9-2-2016

CHANGAMOTO ZA WATU BINAFSI:

1. (Sarah) Katika matokeo yake ya Chuo, kuna somo amepungikiwa poit 2, ameshauriwa ku appeal. Tumombee
2. (Milembe) Hana kazi, amejaza application nyingi za kazi.
3. (Joaharigo) 1. Anumwa meno na miguu; (2) Bintiye Latifa anatafuta kazi
4. (Aiden) Kazi ya mikono yake imekuwa na changamoto nyingi, Bwana Aingilie kati
5. (Getruda) Tumuombee mjomba wake ayashinde majaribu
6. (Flora) Mama yake anasumbuliwa na Presure
7. (Jumanne) Mama yake anaumwa kifua, kila akitumia dawa haponi
8. (Shingashinga) 1. Awe miongoni mwa watakaochaguliwa; (2) Gharama za Chuo: Ada; (3) Changamoto za familia yake: Wazazi wake.
9. (Simon) Ombi rasmi kwa mkwe wake ambaye si wa Imani hii – aweze kuamini. (2)Uwezo wa kupata fedha za ununuzi wa Bati & Mbao kwa ajili ya paa yake. (3) Awe mwaminifu katika utoaji wa Zaka na Sadaka. Tumuombee
10. (Siyajali) “tumwombee mtoto Cleopatra ambae analia sana nyakati za usiku,!akilazwa kitandani tu analia utafikir kitanda kina miba”.
11. (Daniel) Tumombee mgonjwa wangu “Mispina D. Kasara- anasumbuliwa na akili tangu 1994”.
12. (HHES STU) Tuwaombee HHES (timu ya Wainjilisti wetu) “katika mipango yao ya upelekaji Injili kwa njia ya vitabu”.
13. (HHES STU) Tuombee kitabu cha Utume “The Story of Hope” kiswahili “Pendo Lisilo Kifani” tunao mpango kitabu kiwetayari ifikapo October. Tuliweke kwenye maombi.


 

TUOMBE WAPENDWA:

MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU; MUNGU MWENYEZI; Jina Lako lihimidiwe. Asante BWANA kwa nafasi nyingine ya uhai Leo. Katika mapambazuko haya twaja tena mbele Zako, tukihitaji kuliita Jina Lako, Tukihitaji kutafuta Uso Wako.

Asante kwa tabia Yako isiyobadilika. Wewe ni “BWANA, BWANA, MUNGU mwingi wa huruma, Mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, Mwingi wa rehema na kweli; Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, Mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si Mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne”

Asante kwa Huruma Yako, tunakumbushwa katika maandiko kuwa: “Bali MUNGU aonyesha Pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa KRISTO alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa Haki katika DAMU YAKE, tutaokolewa na ghadhabu kwa Yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na MUNGU kwa mauti ya Mwana Wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika Uzima Wake”.

Asante BWANA kwa Upendo huu mkuu, Asante kwa msamaha wa dhambi zetu, Asante kwa Upatanisho, Asante kwa Utakaso Wako, Asante kwa sababu Kristo ni Mbadala Wetu.

Asubuhi ya Leo tuna mizigo mizito tunayoileta kwako. Changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto Wako, kote Ulimwenguni. Tunaombe pia, kazi ya Injili kote Ulimwenguni. Ulituamuru ukisema: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”

Tunaomba uwe pamoja na waalimu wetu katika majukwaa haya ya Injili. Hatutasahau kuwaombea: wachungaji, wazee wa makanisa, waimbaji, watendakazi wote wa Kanisa popote walipo.

Tusaidie tuwe na utambuzi wa nyakati tunazoishi, tukumbushe kuhusu mwito wetu mtakatifu uliotuitia BWANA. Tusamehe makosa yetu. Tutakase BWANA. Tubatize upya kwa ROHO Wako MTAKATIFU.

Katika siku hii, watoto Wako wanapofanya maandalizi ya kina ili kukutana Nawe, tunaomba uwatakase mioyo yao pia, ili watakaposhiriki mibaraka katika Sabato Yako takatifu, waweze kusema: “Atukuzwe BWANA, MUNGU wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu Wake, na kuwakomboa”

Asante BABA kwa yote. Tumeomba haya tukiamini kuwa utatenda sawasawa na Mapenzi Yako. Tunakushukuru, na twaja katika Jina Pekee la BWANA na MWOKOZI wetu-YESU KRISTO, Amen.