12-10-2016

TGV- CHUMBA CHA MAOMBI

 1. Jumatano: 12-10-2016
 2. http://tgvs.org/archives/2012

 

FUNGU KUU: (Zaburi 55:16-18)

 • 16 Nami nitamwita Mungu, Na Bwana ataniokoa;
 • 17 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
 • 18 Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu, Maana walioshindana nami walikuwa wengi.

 

SIFA & SHUKRANI

Tunamshukuru Mungu kwa mambo yafuatayo:

 1. Kwa kutupa Upendo na Mshikamano humu
 2. Ahadi ya Uzima wa Milele
 3. Ushindi dhidi ya dhambi zetu.
 4. Nabarikiwaa kupitaa maelezoo

MAUNGAMO/ KUKIRI MBELE ZA BWANA.

 1. Kujinyenyekeza mbele za Bwana.
 2. Kuomba
 3. Kutafuta uso Wake
 4. Kuziacha njia zetu mbaya
 5. Kuwachukulia wengine kwa Upole

 

MAHITAJI YA KUOMBEA LEO

 1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.
 1. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.
 1. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)
 1. (ISAAC) Naomba muwaombee wazazi wangu, ndugu zangu, Rafiki Zangu, maadui zangu na majira wote Mungu awadirishe na kuwafanya wawe kama apendavyo yeye
 1. (ISAAC) Tuwaombee wagonjwa wote, akiwemo rafiki yangu Dabie Goodluck, Yuko India kwa matibabu.
 1. (ISAAC) Naomba muwaombee wadogo zangu: Jacob na Bhoke, Mungu awafanye wawe kama Mungu anavyotaka wawe.
 1. (WAFULA) Niombeeni nipate mchumba.
 1. (DEDITHA) “Mnikumbuke ktk maombi niikiwa uku rikizo wamevunja rum na kuchukua computer na redio watu waliochukua ni majiran mliombee wapeta kurudishaa”
 1. (EMMANUEL) Nami pia nakiri ndugu zangu mniombee MUNGU anipe nguvu ya kushinda dhambi, anifanye jinsi yeye atakavyo! Nimtumikie yeye maisha yangu yote!
 1. (ENOS) “Mniombee kwa changamoto ya kazI wapendwa”
 1. UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

 

AHADI YA LEO: (1 Yohana 5:14-15)

 • 14 Na huu ndio ujasiri tulio nao Kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi Yake, atusikia.
 • 15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.

 


TANGAZO:

Kila mmoja wetu anaombwa kumuona Katibu wetu  (Mr. Dancan) ili apangiwe Muda/ Zamu  za maombi. Kila mtu awe huru kusema atakuwa na muda wakati gani ili secretary wetu apange Ratiba husika.

 1. ALFAJIRI (Saa 10-12)
 2. ASUBUHI (Saa 3-5)
 3. MCHANA (Saa 7-9)
 4. JIONI (Saa 11-1)
 5. USIKU (Saa 3-5)

BWANA ATUBARIKI SOTE.

 


Diana Goyayi

 • Baba yetu uketie mahali pa juu, tunakushukuru kwa asubuhi njema asante kwa upendo wako, tujalie asubuhi utuongoze kwa kila jambo naombea wagonjwa wote pande nne za dunia shuka Yesu Kristo mahitaji mbali mbali kiroho kiuchumi wabariki kazi zao na biashara, family zetu uzisimamie, uwezo ni mkubwa tunaamin kila moja utamtendea bariki watu wote duniani tujalie kuwa kama wewe asante ktk jina la Yesu kristo, amen

Upendo John:

 • Baba Mtakatifu Mungu wetu, Asante kwa wema na rehema na huruma zako kwani hatustahili Mungu wetu kuja mbela zako maana tu wachafu kwa mawazo na matendo yetu, lakini Bwana wetu kwa Upendo wako unatupokea na kutukalisha pamoja na wewe na kutusikiliza haja zetu. Jina lako Litukuzwe milele zote. Tusamehe dhambi na makosa yetu Mungu wetu. Nakusihi tena kwa wasaa huu ulionopatia kwa kuleta maombi yetu mbele zako, nakusihii Yesu wetu utujalie sawasawa na mapenzi yako. Namuweka ndugu Niwaeli mbele zako unamjua afya yake naye anaikabidhi kwako wewe uliyemuumbaji wake ili uendelee kumuumba upya kila iitwapo leo kwa Utukufu wako. Mbariki yeye na familia yake kwa Jina la Yesu, naombea pia kundi hili la Chumba cha Maombi Uwe pamoja nasi Mungu wetu kwani unajua Nia zetu na Dhamira zetu ni kuzitakasa njia zetu ili tufae kuitwa Wana na binti zako tangu sasa na hata utakapokuja. Nawaombea kaka Isack unamjua Umkumbuke, na Enos pia mpatie kazi ili aweze kujitoa kuisukuma kazi yako mbele kwa matoleo yake na kukurudishia Sifa na Utukufu. Namuombea pia ndugu Emmanuel Umjaze na Roho wako Mtakatifu ili aweze kuichukia na kuiacha dhambi inayo/zinazo mshinda kwani amekimbilia kwako mahala ambapo ndiko Ushindi juu ya dhambi unapopatikana, angalia kukiri kwake Mungu wetu na Hakika Umeshamshindia katika Jina la Yesu. Mkumbuke pia Deditha mali yake imepotea nawe umetuahidi ulinzi sasa Bwana wetu Utende sasa sawasawa na Neno lako Udhoofishe nafsi hizo zilizoshiriki hadi toba ipatikane ndani yao katika Jina Yesu. Namleta pia ndugu Wafula mbele zako Anahitaji mchumba, naomba umpatie wa kufanana naye kwa Jina la Yesu. Naombea program ya TGV ya kutoa Biblia za kiswahili kwa watu wako hivyo naombea uwaunganishe na mibaraka yako kutoka juu mbinguni ili waweze kutenda ndani ya uwezo wako na wasipungukiwe katika huduma hiyo ili kazi yako iharakishwe na Urudi haraka Yesu wetu. Na uguse mioyo ya watu ili utoaji uimarike katika Jina la Yesu. Naombea na Mpango wa ununuzi wa Vifaa vyote vya Presentation za series za Injili uliopangwa na watoto wako katika kukutumikia na kuipeleka mbele kazi yako ya Injili ili Watu wako waokolewe. Bariki sasa kila hoja iliyoletwa mbele zako kwa Utukufu wa Jina Lako kwani nimeomba kwa Imani kwa Jina la Yesu Kristo. Amina

Dada Sabato:

 • Mtakatifu mtakatifu mtakatifu Mungu mwenye Upendo Asante sana kwa siku hii ya Leo, Asante kwa baraka zako juu ya maisha yetu,
 • Masaa haya ya alasiri tunakuja mbele zako tukiwa wenye dhambi tusiostahili tunaomba utakaso kutoka kwako, tusamehe dhambi na makosa tunayokutenda Bwana ili tufae kuzipaza sauti zako mbele ya kiti chako cha enzi
 • Mungu wetu na Baba yetu tunakuja mbele zako tuko na mahitaji mengi ya kimwili na kiroho twaomba utupatie kadiri ya mapenz yako, kunawagonjwa twawaweka kwako uliyetabibu mkuu waguse Bwana, wenye uchumi ulioshuka wainue Mungu na kuzibarki kazi za kila mmoja ili waweze kuitegemeza kaxi yako Bwana, wanyonge watetee Mungu ili waweze kulitukuza jinalako ee Mungu, wanafunz nao wakumbuke Ktk masomo yao
 • Eé mwenyezi Mungu mtetezi Wa wanyonge tunaomba uziimarishe imani zetu tuwexe simama imara ili unaporud tufae kuingia Ktk paradise yako Mungu tufanye kuwa wanyenyekevu, watiifu. Waaminifu, na watakatifu mbele zako ili wengi watuonapo wakuone we we Ktk maisha yetu tusaidie Mungu tunaomba na kushukuru kwajina La Yesu kristo mwokoz wetu aminaaaa

 

Dada Sabato:

 • Bwana Yesu nakushukuru kwa sababu wewe ni mkuu Asante kwa uwepo wako ndani ya maisha yetu Asante kwa maombi yote yalitoombwa mchsna kutwa Wa Leo na yote yanayiendelea kuombwa hadi sasa naomba uyapokee Bwana
 • Tunajua kuwa hatusatahiri tunaomba utusamehe udhaifu wetu na unyonge wetu tunaoonekana nao mbele yako naomba uturehemu sawa na wingi Wa fadhili zako,
  Usk Wa Leo Bwana nakuonesha wagonjwa tabibu mkuu waguse, wanyonge kristo watetee, wenye changamoto za ndoa ingilia ksti na uisuluhishe migogoro hiyo ili ndoa zikawe mbingu ndogo, wasaidie watumishi wako shambani wape nguvu na uweza Wa kuifanikisha kazi yako maana bila we we hatuwezi lolote, wapatie hekima na roho mtakatifu awafunike na kueavuvia ili wafae kwa utumishi ulinz wako uwe nasi sote na maombi yote yanayoondelea kuombwa yapate kibali usoni pako kwa jina LA Yesu Amina