9-24-2016

TGV- CHUMBA CHA MAOMBI

 

SIFA & SHUKRANI

Ushuhuda mbali mbali toka kwa wana maombi Jana Jioni

Tunamshukuru Mungu kwa mambo yafuatayo:

 1. Nimeona matendo yake makuu maishani mwangu.
 2. Ameniponya na magonjwa kiasi kwamba kwa njia ya kibinadamu haiwezekani.
 3. Nakosa maneno yakuelezea jinsi MUNGU alivyomwema!
 4. Nimekuwa na moyo mwepesi baada ya Ombi la Jana.
 5. Kwa upendo wake kwangu,
 6. Yote mema anayo nitendea ikiwemo uzima na afya tele: Jina la Yesu lipewe sifa
 7. Hakika tukiutafuta uso wake bwana kwa bidiii tutauona
 8. Ananilinda pamoja na udhaifu nilionao namshukuru Sana MUNGU.
 9. Namshukuru kuni/ kutu samehe wote
 10. Ulinzi wake kwetu kwa wiki nzima
 11. Kujibu tayari changamoto tulizoombea awali humu
 12. Ujasiri kuwa atajibu changamoto zilizoletwa leo
 13. Kwa kutupa Upendo na Mshikamano humu
 14. Ahadi ya Uzima wa Milele
 15. Ushindi dhidi ya dhambi zetu.
 16. Nabarikiwaa kupitaa maelezoo

MAUNGAMO/ KUKIRI

 1. Kujinyenyekeza mbele za Bwana.
 2. Kuomba
 3. Kutafuta uso Wake
 4. Kuziacha njia zetu mbaya
 5. Kuwachukulia wengine kwa Upole

MAHITAJI YA KUOMBEA LEO

 1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.
 1. (HEAVENLIGHT) Kuwa imara kiroho
 1. (HEAVENLIGHT) afya ya mwanangu, babangu, na mama, Mungu atuponye magonjwa yetu
 1. (HEAVENLIGHT) Mradi wa shule ninayoiongoza kwa maadili ya Kiadventista, uongozi wa shule uimarike uwe na umoja,  kupata pesa za ukarabati majengo na fanicha.
 1. (HEAVENLIGHT) Pathfinder day itakayofanyika katikati ya mwezi wa kumi shuleni
 1. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.
 1. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)
 1. (ISAAC) Naomba muwaombee wazazi wangu, ndugu zangu, Rafiki Zangu, maadui zangu na majira wote Mungu awadirishe na kuwafanya wawe kama apendavyo yeye
 1. (ADVOCATE) Mniombee imani yangu isitetereke hata ktk magumu na changamoto ninazopitia niendeleee kumtumaini Mungu, lakini Roho Mtakatifu anisadie kumju Mungu wa kweli na Yesu Kristo. (b) Pia Jtatu nina mtihani mniombee
 1. (EMMANUEL) Nami pia nakiri ndugu zangu mniombee MUNGU anipe nguvu ya kushinda dhambi, anifanye jinsi yeye atakavyo! Nimtumikie yeye maisha yangu yote!
 1. UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)