9-4-2016

CHUMBA CHA MAOMBI

CHANGAMOTO TUNAZOZIOMBEA LEO HII.
Jumapili: September 4, 2016

 
1. UPENDO, UMOJA, MSAMAHA, UTAKASO, na UAMINIFU wa Members wote wa Timu hii ya Chumba Cha Maombi, ili wawe waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ya Kuomba na Kuombea wengine.

2. DADA SCOLA~ “Ambaye kwa kweli anachangamoto mahali anapoishi amekuwa akitofautiana na dada yake ambaye ni mwenye nyumba, na amekuwa akipigwa vita kwani ni mtu wa maombi na ni msabato ila ndugu zake si wasabato na si watu wa ibada bali wanapenda uganga, wamekuwa wakifanya hapo nyumbani. Sasa huyu binti wamemchukia na wameamua kuhama kesho siku ya sabato na hawataki kuondoka nae kwani atakuwa kanisani. Na wamemwambia hawamtaki kwani yeye ndio mchawi. Nimekuwa nikiomba nae kwa karibu kwa muda sasa na hiiyo ndio hali yake ya sasa na hana pa kukaa”. Tumuombeeni wapendwa.

3. KAPOOZA MAGOTI: “Leo nilikuwa nimeenda kumuombea mgonjwa mmoja katika kijiji kimoja, mana baba yake aliniambia mtoto wake kapooza magoti, hayana nguvu yakutembea huu ni mwaka wa pili. Nikamwambia nitamuombea. Kwakweli badaye aliniambia wao ni waislamu ila wameamua kuombewa ili mtoto wao Apone tu, kwani ni kijana wao mkubwa na wao ni wazee na wamehangaika kwa waganga bila mafanikio. Mgonjwa ni mtu mzima na anafamilia. Anaitwa ABDULLAHI. Nimeomba nao na wana imani juu ya Mungu kuwa Ametenda. Napia nimewaambia Mungu akipenda jumatatu nitampeleka kwa matibabu. Hivyo naomba tuiombee hii familia Mungu Aonekane na Awafungulie vifungo vyao na umasikini walionao uishe kabisa kwa Jina Yesu Kristo. Amina”. Asanteni na Mungu awazidishe sana.

4. (JOAHARIGO) Bado anumwa (1) meno na miguu; (2) Bintiye Latifa anatafuta kazi
5. (AIDEN) Kazi ya mikono yake imekuwa na changamoto nyingi, Bwana Aingilie kati
6. (GETRUDA) Tumuombee mjomba wake ayashinde majaribu
7. (FLORA) Mama yake anasumbuliwa na Presure
8. (JUMANNE) Mama yake anaumwa kifua, kila akitumia dawa haponi
9. (MAMA DAVID) Tumuombee anaumwa

10. (SIMON) Ombi rasmi kwa mkwe wake ambaye si wa Imani hii – aweze kuamini. (2)Uwezo wa kupata fedha za ununuzi wa Bati & Mbao kwa ajili ya paa yake. (3) Awe mwaminifu katika utoaji wa Zaka na Sadaka. Tumuombee

11. (SIYAJALI) “tumwombee mtoto Cleopatra ambae analia sana nyakati za usiku, Akilazwa kitandani tu analia utafikir kitanda kina miba”.

12. (DANIEL) Tumombee mgonjwa wangu “Mispina D. Kasara- anasumbuliwa na akili tangu 1994”.

13. (HHES STU) Tuombee kitabu cha Utume “The Story of Hope” kiswahili “Pendo Liaison Kifani” tunao mpango kitabu kiwetayari ifikapo October. Tuliweke kwenye maombi.

14. (CROWN) Anaumwa, tumkumbuke kwa Maombi
15. (DEVON) Tumuombee Mungu aingilie kati shida kuu inayomsibu

16. (PROJECTOR) Ombi maalumu kuhusu gharama za ununuzi wa Projector/ Screen Yake/ Video Camera, kwa ajili ya Presentation za Series za Injili.

17. EVANGELISTIC CAMPAIGN: Efforti itakayo anza tarehe 11 -25 September 2016, huko Zimbabwe, ikiongozwa na Mwinjilist mmoja wa TGV, Bwana aingilie kati, bado kuna mapungufu mengi katika Bajeti.

18. UKWELI WA SABATO –Kulingana na Waebrania Sura ya 4. Naomba maombi yenu Wapendwa: Somo hili ni gumu na bado sijapata cha kusema/ kufundisha watu wa MUNGU. (Kumbuka majukwaa haya ya watu wengi sana wasio wa Imani hii)

19. TGV BIBLE PROJECT –Jitihada za kupata Biblia za Kiswahili kwa ajili ya Waumini wapya wanaobatizwa kila mwezi na kujiunga na Imani hii ya Waadventista Wasabato, lakini hawana Biblia. (Ombi hili limelewa na Wachungaji mbalimbali)

20. UTII WA NENO- “Lakini iweni watendaji wa NENO, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu”. Tutafakari Maonyo Ya Yesu; Tuungame na Tutubu dhambi zetu, Tujiweke tayari daima: “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”. (Yakobo 1:22; Luka 21:36)


 

NOTE: Tuko Watu 20, kila mtu achague Ombi 1 la Kuombea kwa kina. (Ingependeza kama kila mtu angekuwa na Namba ya kudumu: mfano No. 1 –No.20 – Lakini tutajadili hili pia)

MAANDALIZI YA KESHO

  • Tunaombwa kukusanya ushuhuda/ mahitaji/ maombi/ changamoto mbalimbali na kuyapost humu ndani kwa ajili ya maandalizi ya List ya Kesho. BWANA ATUBARIKI SOTE tunapoendela kujiobea na kuombea mahitaji ya wengine.

,,