58-029 Ukuhani Mkuu katika Agano la Kale

Silhouettes of Three Crosses
SIFA ZA KUHANI MKUU (Ebr. 5:1-4)
- (1) Lazima atwaliwe kutoka miongoni mwa watu (Ebr. 5:1a)
- (2) Lazima atawazwe/ awekwe wakfu kwa ajili ya mambo yamhusuyo Mungu (Ebr. 5:1b)
- (3) Kazi yake = Lazima atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi (Ebr 5:1 c)
- (4) Lazima awe na zabuni na huruma (katika hisia zake) juu ya wajinga (Ebr. 5:2a)
- (5) Lazima awe na uwezo wa kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, (Ebr. 5:2b)
- (6) Lazima akumbuke kwamba, yeye pia, yu katika hali ya udhaifu; (Ebr 5:2 c)
- (7) Lazima atoe dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe (Ebr. 5:3a)
- (8) Lazima atoe dhabihu kwa ajili ya dhambi za watu wengine (Ebr. 5:3b)
- (9) Lazima akumbuke kutojitwalia mwenyewe heshima hii, (Ebr. 5:4a)
- (10) Lazima AITWE NA MUNGU na kupokea heshima kuhudumu kutoka kwa Mungu, kama vile Haruni alivyoitwa na Mungu. (Ebr. 5:4b)
Waebrania 5:1-4
1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;
2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;
3 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.
4 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.