67-003: Ufafanuzi Wa Dhambi

MADA MBALIMBALI KATIKA BIBLIA

DHAMBI (sehemu ya 3)

 • Somo La Leo: UFAFANUZI WA DHAMBI
 • 67-003: Ufafanuzi Wa Dhambi
 • http://tgvs.org/archives/1873

OMBI: Baba yetu na MUNGU wetu mwema, Jina Lako Lihimidiwe BWANA. Asante kwa Wema na Fadhili Zako BWANA. Asante kwa nafasi nyingine ya uhai leo. Kabla ya Kuangalia somo hili fupi, tunaalika uwepo Wako katika Mfululizo wa Mada Mbalimbali katika Biblia. Tunaomba ROHO WAKO atufundishe saa hii. Hebu tuwe “watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu”, hali tukijidanganya nafsi zetu”. Tukayatafakari Maonyo Ya KRISTO YESU; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiandae kwa Umilele unaoandaliwa kwa ajili yetu. Asante BWANA, tunakushukuru, na tunakuja katika Jina Pekee La YESU, aliye BWANA na MWOKOZI wetu, Amina.

FUNGU KUU: Yakobo 2:10-11

 • Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. 11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

UFAFANUZI WA DHAMBI

 • 67-003

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU

 1. Dhambi ni Upotoshaji wa makusudi ya Mungu
 2. Dhambi ni Kufanya uovu mbele ya Mungu
 3. Dhambi ni Kushindwa kufikia kiwango
 4. Dhambi ni Kuingia katika Deni
 5. Dhambi ni Uasi Dhidi ya Mamlaka ya Mungu
 6. Dhambi ni Kutanga Mbali na Njia ya Unyofu
 7. Dhambi ni Kuvunja au Kuasi Sheria za Mungu
 8. Dhambi ni Unajisi
 9. Dhambi ni Mwenendo Mwovu

DHAMBI NI UPOTOSHAJI WA MAKUSUDI YA MUNGU

 • Torati 32:5
  • Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.

DHAMBI NI MWENENDO MWOVU

 • Yuda 14-15
  • 14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, 15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu WAMEYANENA JUU YAKE.
 • Isaya 9:17;
  • Kwa sababu hiyo Bwana hatawafurahia vijana wao, wala hatawahurumia yatima zao wala wajane wao; maana kila mtu ni mnajisi, dhalimu, na kila ulimi hunena upumbavu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
 • 1 Timotheo 1:9-10
  • (9) akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji, (10) na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

DHAMBI NI UASI DHIDI YA MAMLAKA YA MUNGU

 • Isaya 30:9
  • Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;

DHAMBI NI KUVUNJA AU KUASI SHERIA ZA MUNGU

 • 1 Yohana 3:4
  • Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa DHAMBI NI UASI.
 • 1 Samweli 13:13-14: (Mfano wa Mfalme Sauli)
  • (13) Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya Bwana, MUNGU WAKO, aliyokuamuru; kwa maana BWANA angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. (14) Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, Naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu Wake, kwa sababu WEWE HUKULISHIKA NENO LILE BWANA ALILOKUAMURU.
 • 1 Nyakati 10:13: (Matokeo ya Kumuasi Mungu)
  • Basi Sauli alikufa kwa sababu ya KOSA LAKE ALILOMKOSA BWANA, kwa sababu ya NENO LA BWANA, asilolishika; na tena kwa KUTAKA SHAURI KWA MWENYE PEPO WA UTAMBUZI, aulize kwake,
 • ANGALIZO:
  • Wapendwa, tijifunze kitu hapo katika kisa hiki cha mfalme Sauli. Dhambi ni mbaya.
  • Dhambi inaondoa mibaraka yote katika Ulimwengu huu, na ule ujao pia.
 • Nehemia 9:29;
  • Ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria Yako; lakini walitakabari, wasizisikilize Amri Zako, bali wakazihalifu Hukumu Zako, (ambazo mtu akizitenda ataishi katika hizo), nao wakayaondoa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza.
 • Mika 7:18;
  • Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? HASHIKI HASIRA YAKE MILELE, kwa maana Yeye Hufurahia Rehema.
 • Yakobo 2:10-11
  • Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. 11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

DHAMBI NI KUTANGA MBALI NA NJIA YA UNYOFU

 • Isaya 53:6;
  • Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
 • Zaburi 58:3;
  • Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
 • Zaburi 95:10;
  • Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile, Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, Hawakuzijua njia zangu.
 • Zaburi 119:10,21,118
  • 10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
  • 21 Umewakemea wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako.
  • 118 Umewakataa wote wazikosao amri zako, Kwa maana hila zao ni uongo.

 

DHAMBI NI KUINGIA KATIKA DENI

 • Matayo 6:12
  • Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
 • Matayo 18:21-35 (saba mara sabini)
  • 21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
  • 22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
  • 23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.
  • 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.
  • 25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.
  • 26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
  • 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
  • 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho.
  • 29 Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
  • 30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.
  • 31 Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
  • 32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
  • 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?
  • 34 Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.
  • 35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

DHAMBI NI KUSHINDWA KUFIKIA KIWANGO

 • Warumi 3:23
  • Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na UTUKUFU WA MUNGU;

DHAMBI NI UNAJISI

 • Zaburi 51:2;
  • Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
 • Isaya 1:16;
  • Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe Mbele Za Macho Yangu; acheni kutenda mabaya;
 • Zaburi 51:7;
  • Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
 • Waebrania 9:14
  • basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?

 

TUFANYE NINI BASI?

 • Zaburi 51:1-4 (Ombi)
  • (1) Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. (2) Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. (3) Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. (4) Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
 • ANGALIZO:
  • Tutubu dhambi zetu, kama mfalme Daudi alivyotubu.
  • Ahadi ya BWANA iko pale pale, kua atatusamehe, na kutuosha kabisa.

SAUTI YA BWANA KWAKO LEO

 • Isaya 1:18
  • HAYA, NJONI, TUSEMEZANE, ASEMA BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa NYEUPE kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama SUFU.

Bwana atubariki sote. Amina