Matayo 23:23

DHAMBI YA KUTOTIMIZA WAJIBU (NEGLECT)

Matayo 23:23 (Kiswahili)

 • Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha MAMBO MAKUU YA SHERIA, yaani, ADILI, NA REHEMA, NA IMANI; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

Matthew 23:23 (NKJV)

 • “Woe to you, scribes and Pharisees, hypocrites! For you pay tithe of mint and anise and cummin, and have neglected the weightier matters of the law: justice and mercy and faith. These you ought to have done, without leaving the others undone.

UTANGULIZI

 • Katika fungu hili, Yesu anawalaani Waandishi na Mafarisayo kwa kugeuza vipaumbele vya Mungu. Mafarisayo walitukuza mambo madogo (insignificant) na kupuuza mambo muhimu.

SWALI:

Zaka za mnanaa na Bizari na Jira ndiyo nini?

 • Zaka Za Mnanaa (Tithe Of Mint)
 • Bizari (Anise)
 • Jira (Cummin)

UFAFANUZI WA MATAYO 23:23

 • MNANAA na BIZARI na JIRA zilikuwa mimea ya bustani iliyotumika kama manukato ya jikoni, (kitchen spices); yalikuwa hayachukuliwi kama mazao ya shamba, ambayo sheria ya Musa ililazimu  zaka kulipwa ama kupelekwa katika “hazina” (Mambo ya Walawi 27: 30).
 • Kwa sababu ilisaidia sana shughuli za ukuhani na Hekalu kwa ujumla, zaka ilikuwa kama aina ya kodi fulani.
 • Zaka ya pili (A second tenth)  ililipwa kila mwaka kwa ajili ya msaada wa SHEREHE ZA IBADA mbalimbali na MATAMASHA ya kitaifa (Kumbukumbu la Torati 12:11, 17).
 • Zaka nyingine ilikuwa ikilipwa kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya aina ya ustawi, kusaidia WALAWI, WAGENI, YATIMA na WAJANE (Kumbukumbu la Torati 14:28 – 29), ambayo ilifikia asilimia ziada wa 3.3 kwa mwaka.
 • Kwa maana nyingine, Waisraeli walitakiwa kulipa zaidi asilimia 23 ya mapato yao kila mwaka.

FUNDISHO LA YESU KATIKA MATAYO 23:23

Kwa kifupi sana Waandishi na Mafarisayo, walikazia mambo madogo madogo na wakasahau msisitizo wa mambo makubwa kiroho: “MAMBO MAKUU YA SHERIA, yaani, ADILI, NA REHEMA, NA IMANI”

MAFUNGU YA ZIADA

 1. Matayo 9:13;
 2. Matayo 12:7;
 3. Matayo 22:37–40.
 4. 1 Samweli 15:22.
 5. Mitali 21:3.
 6. Yeremia 22:15, 16.
 7. Hosea 5:6.
 8. Mika 6:8.
 9. Wagalatia 5:22, 23.

Zingatia mafungu hayo hapo Juu na usipuuzie.

Bwana Akubariki