9-3-2016

Ombi limetolewa na Mr. Fares Kasubi

Mungu wetu na Baba yetu tunakushukuru sana kuwa pamoja nasi umetulinda tangu siku ya kwanza mpaka sasa hivi siku ya saba, hakuna mwema kati yetu ila ni kwa rehema zako tu umetuwezesha kufika hapa.

Tu wadhambi nasi tumekuwa wakosaji kila siku, tuhurumie Mungu wetu, Wakati mwingine tunasahau kutenda mema kwa ndugu zetu na jamaa zetu, Wakati mwingine twatenda dhambi kwa ukaidi yoote hayo yanamrudisha Kristo msalabani Baba tusameheane sana anza nasi upya asubuhi ya leo, tubatize kwa Roho wako mwema tufanye kuwa viumbe vipya ndani ya Kristo ili siku ujapo mara ya pili aaiwepo miongoni mwetu atakayepotea bali wote tuurithi uzima wa milele…

Ninawaweka wagonjwa wote mikononi mwako akiwepo rafiki yetu mpendwa na ndugu yetu Dabies, Mungu ona machozi yake yanakulilia akiomba msaada kwako alikuwa na uwezo wa kwenda kwa waganga ama sehemu nyingine lakini kule aliona ni ubatili ameamua kubaki miguuni pako akiamini waweza sasa Baba ebu mguse ili adui apate kuaibika maumivu yake yakakome kwa jina la Yesu hata yule ndugu aliyeenda kutembelewa na dada yetu Upendo naye pia asubuhi ya leo unapogusa mahitaji ya watoto wako mguse naye pia apokee uponyaji…
Nasi tupatie upendo, nguvu na uwezo wa kutenda kazi yako tusaidie kufikia malengo ya kimbingu ili tuishi sawa sawa na mapenzi yako.
Asante Mungu wa milele maana umesikia tumeomba na kuamini kwa jina la Yesu ameen.


 

Ombi limetolewa na Ms. Upendo John

Mtakatifu Mungu wetu, Uketie mahali pa Juu sirini, Asante kwa Upendo wako Mkuu, Asante kwa kutuamsha tungali hai tena katika siku hii ya leo Sabato yako Takatifu, tupe macho ya Kiroho tuone Utakatifu wako na tujifunze kuishi maisha Matakatifu kama wewe Mungu wetu ulivyo. Tunaomba kaa nasi Bwana, andaa mioyo yetu kwa kutaniko kuu mbele zako tangu sasa na hata milele. Tunaomba Roho wako Mtakatifu Awe nasi siku zetu zote za maisha haya. Ili Atuwezeshe kuifikia ile mede siku ya mwisho Yesu Utakapokuja kutuchukua. Ondoa makwazo kati ya wana na binti zako, leta Amani, Umoja, Upendo, Uvumilivu, Maelewano, Ushirikiano, Roho ya kunia mamoja Ukitungoza wewe Mungu wetu kupitia Roho wako Mtakatifu Ambaye Ulituahidi kuwa Utatuletea ili tuweze kuishi sawasawa na mapenzi yako. Tupe mioyo ya kuachilia na kusamehe, tupe mioyo ya kutiana moyo kwani safari ni ngumu na vikwazo ni vingi Baba yetu, lakini Upendo wako husitiri haya yote, Tupe sasa Pendo lako tukae ndani yake.

Asanta Baba Mungu wetu, kwakuwa umetusikia na kutujibu, Injili yako ulimwenguni kote inapoendelea Mungu wetu tunaomba Roho wako Mtakatifu awaguse wana na binti zako waijue kweli yako kila kukicha. Bariki watoto wako na Mibaraka ya Sabato, Hakika Furaha ya Sabato ikamfie kila mmoja wetu na iwe Ushuhuda kwetu. Tupe mioyo,roho za kujishusha na kujinyenyekesha, kuheshimu Ibada zetu. Ili maombi yetu yaweze kukufikia Katika Kiti chako cha Enzi mbinguni na kutujibu maombi tuyaombayo. Wote ambao wamekuletea shida na mahitaji yao, tunakuomba uwakumbuke katika siku ya leo. Maana leo ni siku ya Uponyaji.

Asante Yesu wetu kwa Huruma na Rehema Zako kutukubali nakutupokea kama tulivyo, Jina lako Litukuzwe.

Tuna Amini kuwa yote tuliyokuomba Utatujibu na Kuzidi kwani tunaomba kwa Imani kwa Jina la Yesu Kristo. Amina.