Ayubu 4

Kitabu cha Ayubu 4

OMBI: Mwenyezi Mungu na Baba yetu mwema wa mbinguni, tunakushukuru sana na kukutukuza kwa namna ya pekee kwa ajili ya ukuu na upendo Wako kwetu! Tunaalika uwepo Wako katika Mfululizo wa Usomaji wa Biblia kwa Mpango. Tunaomba Roho Mtakatifu, katika tafakari ya somo hili, atukirimie hekima ya utambuzi wa sauti Yako na nguvu ya kuitii. Tusaidie kufanya uamuzi wa busara, kila wakati, tukikuchagua Wewe na kuuchagua wokovu. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tubadilishe ili tufanane Nawe. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!

UTANGULIZI:
Sura hii imebeba maelezo ya mwitikio wa kwanza wa Elifazi kwa Ayubu.


 
1 Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,

2 Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya? Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?

  • [Elifazi anamwuliza Ayubu iwapo angependa kupokea ushauri fulani.]

3 Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.

4 Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.

  • [Maneno haya hukiri tabia ya Ayubu ya kuwa na manufaa (Ayubu 29 :12-17; angalia pia Isaya 35:3; Waebrania 12:12).]

5 Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika.

6 Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?

  • [Neno lililofasiriwa kama “matumaini” yanasomeka kama “uzi, kamba”—vifungo ambavyo humshikilia na kumtegemeza Ayubu pamoja na kwamba anakabiliwa na nyakati za fadhaa (5:16; 13:15; 19:10). Elifazi analisema hili kwa usahihi kabisa.]

7 Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?

8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.

9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.

10 Kunguruma kwake simba, na sauti ya simba mkali, Na meno ya simba wachanga, yamevunjika.

11 Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba mke wametawanyika mbalimbali.

  • [Elifazi ana uelewa wenye kasoro kuhusu upatanifu au uwiano wa maisha—kwamba wema hawateseki na kwamba wauvo ndio tu hunaswa katika dhiki.]

12 Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake.

13 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.

14 Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.

15 Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.

16 Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,

17 Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?

18 Tazama, yeye hawategemei watumishi wake; Na malaika zake huwahesabia upuzi;

19 Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao waliosetwa mbele ya nondo!

20 Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa; Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.

21 Je! Kamba ya hema yao haikung’olewa ndani yao? Wafa, kisha hali hawana akili.


 

UFUPISHO WA AYUBU 4

Elifazi ni rafiki wa kwanza wa Ayubu kujibu kuhusiana na maombolezo yake. Rafiki hawa wa Ayubu hawakuwa na maarifa ya Uasi uliotokea kwenye historia ya Mbinguni juu ya mahojiano yanayoelezwa kati ya Shetani na Mungu kuhusu uaminifu wa Ayubu. Hili halikuwepo katika fahamu zao.

Wakati Elifazi akijaribu kulala usiku mmoja, ndipo pepo alipita mbele ya uso wake (aya ya 15). Aliogopa na kutetemeka (aya ya 14). Nywele zake zikasimama na akaruka toka kitandani (aya ya 16). Sauti inayomlaumu Mungu kwamba anasababisha zahama hutukumbusha juu ya kazi aliyoifanya Lusifa katika Uasi Mbinguni. Lengo lilikuwa kutilia mashaka haki ya Mungu.

Maswali ya mashaka yanaimarishwa kwa shutuma dhidi ya Mungu: “Tazama, Yeye [hawaamini] watumishi Wake” (aya ya 18). Ile roho ya lawama bado inaendelea, na huelekezwa dhidi ya Mungu kwamba aliwasingizia “makosa na maovu yote malaika Wake” na kuwafukuzia mbali na mbingu.

Mungu Mpendwa, sisi pia tunakabiliana na majanga mbalimbali. Shetani huwatumia watu wengine na hata mawazo yetu sisi wenyewe ili kutushutumu juu ya uovu ambao ungestahili kuuadhibiwa haraka. Hata hivyo tunajua kuwa Wewe unasemahe, na hatimaye atawazawadia wote ambao ni waaminifu. Tudumishe katika kitanga cha Mkono Wako. Katika Jina la Yesu, Amina.