9-6-2016

CHUMBA CHA MAOMBI

CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.
▪Jumanne: September 6, 2016
▪Audios/ Videos/Maandishi (Yote ni sawa)
1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, UJAZO WA ROHO MTAKATIFU, pamoja na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.

2. DADA SCOLA~ “Ambaye kwa kweli anachangamoto mahali anapoishi amekuwa akitofautiana na dada yake ambaye ni mwenye nyumba, na amekuwa akipigwa vita kwani ni mtu wa maombi na ni msabato ila ndugu zake si wasabato na si watu wa ibada bali wanapenda uganga, wamekuwa wakifanya hapo nyumbani. Sasa huyu binti wamemchukia na wameamua kuhama kesho siku ya sabato na hawataki kuondoka nae kwani atakuwa kanisani. Na wamemwambia hawamtaki kwani yeye ndio mchawi. Nimekuwa nikiomba nae kwa karibu kwa muda sasa na hiiyo ndio hali yake ya sasa na hana pa kukaa”. Tumuombeeni wapendwa.

3. KAPOOZA MAGOTI: “Leo nilikuwa nimeenda kumuombea mgonjwa mmoja katika kijiji kimoja, mana baba yake aliniambia mtoto wake kapooza magoti, hayana nguvu yakutembea huu ni mwaka wa pili. Nikamwambia nitamuombea. Kwakweli badaye aliniambia wao ni waislamu ila wameamua kuombewa ili mtoto wao Apone tu, kwani ni kijana wao mkubwa na wao ni wazee na wamehangaika kwa waganga bila mafanikio. Mgonjwa ni mtu mzima na anafamilia. Anaitwa ABDULLAHI. Nimeomba nao na wana imani juu ya Mungu kuwa Ametenda. Napia nimewaambia Mungu akipenda jumatatu nitampeleka kwa matibabu. Hivyo naomba tuiombee hii familia Mungu Aonekane na Awafungulie vifungo vyao na umasikini walionao uishe kabisa kwa Jina Yesu Kristo. Amina”. Asanteni na Mungu awazidishe sana.

4. (JOAHARIGO) Bado anumwa (1) meno na miguu; (2) Bintiye Latifa anatafuta kazi
5. (AIDEN) Kazi ya mikono yake imekuwa na changamoto nyingi, Bwana Aingilie kati
6. (GETRUDA) Tumuombee mjomba wake ayashinde majaribu
7. (FLORA) Mama yake anasumbuliwa na Presure
8. (JUMANNE) Mama yake anaumwa kifua, kila akitumia dawa haponi
9. (MAMA DAVID) Tumuombee anaumwa

10. (SIMON) Ombi rasmi kwa mkwe wake ambaye si wa Imani hii – aweze kuamini. (2)Uwezo wa kupata fedha za ununuzi wa Bati & Mbao kwa ajili ya paa yake. (3) Awe mwaminifu katika utoaji wa Zaka na Sadaka. Tumuombee

11. (SIYAJALI) “tumwombee mtoto Cleopatra ambae analia sana nyakati za usiku, Akilazwa kitandani tu analia utafikir kitanda kina miba”.

12. (DANIEL) Tumombee mgonjwa wangu “Mispina D. Kasara- anasumbuliwa na akili tangu 1994”.

13. (HHES STU) Tuombee kitabu cha Utume “The Story of Hope” kiswahili “Pendo Liaison Kifani” tunao mpango kitabu kiwetayari ifikapo October. Tuliweke kwenye maombi.

14. (CROWN) Anaumwa, tumkumbuke kwa Maombi
15. (DEVON) Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu

16. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.

17. EVANGELISTIC CAMPAIGN: Efforti itakayo anza tarehe 11 -25 September 2016, huko Zimbabwe, ikiongozwa na Mwinjilist mmoja wa TGV, Bwana aingilie kati, bado kuna mapungufu mengi katika Bajeti.

18. UKWELI WA SABATO –Kulingana na Waebrania Sura ya 4. Naomba maombi yenu Wapendwa: Somo hili ni gumu na bado sijapata cha kusema/ kufundisha watu wa MUNGU. (Kumbuka majukwaa haya ya watu wengi sana wasio wa Imani hii)

19. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)

20. UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)

21. Mdogo wake Br. Isaac

22. Familia nyingine iliyotajwa, rejea hapo Juu.

23. Aliyefukuzwa kazi kwa sababu ya Imani yake.

24. Kijana mmoja (mchungaji – Mwanafunzi) wa huko Bugema University, anasumbuliwa na Ada. Tumuombee.
➖➖➖➖➖➖➖➖

MAANDALIZI YA KESHO

  • Tunaombwa kukusanya ushuhuda/ mahitaji/ maombi/ changamoto mbalimbali na kuyapost humu ndani kwa ajili ya maandalizi ya List ya Kesho.
  • BWANA ATUBARIKI SOTE tunapoendela kujiobea na kuombea mahitaji ya wengine.

 


MAOMBI YAFUATAYO YAMETOLEWA NA WAPENDWA WA CHUMBA CHA MAOMBI

 

Zachariah

Baba Yetu Mpendwa Ahsante Kwa Upendo wako Mkuu kwetu,,, Umetulinda uck wa Leo na kutuamsha salama,,, Asubuhi hii njema tunapoona Nuru ya Jua Tunaona Mibaraka yako,,,,

Ombi letu Katika siku ya Leo Anza pamoja nasi Bwana,,, wapo watu Wanahitaji wapate chakula katika siku ya Leo kawapatia sawasawa na Mahitaji yao,,,,, lakini wapo wengine ni Wagonjwa Bwana hebu Mkono wako wa Uponyaji kawaponye BABA yetu,,,, maana wewe ndiye Baba yetu Unayetujali,, wewe ni Baba yetu utulindaye,,ni Baba yetu mwenye Upendo,,, Nasi Bwana tunakuomba Katuumbie UPENDO Kama wako Ee,,Mungu wetu,. Wapo watu wako waliokata Tamaa na Maisha,, Tunakuomba Baba yetu yawe Faraja kwao na Kwa wale waliofiwa na na Wapendwa wao,,,, Mungu Wetu katufundishe kuomba Kama ulivyowafundisha Mitume,,, maana mdomo yetu ni Michafu hata kuomba vizuri hatujui,,, lakini Roho wakotakatifu anapotuombea Kwa Namna isiyotamshika tunaomba Maombi yetu yakakubaliwe mbele zako Baba yetu,,,

Tumebeba Jina lako Takatifu lakini sisi hatusitahili,,, na Maovu yetu yanatushuhudia Sasa Tenda wewe Kwa ajili ya Jina lako,,,

Yeremia alizungumza katika Hiyo Yeremia 14:7

Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, Lakini utende wewe Kwa ajili ya Jina lako,,Eee Bwana,, Maana kurudi Nyuma kwetu ni Kwingi; tumekutenda Dhambi.

Baba tunakusihi Sana Baba yetu hili Group Nifanye kuwa Kusoma cha Maombi na mahari pa kupata Uponyaji,,, wewe Mwenyewe ulituambia,,, Maneno yako wakikaa Ndani yetu Basi Tuombe Lolote nawe atatenda,,,, Sasa Tunakuomba Maneno yako kayapande ndani ya Mioyo yetu na tukawa watu wa Kusoma Sana Neno lako na tukawa watendaji wa Neno,,,, nawe Ukafanye Makazi katika Mioyo yetu,,,,

Tumeomba haya machache Bwana Wetu Kwa Amani ni katika Jina la Yesu Kristo Ameen.


Upendo John:

Mtakatifu Baba Mungu, Tunakushukuru kwa wema na rehema zako, tunashukuru kwa Ulinzi na Fadhili zako pia, Jina lako Litukuzwe mbinguni na duniani. Tunaomba msamaha na ondoleo la dhambi katika maisha yetu. Safisha nia zetu, ziongoze zikuelekee wewe. Tupe uwezo wa kulisoma Neno lako na kulitafakari katika maisha yetu, tufanye kuwa Hubiri kila tunapopita na kuongea katika jamii zinazotuzunguka kwa muonekano, kauli, matendo ya wema na huruma zetu mbele ya jamii zinazotuzunguka, tuwe watu jasiri na wenye Imani kuu. Ili tuimariashe jamii kwa kuipa tumaini jipya juu ya ujio wako Mungu wetu. Asante kwa kusikia Ombi letu na kututendea kwa Jina la Yesu Kristo. Bariki kila mmoja wetu hapa. Zungumza nasi Yesu wetu kwa karibu na upole mwingi. Nakuja mbele zako wakati huu nikikushukuru kwa kila jambo unalonitendea maishani mwangu na kunipa kibali kuja mbela zako muda huu kuleta haja za watoto wako uwapendao, uliowafia pale msalabani. Nitakase kuanzia unyayo wangu hata utosi Ili maombi ya wana na binti zako yaweze kukufikia katika kiti chako cha Enzi hapo juu mbinguni, naomba nikilikabili hekalu lako juu mbinguni na kusema Ondoa huzuni kati ya wana wako. Ondoa mapooza na masikitiko, Ondoa uharibifu wowote ulioletwa na yule mwovu shetani katika Jina la Yesu Kristo. Namuombea Jacob Patric Baba, Umponye ugonjwa wake wa kuchanganyikiwa na akili Mungu, Mpatie Akili zenye Akili na Ufahamu wa juu. Jifunue kwake apate kukujua na kukukiri Yesu wetu. Asante kwa kusikia maombi yetu. Naombea kazi yako ya Injili iende mbele kwa kasi kubwa na wabariki watoto wako wanaojitoa kuimaliza kazi yako kwa kuwamwagia vipawa vya Roho wako Mtakatifu, na kufanikisha kazi yako. Wanahitaji vifaa vya kurushia matangazo, Projector na vinginevyo kwa ajili ya kuliinua Jina lako Yesu wetu. Bariki sasa. Pia tunahitaji kutoa Biblia kwa wanaoamini, wapatie Uwezo wa kutoa huduma hiyo Mungu wetu. Asante Mungu wetu kwa kuwa umetusikia na unatenda sasa kwa Jina la Yesu Kristo. Amina.


 

Debies:

Mungu wetu na Baba yetu jina lako lipewe sifa milele zote, ahsante sana kumtuma mwanao akaja kutukomboa sisi wenye dhambi. Twaomba dhambi zikome maishani mwetu tunaomba tuwe watoto wako waaminifu wa kwel na watiifu kila siku. Ondoa mikosi maishani mwetu, magonjwa yasipate nafas katika miili Yesu. Tuokoe na hila mbaya za mwovu shetani. Ibariki kazi yako ya injili inapohubiriwa watu wa kuone wewe, mchana wa leo shughurika na kila mmoja wetu aliepo hapa, familia zetu ndg na jamaa zetu wasaidie waujue ukwel wa Neno lako. Twaomba tukiamin unakwenda kutenda ni katika jina la Yesu, Amina.


Enoch:

BABA, tunakuitaji tena wakati mwingine huu uliokubarika kwa wana wako na binti zako tuzidi kuzitangaza fadhili zako katika ulimwengu uliopotoka na kuchanganyikiwa, twaja mbele zako kwa namna furan tumekuwa watu wa nia mbili wakati fulan tukikuwakirisha wewe na wakati mwingne tumeliahibisha jina lako tunakusihi ukatusamehe sana,

Twaleta haja zetu tena kwa wakati huu ikiwa kuna mmoja miongoni mwetu anania ya dhati na imani nawe kabisa kwa shida aliyonayo nenda kafanye jambo iwe ni ugonjwa, dhambi, ugumu wa maisha, ada na changamoto zote, yatosha YESU kuendelea kuteseka wakati upo! Hapana MUNGU ni wakati umefika kuzitangaza fadhili zako ndilo ombi letu kwa jina la YESU, amina🙏🏻

 


Advocate Kinja

Haleluya Baba na Mungu wetu, unaeishi juu mbinguni mahali palipo inuka sana, tunalitukuza na kulisifu jina lako takatifu. Tunakushukuru kutupatia nafasi nyingine ya pekee cku ya leo, ckwa nguvu wala uwezo wetu, bali ni neema yako tu. Wapo wengi wenye hekima machoni pako wenye kutenda mapenzi yako, lkn wengine wamelala ucngizi wa mauti, ila cc tusiostahili umetupatia fursa hii adhimu tupo hadi sasa, Baba tunakurudishia sifa heshima na utukufu milele na milele daima.

Baba yetu wa mbingu, cc ni wanyonge wadhaifu tena ni wadhambi tusiostahili hata kuliita jina lako, lkn Baba tunaoujacri kwa ajili ya damu ya thamani uliyomwaga ktk msalaba wa kalvari. Ulikubali kuutoa uhai wako ili cc tucpotee bali tuwe na uzima wa milele, kisha tuwe nao tele. Tunakuja kwako wakati huu tuoshe kwa damu yako, kisha tutakase kwa ile kweli maana neno lako ndilo kweli.

Mungu wetu, tumetanga mbali nawe tuvute kwa kamba za pendo lako, tusaidie kukujua wewe Mungu wa kweli wa haki na Yesu Kristo uliyemtuma kuja kuukomboa ulimwengu, ingawa tupo kanisani kwa miaka mingi lkn bado hatujakujua kweli kweli. Tusaidie kwa njia ya Roho Mtakatifu ambae ndie msaidizi wetu tunaomba atutie ktk kweli yote ili tuliishi neno lako, kisha wengine wavutwe kwako kupitia tabia yetu njema tuliyoaksi kutoka kwako.

Mungu wetu mwema, kwa cku nzima ya leo wana na binti zako tumeleta haja zetu kwako maana tunajua wewe ndie Mungu wetu ubaesikia na kujibu haja za miyo yetu, tenda hivyo kwa utukufu wa jina lako. Watoto wako wanalia ucku na mchana, magonjwa yanatuandama, shida za dunia zibatusonga, wengibe kukata tamaa, wengine masomoni, makazini biashara zetu, hali ngumu ya uchumi na vipato, tunakuomba ingilia kati maana pasipo wewe hatuwezi neno lolote.

Baba, wewe watujua hata kabla hatujaja wewe wajua shida zetu, lkn hata kuomba hatujui tufundishe kuomba na Roho wako Mtakatifu yeye anaetuombea tena anaugua kusikoweza kuelezeka na ayageuze maombi yetu yawe manukato safi ktk kiti chako cha enzi nawe ututendee sawasawa na fadhili zako.

Naungana na maombi ya watumishi wako pamoja na ombi hili, unganisha Bwana ili haja zetu zipate majibu na jina lako litukuzwe.

Kwa mahitaji, shida magonjwa tunakusihi kwa neno moja tu kila mmoja atapokea sawasawa na hitaji lake, tenda hivyo nakuzidi. Imarisha imani zetu hata changamoto tubazopitia zisitukatishe tamaa bali zitufanye tukulilie wewe daima na kuunganishwa mioyo yetu nawe, kisiwepo chochote cha kututenga nawe maana tumekutegemea tusiabike milele.

Ucku tunapokwenda kulala, tunaomba ulinzi wako thabiti ukawe pamoja nasi, tutakapoamja asbh tukiwa wazima wa afya tulisifu jina lako. Ndilo ombi letu kwa imani tumeomba kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu amina.