2. Kwa nini ni muhimu kujifunza kujifunza Maandiko Matakatifu?

🌎🌎🌎🌎🌎🌎🌎🌎🌎🌎
πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯πŸ’₯ πŸ’₯πŸ’₯
MLIPUKO WA INJILI

TAFAKARI YA MAANDIKO MATAKATIFU

πŸ“•πŸ“•πŸ“•πŸ“•πŸ“•πŸ“•πŸ“•

Ndugu mpendwa naomba kwa mara nyingine tena kukuarika kwenye tafakari ya Neno la Mungu katika jioni hii nyingine tena. Ninatumaini somo hili nalo litakubariki pia.

SIKU YA 2: KWA NINI NI MUHIMU KUJIFUNZA MAANDIKO MATAKATIFU?πŸ™‡
🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌🌌

✍Nianze kwa kusema kuwa watu wengi wanaposhauriwa kujifunza Maandiko Matakatifu mara nyingi hutoa udhuru😰. Mara kwa mara utasikia majibu haya:
➑ “Mimi nina mambo mengi muhimu ya kufanya, kwa nini nipoteze muda wangu kujifunza biblia? Muda wangu hautoshi hata wa kufanya mambo mengine muhimu. Hata hivyo huwa nakwenda kanisani au msikitini.”

πŸ˜’Hivi ndivyo wasemavyo wengi unapowaambia kujifunza Maandiko Matakatifu.

➑ Yesu alisema β€œKwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?” Mathayo 16:26
➑ Watu wengi wamepoteza kila chembe ya fahamu ya kusudi la maisha haya, ukomo wake na umuhimu wa kuyaandaa maisha ya umilele wao. Wamepoteza kabisa fahamu juu ya haya, ingawa ni ya muhimu sana.

➑ Hebu tafakari kisa hiki:πŸ€”
β€œMzungu mmoja aliyekuwa amepoteza ramani yake ya Tanzania alikuwa akisafiri kwa gari lake toka Dar kwenda kupanda mlima Kilimanjaro na hakuwa makini kusoma vibao vya barabaraniπŸ˜’. Alipofika njia panda ya Chalinze hakuelewa njia ya kupita. Mara aliwaona watu 2 wamevaa suti😳 wakipita karibu naye akawauliza. Walimwelekeza aendelee na barabara ya Morogoro (uelekeo wa Magharibi badala ya Kaskazini). Watu wale wakamhakikishia kuwa atafika Kilimanjaro😊. Aliwaamini na mara akaanza safari. ALIKUWA AMEPOTEA”

πŸ‘‰