Ushuhuda; October 12, 2016

USHUHUDA WA LEO

Wednesday, 10/12/16    

  1. Napenda kumshukuru Mungu kwa Ulinzi wake juu yangu na kunipigania katika maisha yangu.
  2. Namshukuru MUNGU kwa kunipatia afya njema na uhai maana wengi tulilala nao lakini hawakuamka au ni wagonjwa. Pia familia yangu ameilinda.
  3. Namshukuru Mungu kwa kumponya Shemeji yangu, anaendelea vizuri kidogo….Kwakweli tunasema Asante.

 

MBEYA: (Mchungaji Haruni Kikiwa)

Kanisa la Waadventisa wa sabato Mbalizi la Nusurika Kulipuka Moto hii leo Tarehe 12/10/2016

  • Kanisa la Waadventista wa Sabato Mbalizi Mbeya limenusurika kuwaka moto hii leo Majira ya Saa Tisa Jioni Baada ya Kimbunga kilicho pita eneo hilo  Kuezua Paa la Nyumba ya Jirani na Kanisa na kulitupa juu ya Paa la Kanisa  na Kufunika Waya za Umeme zilizo pita juu ya paa hilo na kusababisha Cheche kali kutokea Hatahivyo Tanesco kupitia Idara ya dharula Waligundua jambo hili mapema na kuzima umeme katika Eneo hilo.
  • Mara Baada ya Kutoa Mabati hayo tumegundua kua Hasara chache zilizo jitokeza kwani Dish la King’amuzi cha Ting limeharibika pia Bati 4 za Kanisa zilichimbwa na kuharibiwa kwa mkito wa Hilo paa.
  • Tunamshukuru Mungu kwani hakuna mtu aliye dhurika katika kimbunga hiki.
  • Pia Tunapenda kukishukuru kitengo cha Dharula cha Tanesco  kwa umakini na Umahili katika kazi yao kwani walichukua hatua mapema na ndani ya Mda mfupi walikuwa wamesha fika katika Tukio hili na kushirikana nasi katika Utoaji wa Paa hilo na hatimaye kurudisha Umeme.

By. Mwanahabari wako Mchungaji Haruni Kikiwa Mchungaji wa Mtaa Mbalizi.