67-002 Tabia Ya Wenye Dhambi

MADA MBALIMBALI KATIKA BIBLIA

Mada Kuu: DHAMBI (sehemu ya 2)

 

OMBI: Baba yetu na MUNGU wetu mwema, Jina Lako Lihimidiwe BWANA. Asante kwa Wema na Fadhili Zako BWANA. Asante kwa nafasi nyingine ya uhai leo. Kabla ya Kuangalia somo hili fupi, tunaalika uwepo Wako katika Mfululizo wa Mada Mbalimbali katika Biblia. Tunaomba ROHO WAKO atufundishe saa hii. Hebu tuwe “watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu”, hali tukijidanganya nafsi zetu”. Tukayatafakari Maonyo Ya KRISTO YESU; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiandae kwa Umilele unaoandaliwa kwa ajili yetu. Asante BWANA, tunakushukuru, na tunakuja katika Jina Pekee La YESU, aliye BWANA na MWOKOZI wetu, Amina.


TABIA YA WENYE DHAMBI

Muhtasari Wa Somo

 1. Wanakuwa wajasiri kushuhudia/ kushangilia dhambi.
 2. Wanatamani kushirikisha wengine katika dhambi zao
 3. Wao ni wapumbavu
 4. Wao ni walengwa (subjects) wa ghadhabu ya Mungu

 

WANAKUWA WAJASIRI KUSHUHUDIA/ KUSHANGILIA DHAMBI.

 • Zaburi 12:8
 • Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

WANATAMANI KUSHIRIKISHA WENGINE KATIKA DHAMBI ZAO

 • Mwanzo 3:6
 • Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

WAO NI WAPUMBAVU

 • Zaburi 14:1-3
  • 1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. 2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. 3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
 • Zaburi 14:4
  • Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana.

WAO NI WALENGWA WA GHADHABU YA MUNGU

 • Torati 9:7 – 8
  • 7 Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana   8 Tena mlimkasirisha Bwana katika Horebu, BWANA AKAKASIRIKA NANYI hata Akataka Kuwaangamiza.
 • Torati 9:18 – 19
  • 18 Nikaanguka nchi mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyokosa, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kwa kumkasirisha. 19 Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio ALIYOWAKASIRIKIA BWANA kutaka kuwaangamiza. Lakini Bwana alinisikiza wakati huo nao.
 • 2 Nyakati 19:1 – 2
  • 1 Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi Yerusalemu nyumbani kwake kwa amani.  2 Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao Bwana? Kwa ajili ya hayo GHADHABU I JUU YAKO itokayo kwa BWANA.
 • 2 Nyakati 19:9 – 10
  • 9 Akawaagiza, akasema, Ndivyo mtakavyotenda kwa hofu ya Bwana, kwa uaminifu, na kwa moyo kamili. 10 Na kila mara watakapowajia na teto ndugu zenu wakaao mijini mwao, kati ya damu na damu, kati ya torati na amri, sheria na hukumu, mtawaonya, wasiingie hatiani mbele za Bwana, MKAJILIWA NA GHADHABU ninyi na ndugu zenu; fanyeni haya wala hamtakuwa na hatia.
 • 2 Nyakati 36: 15 – 16
  • 15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;  16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi GHADHABU YA BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
 • Ezekieli 7:8
  • 8 basi hivi karibu nitamwaga Ghadhabu Yangu juu yako, nitazitimiza hasira Zangu juu yako, Nami Nitakuhukumu Sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.
 • Ezekieli 20:13
  • 13 Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, wakazikataa hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda; na Sabato Zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga HASIRA YANGU JUU YAO jangwani, ili niwaangamize.
 • Ezekieli 22:29 – 31
  • 29 Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang’anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki.  30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.  31 Kwa sababu hiyo nimemwaga Ghadhabu Yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa Hasira Yangu; Nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.
 • Ezekieli 36: 16 – 18
  • 16 Tena, neno la Bwana likanijia, kusema,  17 Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake. 18 Kwa hiyo Nalimwaga Hasira Yangu juu yao, kwa ajili ya damu waliyoimwaga juu ya nchi, na kwa sababu wameitia uchafu kwa vinyago vyao.
 • Warumi 1:18
  • Kwa maana GHADHABU YA MUNGU IMEDHIHIRISHWA KUTOKA MBINGUNI juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
 • Warumi 2:5
  • Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea AKIBA YA HASIRA kwa SIKU ILE YA HASIRA na UFUNUO WA HUKUMU YA HAKI ya MUNGU,
 • Warumi 2:8
  • Na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata Hasira Na Ghadhabu;
 • Warumi 13:3 – 4
  • 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, OGOPA; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, Amlipizaye Kisasi Mtenda Mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
 • Waefeso 2:3
  • ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
 • Waefeso 5:5 – 6
  • 5 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo Hasira Ya Mungu Huwajia Wana Wa Uasi

TUFANYE NINI BASI?

 • Wakolosai 3:5 – 6
  • 5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;
 • Yohana 3:36
  • 36 Amwaminiye Mwana yuna Uzima Wa Milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali Ghadhabu Ya Mungu Inamkalia.

 

WITO WA LEO.

 • Tumwamini KRISTO YESU, Tuachane na dhambi zetu, Twende Kwake, naye amehaidi kutupa Ushindi dhidi ya dhambi.

 

SAUTI YA KRISTO YESU:

“(1) Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye Haki, (2) Naye Ndiye Kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote”. [1 Yohana 2:1-2]

Bwana Atubariki Sote! Amina.