13-10-2016

TGV- CHUMBA CHA MAOMBI

 1. Alhamisi: 13-10-2016
 2. http://tgvs.org/archives/2022

 

FUNGU KUU: (Isaya 64:8-9)

 • 8 Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u Baba yetu; sisi tu udongo, Nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono Yako.
 • 9 Ee Bwana, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu Wako.

SIFA & SHUKRANI

 1. Nafasi nyingine ya Uhai Leo
 2. Ahadi ya Uzima wa Milele
 3. Ushindi dhidi ya dhambi zetu.

MAUNGAMO/ KUKIRI MBELE ZA BWANA.

 1. Kujinyenyekeza mbele za Bwana.
 2. Kuomba
 3. Kuutafuta uso Wake
 4. Kuziacha njia zetu mbaya
 5. Kuwachukulia wengine kwa Upole

MADA KUU YA MAOMBI YA JUMLA -LEO

 1. Imani, Upendo, Haki Ya Kristo

 

MAHITAJI YA KUOMBEA LEO

 1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.
 1. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.
 1. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)
 1. (ISAAC) Naomba muwaombee wazazi wangu, ndugu zangu, Rafiki Zangu, maadui zangu na majira wote Mungu awadirishe na kuwafanya wawe kama apendavyo yeye
 1. (ISAAC) Tuwaombee wagonjwa wote, akiwemo rafiki yangu Dabie Goodluck, Yuko India kwa matibabu.
 1. (ISAAC) Naomba muwaombee wadogo zangu: Jacob na Bhoke, Mungu awafanye wawe kama Mungu anavyotaka wawe.
 1. (WAFULA) Niombeeni nipate mchumba.
 1. (DEDITHA) “Mnikumbuke ktk maombi niikiwa uku rikizo wamevunja rum na kuchukua computer na redio watu waliochukua ni majiran mliombee wapeta kurudishaa”
 1. (EMMANUEL) Nami pia nakiri ndugu zangu mniombee MUNGU anipe nguvu ya kushinda dhambi, anifanye jinsi yeye atakavyo! Nimtumikie yeye maisha yangu yote!
 1. (ENOS) “Mniombee kwa changamoto ya kazI wapendwa”
 1. (NIWAEL) Mniombee afya yangu c nzr
 1. (NEEMA) Mniombee naumwa
 1. UTII WA NENO– “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

 


AHADI YA LEO: (Waefeso 3:11-12)

 • 11 kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
 • 12 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.

 


TANGAZO:

 1. Tunaendelea kukusanya Mahitaji ya kuombewa siku nzima. Andika hitaji lako nawe Utaombewa.
 1. Angalizo: Sote tunapaswa kuendelea kushiriki katika Maombi bila kukoma.
 1. Jana jioni Viongozi wa Jukwa hili walikutana, kuna maazimio mbalimbali yaliyopitishwa, Hapo baadaye, Katibu wetu (Br. Dancan) ataleta Repoti kamili.

BWANA ATUBARIKI SOTE.