9-11-2016

Silhouettes of Three Crosses

CHUMBA CHA MAOMBI

CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.

 • Jumapili: September 11, 2016
 1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.
 1. (JOAHARIGO) Bado anumwa (1) meno na miguu; (2) Bintiye Latifa anatafuta kazi
 2. (AIDEN) Kazi ya mikono yake imekuwa na changamoto nyingi, Bwana Aingilie kati
 3. (GETRUDA) Tumuombee mjomba wake ayashinde majaribu
 4. (FLORA) Mama yake anasumbuliwa na Presure
 5. (JUMANNE) Mama yake anaumwa kifua, kila akitumia dawa haponi
 6. (MAMA DAVID) Tumuombee anaumwa
 1. (SIMON) Ombi rasmi kwa mkwe wake ambaye si wa Imani hii – aweze kuamini. (2)Uwezo wa kupata fedha za ununuzi wa Bati & Mbao kwa ajili ya paa yake. (3) Awe mwaminifu katika utoaji wa Zaka na Sadaka. Tumuombee
 1. (SIYAJALI) “tumwombee mtoto Cleopatra ambae analia sana nyakati za usiku, Akilazwa kitandani tu analia utafikir kitanda kina miba”.
 1. (DANIEL) Tumombee mgonjwa wangu “Mispina D. Kasara- anasumbuliwa na akili tangu 1994”.
 1. (HHES STU) Tuombee kitabu cha Utume “The Story of Hope” kiswahili “Pendo Liaison Kifani” tunao mpango kitabu kiwetayari ifikapo October. Tuliweke kwenye maombi.
 1. (CROWN) Anaumwa, tumkumbuke kwa Maombi
 2. (DEVON) Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu
 1. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.
 1. EVANGELISTIC CAMPAIGN: Efforti itakayo anza tarehe 11 -25 September 2016, huko Zimbabwe, ikiongozwa na Mwinjilist mmoja wa TGV, Bwana aingilie kati, bado kuna mapungufu mengi katika Bajeti.
 1. UKWELI WA SABATO –Kulingana na Waebrania Sura ya 4. Naomba maombi yenu Wapendwa: Somo hili ni gumu na bado sijapata cha kusema/ kufundisha watu wa MUNGU. (Kumbuka majukwaa haya ya watu wengi sana wasio wa Imani hii)
 1. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)
 1. Tuombee kuna efoti inaanza jumapili SUMBAWANGA
 1. Naomba mniombee nimefanya interview jana . ilikua ngumu ila naamini Mungu amenipa hiyo kazi. Niombeeni imani yangu ikamilishwe na Bwana. Yani nipokee majibu mazuri.
 1. Jamani tuwaombee wadogo zetu wanaofanya MITIHANI yao ya KUHITIMU ELIMU YA MSINGI.
 1. MUNGU anishindie kila aina ya changamoto katika maisha yangu (ENOCH)
 1. Mimi niombeni mniombee niweze kupata kazi na ninaamini kupitia maombi haya kazi nimepata (MWAMVITA)
 1. UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

USHUHUDA:

 1. Nawashukuru Sana kwa Maombi yenu mdogo Wangu bado Yuko hospitalini ili namshukuru Sana MUNGU Maana anaendelea vizuri
 1. Mfungo wa mwanzo wa mwaka wa sik10, Nilimwombea dada mmoja tuliyekuwa tukiimba naye kwaya aliye kwapua Mme wa MTU, habari njema ni kuwa wamekwisha achana na hawakuzaa mtoto hata mmoja nilikuwa nikimsihi sana aachane na Mme wa MTU ilikuwa ngumu lakin kwa vile nilimwambia wa yasiyo wezekana alitenda jambo juu yake
 1. Mfungo wa siku 3: Niliwaombea ndugu zangu na wazazi wangu MUNGU amefanya kitu pia kaka yangu alie acha kwenda kanisan sasa anakwenda na nimeshangaa sana akinieleza aliichangia kwaya kwenda mtukurà na pia Mzazi wangu mmoja MUNGU amefungua njia kwàn alisema hata nisaidia kwa chochote lakin leo tumeongea naye vyema àmbapo sikutegemea, BWANA naamini anajibu maombi

 

ANGALIZO:

 1. Tukusanye Ushuhuda/ Mahitaji/ Maombi/ Changamoto mbalimbali na kuzipost humu ndani
 2. Tuendelee kutoa Ushuhuda wa matendo makuu Ya Mungu wetu
 3. Kama ombi lako limejibiwa, Tueleze ili tulitowe katika List.

Bwana Atubariki Sote tunapoendela kuombea MAHITAJI YA WENGINE.