9-8-2016

CHUMBA CHA MAOMBI

CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.

 

 1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.
 1. (JOAHARIGO) Bado anumwa (1) meno na miguu; (2) Bintiye Latifa anatafuta kazi
 2. (AIDEN) Kazi ya mikono yake imekuwa na changamoto nyingi, Bwana Aingilie kati
 3. (GETRUDA) Tumuombee mjomba wake ayashinde majaribu
 4. (FLORA) Mama yake anasumbuliwa na Presure
 5. (JUMANNE) Mama yake anaumwa kifua, kila akitumia dawa haponi
 6. (MAMA DAVID) Tumuombee anaumwa
 1. (SIMON) Ombi rasmi kwa mkwe wake ambaye si wa Imani hii – aweze kuamini. (2)Uwezo wa kupata fedha za ununuzi wa Bati & Mbao kwa ajili ya paa yake. (3) Awe mwaminifu katika utoaji wa Zaka na Sadaka. Tumuombee
 1. (SIYAJALI) “tumwombee mtoto Cleopatra ambae analia sana nyakati za usiku, Akilazwa kitandani tu analia utafikir kitanda kina miba”.
 1. (DANIEL) Tumombee mgonjwa wangu “Mispina D. Kasara- anasumbuliwa na akili tangu 1994”.
 1. (HHES STU) Tuombee kitabu cha Utume “The Story of Hope” kiswahili “Pendo Liaison Kifani” tunao mpango kitabu kiwetayari ifikapo October. Tuliweke kwenye maombi.
 1. (CROWN) Anaumwa, tumkumbuke kwa Maombi
 2. (DEVON) Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu
 1. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.
 1. EVANGELISTIC CAMPAIGN: Efforti itakayo anza tarehe 11 -25 September 2016, huko Zimbabwe, ikiongozwa na Mwinjilist mmoja wa TGV, Bwana aingilie kati, bado kuna mapungufu mengi katika Bajeti.
 1. UKWELI WA SABATO –Kulingana na Waebrania Sura ya 4. Naomba maombi yenu Wapendwa: Somo hili ni gumu na bado sijapata cha kusema/ kufundisha watu wa MUNGU. (Kumbuka majukwaa haya ya watu wengi sana wasio wa Imani hii)
 1. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)
 1. Tuombee kuna efoti inaanza jumapili SUMBAWANGA
 1. Naomba mniombee nimefanya interview jana . ilikua ngumu ila naamini Mungu amenipa hiyo kazi. Niombeeni imani yangu ikamilishwe na Bwana. Yani nipokee majibu mazuri.
 1. Jamani tuwaombee wadogo zetu wanaofanya MITIHANI yao ya KUHITIMU ELIMU YA MSINGI.
 1. MUNGU anishindie kila aina ya changamoto katika maisha yangu (ENOCH)
 1. Mimi niombeni mniombee niweze kupata kazi na ninaamini kupitia maombi haya kazi nimepata (MWAMVITA)
 1. UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

USHUHUDA:

 1. Nawashukuru Sana kwa Maombi yenu mdogo Wangu bado Yuko hospitalini ili namshukuru Sana MUNGU Maana anaendelea vizuri
 1. Mfungo wa mwanzo wa mwaka wa sik10, Nilimwombea dada mmoja tuliyekuwa tukiimba naye kwaya aliye kwapua Mme wa MTU, habari njema ni kuwa wamekwisha achana na hawakuzaa mtoto hata mmoja nilikuwa nikimsihi sana aachane na Mme wa MTU ilikuwa ngumu lakin kwa vile nilimwambia wa yasiyo wezekana alitenda jambo juu yake
 1. Mfungo wa siku 3: Niliwaombea ndugu zangu na wazazi wangu MUNGU amefanya kitu pia kaka yangu alie acha kwenda kanisan sasa anakwenda na nimeshangaa sana akinieleza aliichangia kwaya kwenda mtukurà na pia Mzazi wangu mmoja MUNGU amefungua njia kwàn alisema hata nisaidia kwa chochote lakin leo tumeongea naye vyema àmbapo sikutegemea, BWANA naamini anajibu maombi

ANGALIZO:

 1. Tukusanye Ushuhuda/ Mahitaji/ Maombi/ Changamoto mbalimbali na kuzipost humu ndani
 2. Tuendelee kutoa Ushuhuda wa matendo makuu Ya Mungu wetu
 3. Kama ombi lako limejibiwa, Tueleze ili tulitowe katika List.

 

Bwana Atubariki Sote tunapoendela kuombea mahitaji ya wengine.


 

 

PRAYER SECTION

Debies

Mungu wetu mwema ahsante kwa upendo wako kwetu, ahsante kwa Neema yako bure. Twaomba msamaha wa dhambi zetu. Twaungama mbele zako wakubwa kwa wadogo tuhurumie na kutusamehe Baba. Twaomba utupatie upendo na umoja maishani mwetu, tupatie uaminifu na ujazo wa Roho Mtakatifu maishani mwetu, namleta rafiki yetu Heavenlight ni mgonjwa amasumbuliwa na moyo Yesu. Twaomba umponye kwa jina lako, akapone aweze kuwa na afya njema pamoja na wagonjwa wote popote walipo. Ahsante Yesu kwa mchana wa leo ni katika jina la Yesu, Amina.

Upendo John

Baba Mtakatifu Mungu wetu Uketie mahali pa Juu Mbinguni, Asante kwa wema na neema yako, Asante kwa fadhili na ulinzi wako juu yetu. Jina lako Litukuzwe usiku na mchana, Ufalme wako uje na mapenzi yako yatimizwe hapa duniani na hata mbinguni. Tunaomba Roho wako Mtakatifu atutangulie katika kila jambo tuombalo na tunalolihitaji mbele zako Mungu wetu. Tunakushukuru pia kwa kusikia maombi yetu na kuyakubali na kutujibu sawasawa na mapenzi yako. Asante kwa kuwa umelijibu Ombi la dada Mwamvita kwa kumpatia kazi nzuri, Asante kwa kuwa karibu na kaka Enock kwa kumshindia majaribu yake yote, Asante kwa Ndugu yetu Aliyefanya interview kwa kumpatia kazi mana wewe ni mkuu na utampatia mtoto wako hitaji lake kwa kuwa wewe ni Baba yake na unajua kutupatia vilivyo bora Mungu wangu. Tunaombea uifanikishe efoti ya huko sumbawanga ambayo itaanza jumapili isipungukiwe kitu maana wewe ni Mfalme wa wafalme. Anza kuwaandaa wana na binti zako kukutana na wewe. Wabariki watumishi wako wote wanaojitoa kukutumikia kwa hali na mali Mungu wetu. Naombea pia TGV Bible Project Uwafanikishie maana ni kwa ajili ya kulihubiri Neno lako. Wanahitaji Biblia za kiswahili kwa kuwapatia waumini wapya wanaobatizwa. Tubariki Mungu wetu tukutolee Ee Mungu wetu. Asante kwa kuwa umetusikia na Unakwenda kutenda sawasawa na mapenzi yako. Mungu wangu naomba uruhusu Roho wako Mtakatifu kwa watu wako ili Uinjilisti wa kuitangaza kweli yako, na Sabato yako ufanikiwe ulimwenguni kote hata Yesu ajapo. Baba Mungu naombea pia efoti itakayofanyika huko Zimbabwe na Muongoze mtumishi wako uliyemuandaa kwa ajili ya Utukufu wako na kamilisha mipango yote iliyopangwa na watumishi wako. Wapatie Fedha za kutosha na kuzidi Mungu wetu mana Jina lako ni kuu mno.na lina Uwezo wa kutenda hayo yote. Baba tunaomba kwa Imani kwa Jina la Yesu kristo. Amina.

 

David

Baba yetu na Mungu wetu, Jina Lako Lihimidiwe milele. Asante kwa Nafasi nyingine ya Uhai leo. Asante kwa fursa nyingine uliyotupa kukikaribia kiti chako cha Rehema na Neema nyingi. Asante kwa Uaminifu Wako, Msamaha wa dhambi zetu. Asante kwa Ahadi ya Marejeo Yako.

Naomba kuleta maombi haya mbele Zako. Tunamuombea, mtoto Cleopatra ambae analia sana nyakati za usiku. Namuombea, dada Mispina, anasumbuliwa na ugonjwa wa akili tangu 1994. Bwana huyu amehangaika sana kwa kipindi kirefu, Ebu fanya jambo fulani kwa ajili yake.

Tunaomba pia kwa ajili ya kitabu cha Utume “The Story of Hope” tunaomba mipango ya uchapishaji ikamilike ili kitoke na watu wapate injili. Ndugu yetu, DEVON ana shida fulani, tunaomba ukaingilie kati shida kuu inayomsibu. Bwana tunaleta ombi rasmi kwa ajili ya gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series mbalimbali za Injili. Hatuna fedha lakini maandiko yako wazi kuwa: “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake”. Sisi ni watu na mali yako, na umetupa kazi ya kufanya, Bwana. Tunasema asante in advance kuwa utatupa vitendea kazi ili hii injili isikike Ulimwengini pote. Pia, Bwana, tunakumbuka Efforti itakayo anza tarehe 11 -25 September 2016, huko Zimbabwe, ikiongozwa na Mwinjilist mmoja wa TGV. Tunahitaji Biblia kama 50 hivi, Tubariki tufikie lengo Bwana.

Zaidi ya yote, tusamehe makosa yetu Bwana. Tutakase, tukawe wateule Wako, watakatifu mbele Zako,  “wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu YESU KRISTO kila mahali, Bwana wao na wetu”

Siku itakapo kuja, hebu kila mmoja wetu aonekane akiwemo miongoni mwa watakatifu watakaokulaki Bwana, tutakapo imba na kusema: “Tazama, Huyu Ndiye Mungu Wetu, Ndiye Tuliyemngoja Atusaidie; Huyu ndiye BWANA TULIYEMNGOJA, Na TUSHANGILIE na KUUFURAHIA Wokovu Wake”. Asante, Bwana kusikia maombi haya. Ni katika Jina la Yesu, tumeomba, Amen.


 

Dada Sabato

Mwenyez Mungu mfalme Wa uzima, asante kwa kutulinda siku nzima ya Leo, tunakushukuru sana kwa upendo wako wa agape maishan mwetu

Tunaanguka miguun pako kristo tukiomba utusamehe makosa na dhambi tulizokutenda ,tuumbie moyo safi Bwana tufae kuitwa wana na Bint zako ktk ufalme wako

Muumbaji wetu tunskuja na mahitaji mbalimbali mbele zako, tunaomba utakaso wako juu yetu ili maombi yetu yakapate kibal mbele zako,

Bwana Yesu tunaomba kwa ajiri ya wagonjwa wote, walioko majumban na mshospitalin, na hata waliomo ktk kundi hili kristo uwaguse wote, wajalie afya njema, wapatie amsni wapatie faraja wakazid kulihimid jina lako, Mungu mkuu wapo na wagonjwa wengine ambao magonjwa yao yamesjindikana, yamkini hata wamrkeisha kukata tamaa na hata kujichoka kristo uliye muumbaji wao nyosha mkono wako ulio hodar ukawaguse na kiwaponya maana wewe ni tabibu mkuu

Wengine wanaomba kupata kaz, yamkini yawezekana imepita miaka kadhaa, nahata miez mingi watumishi wako wanaomba kupata kaz Bwana mahali popote wanapo omba kaz na watakapo enda kuomba kaz Bwana ukawapatie kwa uweza wako

Wapo wengine wanaomba uwabarki ktk kaz zao, Mungu gusa kila mlango wanaopita Wateja, uwabarki ktk mapato yao, wengine uchumi wao unayumba Bwana Yesu imarisha mitaji yao na kuikuza wakafanikiwe kwa namna ya pekee wakaliinue jina lako

Mfalme wetu tunaomba kwa wale wote waliojitoa kuifanya kaz yako yawezekana Bwana wanahis kushindwa Bwana wainue , wafadhili, wahekimishe, wapatie busara wakasimame imara kwa ajili ya kaz yako Mungu, lkn pia watumishi wako walioko kazin nao uwakumbuke,
Injil inayo hubiriwa pande kuu za dunia Bwana ikapate kibal uson pako,, watu wako wanaojitoa kujiunga na kanisa lako waimarishe kusimama imara , Tunaomba uvuvio Wa Roho Mtakatifu ndani mwetu atufundishe na kutuonya namna ya kuish ktk kipind hik cha machafuko, ili mwisho Wa safar yetu ukazae matunda yapasayo toba

Mungu wetu, tujalie kudum kwako siku zote za uhai wetu, Wana na Bint zako Bwana uck huu tunaomba utulinde ,Pamoja na familia zetu, ndg zetu, wazazi wetu,jamaa zetu, Aman yako ikayatawale maisha yetu tukadum heman mwako, Litukuzwe milele jina lako tukufu sasa na siku zote ktk jina la Yesu kristo
Ameeeeen


Diana Goyayi

Ombi Baba yetu mtakatifu asante kwa kutulinda tangu asubuhi mpaka mida hii, tuomba utusamehe dhambi zote za wazi na za siri, asante kwa uhai afya na ulinzi na mahitaji, kila mtu ulivyomtendea, tunatanguliza shukrani kwako Yesu kristo uliye kabila la simba wa yuda, Uwezo na nguvu ni mkuu shetani alishashindwa tupo omba tunaamin unaweza Yesu kristo naomba ushuke nyumbani mwetu na majeshi yako ya malaika kuta za nyumba tumezifunika damu ya Yesu kristo na sakafu iwe moto , mtoto anayelia naomba Yesu kristo asilie we unamfunika na damu yako nguo zao vitanda tunavifukia na damu ya Yesu nyumba yote malaika wa mbinguni wafanye msako mtoto alale ktk jina la Yesu kristo Leo siku zote, mgonjwa wa akili nae a pone kuwa huru ktk vifungo vyote, vifaa vinavyoitajika Mungu utendee ili kazi ifike watu waokolewe. Kila shida na mahitaji ya kiafya kiuchumi kiroho ninatuma Ombi hill kwa jina la Yesu kristo neno lake nikiamin Mungu anatenda amen .