67-001 Mambo mawili ya msingi kuhusu Dhambi

MADA MBALIMBALI KATIKA BIBLIA

  • 67-001 Dhambi (sehemu ya 1)

OMBI: BABA yetu na MUNGU wetu mwema, Jina Lako Lihimidiwe BWANA. Asante kwa Wema na Fadhili Zako BWANA. Asante kwa nafasi nyingine ya uhai leo. Kabla ya Kuangalia somo hili fupi, tunaalika uwepo Wako katika Mfululizo wa Mada Mbalimbali katika Biblia. Tunaomba ROHO WAKO atufundishe saa hii. Hebu tuwe “watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu”, “hali tukijidanganya nafsi zetu”. Tukayatafakari Maonyo Ya KRISTO YESU; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiandae kwa Umilele unaoandaliwa kwa ajili yetu. Asante BWANA, tunakushukuru, na tunakuja katika Jina la YESU, aliye BWANA na MWOKOZI wetu, Amina.

MUHTASARI WA SOMO LA LEO

Mambo mawili ya msingi kuhusu dhambi

  1. Dhambi zote hutendwa dhidi ya Mungu
  2. Dhambi kimsingi ni ukosefu wa imani katika Mungu

 

DHAMBI ZOTE HUTENDWA DHIDI YA MUNGU

Zaburi 51: 4

  • Nimekutenda dhambi Wewe peke Yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

Mwanzo 13:13;

  • Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.

Kutoka 10:16;

  • Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni haraka; akasema, Nimemfanyia dhambi Bwana, Mungu wenu na ninyi pia.

Waamuzi 10:10;

  • Ndipo wana wa Israeli wakamlilia Bwana, wakisema, Sisi tumekufanyia dhambi, kwa sababu tumemwacha Mungu wetu, na kuyatumikia Mabaali.

Zaburi 41:4;

  • Nami nalisema, Bwana, unifadhili, Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.

Luka 15:18

  • Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;

 

DHAMBI KIMSINGI NI UKOSEFU WA IMANI KATIKA MUNGU

Warumi 14:23

  • Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Waebrania 11:6

  • Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

 

TUFANYE NINI BASI?

Yohana 1:8-9

  • (8) Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. (9)Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

BWANA ATUBARIKI SOTE