguni Kote

MAHITAJI YA KUOMBEA LEO

 1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.
 1. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.
 1. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)
 1. (ISAAC) Tuwaombee wagonjwa wote, akiwemo rafiki yangu Dabie Goodluck, Yuko India kwa matibabu.
 1. (ISAAC) Naomba muwaombee wadogo zangu: Jacob na Bhoke, Mungu awafanye wawe kama Mungu anavyotaka wawe.
 1. (WAFULA) Niombeeni nipate mchumba.
 1. (DEDITHA) “Mnikumbuke ktk maombi niikiwa uku rikizo, wezi wamevunja chumba  na kuchukua computer na redio.  Watu waliochukua ni majirani;  “mliombee hili wapeta kurudisha
 1. (EMMANUEL) Nami pia nakiri ndugu zangu mniombee MUNGU anipe nguvu ya kushinda dhambi, anifanye jinsi yeye atakavyo! Nimtumikie yeye maisha yangu yote!
 1. (ENOS) “Mniombee kwa changamoto ya kazi wapendwa”
 1. (NIWAEL) Mniombee afya yangu c nzr
 1. (NEEMA) Mniombee naumwa
 1. (UPENDO) Naomba mniombee, mwanangu ameshikwa na homa kuanzia jioni hii anatapika tu. First twin wangu. Wapendwa anaitwa MARTHARITA.
 1. (AWIL) Naomba mnikumbuke katika maombi mimi na familia yangu yote, mtoto wa kaka yangu anasumbuliwa na miguu, katika jitihada tulizofanya kama binadamu,za kwenda kwenye baathi ya hospitali na ķuonana na Madaktari, mtoto amepimwa lakini ugonjwa hauonekani.(mtoto Anaitwa KURWA ).
  1. (IMANI & UJASIRI WA OMBI HILI)
   1. Mungu wetu ajue mambo yote ya sirini, kwa maombi yenu mtoto wetu mpendwa atakuwa mzima na kuyafunua yaliyo juu ya uwezo wetu.
   2. Mubarikiwe munapoungana nami katika kumuombea mtoto wa kaka yangu aitwaye KURWA.
   3. Ili aweze kupona na kuendelea na masomo ,ana umri wa MIAKA SABA.
 1. UTII WA NENO
  1. Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”.
   1. Tutafakari Maonyo Ya Yesu;
   2. Tuungame na Tutubu dhambi zetu,
   3. Tujiweke tayari daima:
  2. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

 

AHADI YA LEO: (Matayo 18:20)

 • 20 Kwa kuwa walipo wawili -watatu wamekusanyika kwa Jina Langu, Nami Nipo papo hapo katikati yao.

 

BWANA ATUBARIKI SOTE.